Elections 2010 Hatimaye rais ataapishwa!

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Hatimaye rais ataapishwa!
ban.blank.jpg


Edward Kinabo​

ENYI wana wa Tanzania, mnaolia kwa uchungu wa kupewa rais msiyemtaka, yule mnayemwita rais wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), nimetafakari sana jinsi ya kuzipoza hasira zenu, nimeshindwa!

Nimeshindwa kwa sababu naujua uchungu wenu, si rahisi sana kupozwa kwa wito wa kuweka mbele amani badala ya haki. Najua hasira za kila mmoja wenu ni nzito kuliko uzito wa taifa lolote ukilibeba pamoja na watu wake. Nani awezaye kupoza uchungu kama huo? Nani awezaye angalau kufariji mioyo inayokata tamaa kama hiyo?

Nakiri tena nilitamani kulitimiza jukumu hilo lakini nimeshindwa. Kitu pekee nilichoweza ni kuuchomoa ujumbe huu kutoka kwa mmoja wa vijana wazalendo wa taifa hili, Eric Ongara.

Yeye angalau amejaribu kutoa maneno yanayoweza kulifariji taifa linaloumia. Naitumia safu hii, kuwasilisha kile Ongara alichokiandika kwenu, kama ifuatavyo:

"Enyi watu mahiri na mashujaa wa wakati wenu na kwa kizazi chenu. Poleni sana kwa harakati za uchaguzi na hongereni sana kwa kujitoa katika kila hali katika kutetea na kusimamia kile mnachokiamini.

Mungu azidi kuwajaza nguvu, ujasiri na mafanikio katika maisha yenu, kwa maana nyinyi ni watu huru ambao mnakula vilivyo halali kutokana na jasho lenu. Misukumo yenu ya kisiasa ni uzalendo na mapenzi yenu kwa nchi yetu iliobarikiwa na wala si ufisadi kama walivyo washindani wetu waovu.

Ni kweli hatimaye walio waovu, mafedhuli, mafisadi na wahuni wamepoka ridhaa yenu, wameamua kufanya uteuzi badala ya kusimamia ridhaa yenu. Haya yasiwarudishe nyuma. Sisi ni dhaifu kiasi gani hata kukatishwa tamaa na uovu?

Historia inatufundisha siku zote wema hushinda uwovu, ukweli husimama juu ya uongo na haki ya mtu haipotei. Sisi kushinda na wao kukamata mamlaka ni changamoto za kawaida katika harakati za ukombozi. Wanaye mkuu wa mamlaka lakini katika mioyo yetu yupo kiongozi wetu tumembeba na kumhifadhi.

Wana wa Israeli kule Misri kiongozi wao alikuwa Musa lakini mwenye mamlaka alikuwa Farao, kwa shurti walitii maagizo ya kikatili ya Farao, pamoja na jeshi lake lakini uhalali wa kuwa kiongozi katika mioyo ya wana wa Israeli ulibaki kwa Musa.


Makaburu waliwatesa weusi wenzetu kule Afrika ya Kusini, Botha alikuwa na mamlaka makubwa lakini katika mioyo ya wazalendo kiongozi wao alikuwa Mandela pamoja na kuwa jela.

Wakoloni walikuwa na nguvu ya kupindukia lakini kamwe hawakuweza kuteka mioyo ya Watanganyika wazalendo, kiongozi wao alikuwa Nyerere. Huko Burma leo hii utawala dhalimu wa kijeshi unamnyanyasa mwanamama mpambanaji kwa vifungo vya ndani lakini pamoja na hayo ridhaa yake haijafutika katika mioyo ya wana wa ardhi. Je, sisi ni bora kuliko wao?

Tunajifunza kutoka katika historia hizi zilizotukuka kwa wazalendo kutochoka pamoja na mateso, unyanyasaji, ubabe na dhihaka. Hata siku moja hatuwezi kumchukia mama yetu, hatuwezi isusa nchi yetu tuliyopewa na aliye na mamlaka juu ya wahuni na mafisadi.

Natambua mna hasira, dhibitini hasira zenu, tujipange………ila msisahau muda wote kuwakumbusha kuwa tunajua uhuni wao na hatukubaliani na unajisi wao kwa taifa.

Watakuwa na kauli zao za kawaida za kuwaambia tugange yajayo, yaliyopita si ndwele! Cha msingi ni kuwakumbusha kuwa tunafahamu na hatuwezi kusahau kwamba tunapambana na wezi na waovu. Tunajipanga, tutawashinda karibuni bila kumwaga damu, wala hatuchukua miaka arobaini kuelekea nchi ya ahadi.

Mungu amewajalia maarifa na vipaji vya kuzaliwa akawabariki na upendo kwa wengi wanaowazunguka. Fanyeni kazi kwa bidii, imarisheni familia zenu, mfanikiwe katika kazi zenu, mzidishiwe rasilimali na mkumbuke kujiwekea akiba na kujipanga.

Malaika wa mbinguni wanapaza sauti kuimbia na kusifia majina yenu kwa maana mmesimama upande wa haki. Msichoke, Msinyong'onyee kuweni imara kwa maana tunajipanga, unabii u-karibu kutimia. Nawapenda kama aliye juu anavyowapenda", mwisho wa kunukuu. Ahsante sana Eric.

Na ikiwa kila mmoja wetu atabaki imara bila kukata tamaa, huku akitii nasaha za rais aliyetazamiwa, Dr.Willbrod Slaa, hatimaye siku si nyingi sana lolote linaweza kutokea. Rais wa kweli hatimaye ataapishwa!

Yaliyotokea yametupa njia, tunakaribia kufika. Tuunge mkono msimamo wa Dk. Slaa wa kuyapinga matokeo feki ya urais. Tushiriki kikamilifu katika vuguvugu la kudai kuundwa kwa tume huru ya kupitia matokeo ya uchaguzi.

Tujiandae kuwa sehemu ya kupigania katiba mpya mapema iwezekanavyo maana vuguvugu hilo ndilo litakalobeba matumaini mapya ya taifa hili.

Tuweke mbele amani ya taifa letu bila kutoa fursa ya kuendelea kuporwa haki zetu. Siku ya haki yafanya hima kuja na siku hiyo ikifika hatimaye rais wa kweli ataapishwa.

Aluta continua.


Source: Tanzania Daima
 
Nimeisoma, imenitafakarisha na nimeipenda! Upo ukweli mwingi sana humo ndani.
 
Siku hiyo si mbali, siku ambayo watanzania watatoka mdomoni mwa joka liumalo na kutisha. Joka lenye sumu kali linalouma kwa tabasamu likifurahia unyonge wa watanzania.Mungu atazisikia sauti za watu wake naye atalitoa taifa hili mikononi mwa madhalimu.
 



Kikwete haujui kwanini vyama vya upinzani havifanyi vizuri?!!!! Balozi gani anayetaka kuangusha CCM, mtaje .
 
Last edited by a moderator:
Nani ana website ya ikulu ambayo mkulu anasoma tutume hii. Tafadhalini wajameni. Nimesoma nimetoa machozi
 
Asante kaa la moto lakini ukumbuke uzuri wa maneno ya hiyo article haiondoi kuja kuchekwa na vizazi vijavyo, kuwa hawa babu zetu what the hell happened with them? kwa nini waliingia kwenye uchaguzi hali wakijua NEC ni ya CCM, hakuna maelezo wala majibu ya hili, bali ni ujinga, haijalishi ulifanywa na watu wangapi ila ulikuwa ujinga, hata baada ya kutahadharishwa mara nyingi. wasitegemee miujiza ya Slaa kuingia IKULU na NEC hii "wasusia" matokeo hawa walizikaza shingo zao kama hawajasikia kitu!

Haya maneno hata kama yameandikwa na malaika, bado tunaibiwa mali zetu, tunanyanyaswa, tunaonewa na CCM, bado ccm wanatutawala kimabavu na hakuna wa kutusaidia not slaa not tlp, may be cuf zanzibar wameweza!
 
Asante kaa la moto lakini ukumbuke uzuri wa maneno ya hiyo article haiondoi kuja kuchekwa na vizazi vijavyo, kuwa hawa babu zetu what the hell happened with them? kwa nini waliingia kwenye uchaguzi hali wakijua NEC ni ya CCM, hakuna maelezo wala majibu ya hili, bali ni ujinga, haijalishi ulifanywa na watu wangapi ila ulikuwa ujinga, hata baada ya kutahadharishwa mara nyingi. wasitegemee miujiza ya Slaa kuingia IKULU na NEC hii "wasusia" matokeo hawa walizikaza shingo zao kama hawajasikia kitu!

Haya maneno hata kama yameandikwa na malaika, bado tunaibiwa mali zetu, tunanyanyaswa, tunaonewa na CCM, bado ccm wanatutawala kimabavu na hakuna wa kutusaidia not slaa not tlp, may be cuf zanzibar wameweza!

Nani ana website ya ikulu ambayo mkulu anasoma tutume hii. Tafadhalini wajameni. Nimesoma nimetoa machozi

Maneno mazito haya!
 
""Yaliyotokea yametupa njia, tunakaribia kufika. Tuunge mkono msimamo wa Dk. Slaa wa kuyapinga matokeo feki ya urais. Tushiriki kikamilifu katika vuguvugu la kudai kuundwa kwa tume huru ya kupitia matokeo ya uchaguzi.

Tujiandae kuwa sehemu ya kupigania katiba mpya mapema iwezekanavyo maana vuguvugu hilo ndilo litakalobeba matumaini mapya ya taifa hili""

Sijui Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema nini kuhusu hili

Pengine ingekuwa vema kwa Wabunge 46 wa CHADEMA kuanzisha hoja ya kudai katiba mpya kwa kukusanya Majina na sahihi za Watanzania,wenye umri usio pungua miaka 18, wanaounga mkono hoja hiyo popote pale walipo duniani.
Naamini kuna Watanzania zaidi ya Milioni (10,000,000) wanao amini kwa dhati kwamba Katiba yetu ni mzigo kwa kila mwananchi wa Tanzania, haitafsiriki kiutendani na zaidi ni chanzo kikubwa cha vurugu za Kiuchumi na Kisiasa. Pia, katiba hii inawapa uwezo wa Kimungu watendaji wa serikali bila kuwapa nafasi wananchi kuhoji utendaji wao.

Huu ni Mkuki wa umoja.
Wabunge 46 wa CHADEMA kiwe ndicho chuma kitanguliacho katika mkuki wetu(Tindu Lissu awe kwenye Tip) Sisi waTanzania tuliobaki tuwe mpini ujishikao imara nyuma ya chuma kilicho kichwa cha mkuki.
Dr Slaa atatakiwa kufanya kazi moja tu, kukamata mpini ule na kunuiza maneno yenye kubeba Upendo, Haki na Hekima na kuurusha kwa nia moja katikati ya utata wa katiba na kupenyeza hadi ndani.

Ukiwa mnyonge kwa sababu ya Dhurma na Kunyimwa haki tumia Unyonge wako kupambana na dhurma ili kurejesha haki yako.
 
natamani iwe mwaka 2015 nikiwa sijasikia sauti ya JK aende akapumzike,maana miaka hii 5 inayokuja itakuwa miaka ya kuugulia maumivu hasa kwa scandal zitakazokuwa zinaibuka kila iitwao leo huku wakimuandaa fisadi mwingine wa kuchukua nchi 2015 ili alinde madudu waliyofanya kwa ngwe yao ya mwisho. Natabiri mwisho mbaya sana kwa RA sidhani kama watanganyika wataendelea kumvumilia wakija kutambua kwamba yeye ndiyo adui wao namba moja!
 
Back
Top Bottom