Waziri wa zamani, Profesa Juma Kapuya afunga ndoa na binti wa miaka 25

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,646
218,101
Wale wote waliokuwa wanamuulizia Kiongozi wao wa zamani mahali aliko na anavyoendelea basi sasa bila shaka kiu yao itakwisha

Kiufupi ni kwamba mkubwa anaendelea vema tu na wala hana wasiwasi na jana amefunga ndoa na binti wa miaka 25


Profesa Juma Athumani Kapuya, anawatakia usiku mwema.!.jpg




Ndoa hiyo imefungwa Wilayani Urambo Mkoani Tabora siku ya jana tarehe 17 Februari, 2019

Profesa Kapuya aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi na Waziri kwenye Wizara Mbalimbali kwa miaka tofauti, alizaliwa Juni 22, 1945

Katika kudhihirisha usemi wa 'mapenzi hayachagui umri' inadaiwa kuwa binti aliyeolewa na Profesa Kapuya ana umri wa miaka 25

Mbali na kufahamika kupitia uwanja wa siasa Procesa Kapuya pia aliwahi kuwa Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)

Ikumbukwe kuwa mwaka 2013 Profesa Kapua aliingia katika matata baada ya kukumbwa na kashfa ya kumbaka binti wa miaka 16 aliyekuwa anamsomesha

Katika kujaribu kudhibiti mtoto huyo aliyedai alibakwa na Prof Kapuya na kuambukiwa virusi vya ukimwi, Mwanasiasa huyo alitoa vitisho vya kumuua binti huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.

=====

Kapuya Matatani: Adhibitiwa na kitoto kinachodai alikibaka, akakiambukiza virusi - JamiiForums


Ukweli kuhusu CCM kumbeba Kapuya dhida ya Ubakaji alioufanya, huu hapa... - JamiiForums
 
Njaa inauma!!!! chunga usicjinjenyau!!!! nyaa inauma !!!!umekula kirimotoe!!! huyu dem njaa imempeleka
 
Back
Top Bottom