Hatimaye nimerudi kwenye mshahara wangu wa laki 4 kwa mwezi

gidume

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
743
906
Baada ya kupigika ndani ya miaka mitatu ya kuacha kazi niliyoona haina maslahi..kufungua biashara zikanishinda na kuzifunga nyingine kuziuza baada ya kuchoka kuumiza kichwa.

Nimerudi rasmi kwenye maisha ya mshaara wa laki nne kwa mwezi..uzuri nna gari yangu nilionunua baada ya kuuza biashara zangu..maisha sio shida kabisa..nimerudi kwenye nyumba ya bure kabisa, sijilipii matibabu nalipiwa na ofisi yangu pendwa nashkuru wamenipokea.

Tuacheni uongo biashara ni jambo lingine kabisa, asije akakushauri mtu uache kazi uingie kwenye ujasiliamali..biashara zina mambo mengiii hatari..nilipigika adi tsh 10 nilikua naiona kubwa.

Nashkuru sasa maisha yamenifunza nna adabu ofisini hapa sbabu najua nilipotokea.

Bahati mbaya sana nilishazoea maisha na ya udalali pia kwaiyo kule ilikua full kupigwa na jua kupambana na ela ukipata inaishia siku io io au kesho yake.

Hivyo mshahara nikipata hua unaisha ndani ya siku mbili alaf naanza ganga njaa au kuishi kimiujiza..ila nimeridhika kama ipo ipo tu siku moja mungu akiamua kunifungulia atafungua bila kutoa jasho kama nilivyotoa jasho kabla bila mafanikio yoyote..nakumbuka kuna njia nilikua sijawahi kupita ndani ya miaka lakini nilizipita..njaa nilikua nashinda hata siku mbili kwaiyo hamna kinachonitisha kwa sasa.

Tushukuruni sana hizi nafasi zetu mungu alizotupa..tusiziwekee kiburi wala kudharau na kujiona tunaweza kuliko wengine..maarifa ni muhimu sana kabla ya kufanya maamuzi ya haraka.

Wasalaam…
 
Duuuh unachekelea kurudi kwenye utumwa


Biashara mpaka isimame sio kitu cha mwezi au mwaka mmoja

Ilinichukua miaka minne kuisimamisha japo ni kweli niliangusha biashara zangu na kukumbiwa na wafanyakazi mpaka kuamua mimi au mke tu ndio tusimamie

Hapo ikaleta matunda, nakushauri japo umerudi kazini ila tengeneza misingi mkuu ya biashara zako kuna kukosa nguvu mbeleni kwenye fainali
Tena usipende sehemu za bure bure ubongo unalala

Asante
 
Baada ya kupigika ndani ya miaka mitatu ya kuacha kazi niliyoona haina maslahi..kufungua biashara zikanishinda na kuzifunga nyingine kuziuza baada ya kuchoka kuumiza kichwa..

Nimerudi rasmi kwenye maisha ya mshaara wa laki nne kwa mwezi..uzuri nna gari yangu nilionunua baada ya kuuza biashara zangu..maisha sio shida kabisa..nimerudi kwenye nyumba ya bure kabisa,sijilipii matibabu nalipiwa na ofisi yangu pendwa nashkuru wamenipokea..


Wasalaam…
Private or government???
 
Kuna watu waliozaliwa kutengeneza.

Kuna watu waliozaliwa kusaidia kundi hilo la watengenezaji.

Halafu kuna kundi la waliozaliwa kutumia, wenyewe huwa wanasubiri hayo makundi mawili yaandae.


Kila kundi limejaaliwa uwezo binafsi wa kutimiza majukumu yao.


Ukiwa mtumiaji ukajifanya mtengenezaji, huwezi fika mbali. Utarudi kwenye uhalisia wako.


Vilevile ukiwa msaidizi wa kundi la kwanza nawe ukajifanya mtengenezaji, hutofika mbali pia, Utarudi kwenye uhalisia wako.


Kila mmoja kwa NAMNA Yake.

Wahuni husema "Usi force tufanane".
 
wakuu mim kuna kitu huwa kinanichanganya
asilimia kubwa ya wanaoacha kujiajiri na kwenda kuajiriwa ni nying kuliko wanaoacha ajira kwenda kujiajiri

ila ukitembea mtaa kwa mtaa utakuta nyumba za waliojiajir ni nying kuliko za walioajiriwa (hii imekaaje ilhali serikalin uhakika wa mshahara ni 100%) hata magari pia ni hvyo hvyo

sasa unajiuliz wengne wanafanyaje kufikia hapo na kila siku wao misemo yao ni "biashara ngum" ila wamejenga na wanazidi kuongeza mijengo

ikianzishwa thread ya kuajiriwa vs kujiajiri (upande wa kuajiriwa itakuwa na point nyng)

ukirudi kitaa waliojiajir weng wamewapiga gape walioajiriwa (japo sio wote)

hii imekaaje wadau
 
Duuuh unachekelea kurudi kwenye utumwa


Biashara mpaka isimame sio kitu cha mwezi au mwaka mmoja

Ilinichukua miaka minne kuisimamisha japo ni kweli niliangusha biashara zangu na kukumbiwa na wafanyakazi mpaka kuamua mimi au mke tu ndio tusimamie

Hapo ikaleta matunda, nakushauri japo umerudi kazini ila tengeneza misingi mkuu ya biashara zako kuna kukosa nguvu mbeleni kwenye fainali
Tena usipende sehemu za bure bure ubongo unalala

Asante

Bora kua mtumwa lakini sio kwa kupigika kule ..ndo maisha niliochagua..
 
Hahahaha ngoja nicheke tu... kufanya biashara ni moyo.. yaan biashara n sawa na Jeshi... kunawanaoweza kutak risk na ambao hawawez...
Mshukuru Mungu kwa kujtambua kuwa ww Biashara huwez kaza buti mzee mwenzangu kwenye Ajira tu
Wala sio jambo baya

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app

Kabisa kabisa mkuu..tena uzuru nimegundua mapema..apa naomba niongezewe kamshaara tu
 
Back
Top Bottom