Hatimaye nimegundua mpenzi wangu ameshaniacha japo hajanitamkia. Naombeni ushauri namna ya ku-handle hii hali

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Baada ya safari ndefu kati ya Mimi na yeye leo ndo nimegundua mpenzi wangu ameshaniacha japo hajanitakia baada ya kugundua viashiria vifuatavyo:

1. Ameshanitamkia live kuwa upendo wangu kwake umeshapungua hivyo ananiona ni mtu wa kawaida baada ya kunipigia simu akinisalimia katika maongezi ameshanitamkia hivi

2. Ameniambia hivi sasa akili yake inawaza maendeleo hivyo hisia za mpenzi kwangu Mimi zipo chini sana

3. Ameshaniambia sasa hivi mimi na yeye tuna utofauti mkubwa sana

4. Nimejaribu sana kujitetea kujiweka sawa lakini naona hakuna uelekeo tena wa Mimi na yeye kurudi katika hali ya zamani hivyo kisaikolojia hapo binti kashaniacha japo kuna muda anaweza kunicheki kunisalimia kama mtu wa kawaida tuu

Hivyo wandugu naombeni ushauri maji yameshamwagika tiyari japo bado hajanitamkia sikutaki bado ila matendo na vitengo pamoja na maneno nimeshaona

Hivyo naombeni ushauri na kitu gani natakiwa nifanye kipindi hiki hii hali isinitese maana maji yameshamwagikaa hivyoo
 
Achana nae, sio fungu lako. Usilazimishe mapenzi just move on huwezi jua labda utakuwa umekwepa mengi.

Focus katika kujijenga na wala usimwambie chochote ikiwemo na kutompigia simu wala kumtext kuanzia leo wala akikutafuta usimjibu, wewe ni mwanaume fanya maamuzi ya kiume narudia tena focus on you mzee baba tafuta hela za kutosha
 
Huyo ni polygon anakupotezea muda,tembelea mtaa wa pili ukutane na vifaa...upooze mauchungu
 
Hiyo ni kawaida sana kwenye mahusiano... kupanda na kushuka. Mahusiano yote huwa yanapitia vipindi kama hivyo - wakati ambapo mmoja anaona kabisa upendo wake kwa mwenzake unasoma negative.
Sasa mahusiano imara ni yale ambayo yanaweza kuvuka nyakati hizi, na ukweli ni kwamba mahusiano mengi huwa hayavuki hapo.

Kwahiyo, kama hamna reason nyingine inayowafanya muendelee kuwa pamoja zaidi ya hisia - uwe na uhakika huu ndio mwisho wa enzi. As long as wewe ni mwanaume, utapitia sana nyakati kama hizi; haijalishi una mpenzi mmoja au ni mali ya umma.

Cha msingi kuwa mwelewa, ukishaona bundi analia dirishani, ujue mgonjwa wako kashaanza kufa miguuni, kwahiyo akihema anatoa harufu ya mzoga ndo maana bundi kaja.

Usitafute mchawi, jiandae kwa mazishi.

Na maisha ni lazima yaendelee.
 
Mwanamke kufika hatua hiyo ujue kuna tatizo.
Unatakiwa ujue ni kwanini huo upendo umepungua. Ujue pia ni kwanini ghafla anasema anaweka akili yake kwenye kutafuta pesa.

Kila tatizo lina solution yake, labda ukute mpenzi wako ni mtu wa kumeza vitu. I mean asiyependa kuweka vitu wazi. Na kuna sehemu wewe unamkera au kumuumiza ila anashindwa kukupa ukweli. (Hata hivo wanaume wengi sana hawapendi kuambiwa ukweli)

Jaribu kutafuta tatizo ni nini. Au wewe kama mwanaume ni wapi una-fail.
 
Hiyo ni kawaida sana kwenye mahusiano... kupanda na kushuka. Mahusiano yote huwa yanapitia vipindi kama hivyo - wakati ambapo mmoja anaona kabisa upendo wake kwa mwenzake unasoma negative. Sasa mahusiano imara ni yale ambayo yanaweza kuvuka nyakati hizi, na ukweli ni kwamba mahusiano mengi huwa hayavuki hapo.

Kwahiyo, kama hamna reason nyingine inayowafanya muendelee kuwa pamoja zaidi ya hisia - uwe na uhakika huu ndio mwisho wa enzi. As long as wewe ni mwanaume, utapitia sana nyakati kama hizi; haijalishi una mpenzi mmoja au ni mali ya umma. Cha msingi kuwa mwelewa, ukishaona bundi analia dirishani, ujue mgonjwa wako kashaanza kufa miguuni, kwahiyo akihema anatoa harufu ya mzoga ndo maana bundi kaja. Usitafute mchawi, jiandae kwa mazishi.

Na maisha ni lazima yaendelee.
Broo umezungumza ukweli mtupu ktk haya mahusiano ni Mimi ndio ninamuitaji sana binti ila kama ulivyozungumza ushauli wako ukoo vizuli sana nimeufatilia kwa umakini sana ,

Asante sana niggaz kwa sasa nimeshakubali matokeoo
 
Back
Top Bottom