Hatimaye nimefanikiwa kuondoka Afrika

Wabongo kwa ujuaji? aisee... hizi fursa naziskiaga miaka mingi sana.. kwa nini uchumi unadorola kama kweli Africa na Tanzania kuna fursa?

Wabongo wengi tuna roho mbaya na wivu, mtu hajawahi cross border yeyote lakini ana negative kibao mara utaosha vyombo, mara utakua bek3? Hivi wote wanaoenda huko Canada wanaishia kujuta?
Mkuu hao watu wasiwakatishe tamaa. Mtu akija nje kwa malengo anapiga hatua tu kwa kuwa kazi zipo kwa wote (yaani wenye elimu ndogo na kubwa). La muhimu ni kutochagua saana kazi. Nyingi ni za viwandani, care homes,usafi na shambani. Ila usirogwe ukaenda nchi za ulaya mashariki kwani wao ni wachovu pia. Mimi niko hapa UK. Kima cha chini cha mshahara ni pound 8 kwa saa. Hii ni takribani shs 24, 000 kwa saa. Ukifanya kazi masaa kumi kwa siku una Tshs zako 240,000.
 
Shukuru saana Mungu kwa kukutoa jahanamu. Kisha usijerudia tena kosa la kurudi huko sijeazibiwa tena.
 
Umachinga unalipa awamu hii...imebaki miaka sita tu...jiwe akiondoka tunaweza rudi enzi zile za kupigwa na mgambo...changamkieni fursa...laki mbili ni mtaji tosha pale kariakoo..
 
Hongera mkuu soon utaanza au ushaanza kupiga box kwa maana ya zile kazi za shuruba ambazo haziitaji skills ambazo ukiwa huku hata hufikirii kuzifanya lakini maisha popote muhimu uwe na malengo na uyazingatie.
 
kila la heri mkuu.
Ukishindwa kuishia Afrika kuliko na kila aina ya fursa na uhuru bwerere nje ya afrika utaishi ka punda na mtumwa.
maana utafanya kazi za usafi , jikoni, bar na kazi nyingine nyingi ambazo huku ulizikataa pia itafika wakati utafanya kazi zaidi ya moja ili kukudhi maisha
 
Mkuu hao watu wasiwakatishe tamaa. Mtu akija nje kwa malengo anapiga hatua tu kwa kuwa kazi zipo kwa wote (yaani wenye elimu ndogo na kubwa). La muhimu ni kutochagua saana kazi. Nyingi ni za viwandani, care homes,usafi na shambani. Ila usirogwe ukaenda nchi za ulaya mashariki kwani wao ni wachovu pia. Mimi niko hapa UK. Kima cha chini cha mshahara ni pound 8 kwa saa. Hii ni takribani shs 24, 000 kwa saa. Ukifanya kazi masaa kumi kwa siku una Tshs zako 240,000.
Vp kuhusu hal ya Maisha lakn...?
 
Vp kuhusu hal ya Maisha lakn...?
Ugumu wa maisha, labda kodi ya nyumba tu ndio kubwa kidogo. Lakini vyakula ni vingi sana na vinanunulika kwa bei za kawaida. Kama wewe ni mpenzi wa maziwa, mayai na nyama ya kuku , basi hivyo ndio vitu vya bei rahisi kabisa. Ukiacha majiji makubwa sana kama London, Birmingham , Manchester na Liverpool bei ya chini kabisa ya chumba kwa baadhi ya miji unaweza kupata kwa pound 180 au 200 kwa mwezi. Hiyo ni sawa na shs 600,000. Sasa ukifanya kazi kwa masaa 40 kwa wiki una kipato kisichopungua 960,000 shs. Hii ni kwa wiki tu.
 
Njoo inbox 2ongee vzur mkuu
 
Nilikuwa nina tamani sana kujaribu maisha nje ya afrika na ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu.

Nimejaribu kuondoka Tanzania toka mwaka 2015 bila mafanikio mwaka 2017 nikafanikiwa kwenda kujaribu maisha Dubai nikitegemea nitapata ajira sema nilienda kipindi cha low season sikupata ajira nikaishia kuwa dalali na visa ilipoisha ikabidi nirudi zangu bongo.
Mwaka 2018 nikaanza tena tafuta njia ya kuruka Germany au Canada.

Hatimaye Mungu ni mwema nimefanikiwa nina mwezi niko Anderson Vancouver. Maisha siyo rahisi kama nilivyokuwa nina imagine ila nina imani within a period of time yatakuwa sawa.

Kazi za kufanya zipo, sija experience ubaguzi wala nini labda kwakuwa sijichanganyi sana na bado nasoma mchezo.

Wanaotaka kuruka nje msikate tamaa maisha popote dunia yetu sote

Huja-experience ubaguzi na hautau-experience mimi nakuhakikishia. Unajua kwa nini? Huna mentality hiyo. Kawaida ubaguzi huwa unaanzishwa na mbaguliwa mwenyewe kichwani kwake, halafu baadaye anau-project kwa wenzake, halafu ndiyo hapo anakamilisha circle yake na kuanza kudai kuwa anabaguliwa, wakati kumbe anajibagua yeye mwenyewe halafu anawasingizia wengine. Na ukishajibagua mwenyewe, lazima watu wengine wakukimbie kwa sababu nao wataona kuwa unawabagua, na wakishakukimbia, lazima ujione kuwa umebaguliwa.

Nakupa hongera sana endelea kuishi kwa staili hiyo hiyo na utaishi maisha mazuri sana na wenzako wanaokuzunguka. Negative thoughts za kujenga mwenyewe kichwani halafu unaanza kuzi-project kwa wengine huwa ni shetani mbaya sana katika maisha. Watu wa aina hii huwa wanawasumbua sana wengine katika maisha yao ya kila siku
 
Mkuu hao watu wasiwakatishe tamaa. Mtu akija nje kwa malengo anapiga hatua tu kwa kuwa kazi zipo kwa wote (yaani wenye elimu ndogo na kubwa). La muhimu ni kutochagua saana kazi. Nyingi ni za viwandani, care homes,usafi na shambani. Ila usirogwe ukaenda nchi za ulaya mashariki kwani wao ni wachovu pia. Mimi niko hapa UK. Kima cha chini cha mshahara ni pound 8 kwa saa. Hii ni takribani shs 24, 000 kwa saa. Ukifanya kazi masaa kumi kwa siku una Tshs zako 240,000.
Hongera mkuu watu hawajui mtu mmoja aliye huko anasaidia watu kibao walioko huku wanapodai kuna fursa.
 
Huja-experience ubaguzi na hautau-experience mimi nakuhakikishia. Unajua kwa nini? Huna mentality hiyo. Kawaida ubaguzi huwa unaanzishwa na mbaguliwa mwenyewe kichwani kwake, halafu baadaye anau-project kwa wenzake, halafu ndiyo hapo anakamilisha circle yake na kuanza kudai kuwa anabaguliwa, wakati kumbe anajibagua yeye mwenyewe halafu anawasingizia wengine. Na ukishajibagua mwenyewe, lazima watu wengine wakukimbie kwa sababu nao wataona kuwa unawabagua, na wakishakukimbia, lazima ujione kuwa umebaguliwa.

Nakupa hongera sana endelea kuishi kwa staili hiyo hiyo na utaishi maisha mazuri sana na wenzako wanaokuzunguka. Negative thoughts za kujenga mwenyewe kichwani halafu unaanza kuzi-project kwa wengine huwa ni shetani mbaya sana katika maisha. Watu wa aina hii huwa wanawasumbua sana wengine katika maisha yao ya kila siku

Mkuu nina zawadi yako, seriously. Mindset ndo kila kitu
 
Oooh wonderful! Basi tufanye hivi kwa zawadi hiyo: Weka hapa vocha ya tigo halafu uzi-reverse namba hakuna atakayejua, halafu mimi nitajaza kwenye simu yangu
Basi Weka vocha ya tigo hapa halafu uzi-reverse namba hakuna atakayejua, halafu mimi nitajaza kwenye simu yangu
 
Back
Top Bottom