Hatimaye nimefanikiwa kuondoka Afrika

Canada wanatoa nafasi za kuishi watu nchi kubwa halafu ina watu wachache. Canada ni miongoni mwa Nchi tajiri kabisa. Kiuchumi ni nchi ya 10 lakini ina ardhi na rasilimali nyingi Sana kwa mafuta ni nchi ya tatu kwa kuwa na reserve kubwa ikiwa ya Kwanza ni Venezuela, ya pili ni Saudi Arabia na ya tatu ni Canada. Pia Canada ina viwanda kibao. Canada ndio business partner wa Marekani. Marekani inategemea iuze bidhaa zake nyingi Canada
Kuna watu wachache ila marekani inategemea iuze bidhaa zake?!!!Huwa mnajisahau sana mnapoandika.mnafikiri humu wote wana akili kama ya msukuma.
 
Nilikuwa nina tamani sana kujaribu maisha nje ya afrika na ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu.

Nimejaribu kuondoka Tanzania toka mwaka 2015 bila mafanikio mwaka 2017 nikafanikiwa kwenda kujaribu maisha Dubai nikitegemea nitapata ajira sema nilienda kipindi cha low season sikupata ajira nikaishia kuwa dalali na visa ilipoisha ikabidi nirudi zangu bongo.
Mwaka 2018 nikaanza tena tafuta njia ya kuruka Germany au Canada.

Hatimaye Mungu ni mwema nimefanikiwa nina mwezi niko Anderson Vancouver. Maisha siyo rahisi kama nilivyokuwa nina imagine ila nina imani within a period of time yatakuwa sawa.

Kazi za kufanya zipo, sija experience ubaguzi wala nini labda kwakuwa sijichanganyi sana na bado nasoma mchezo.

Wanaotaka kuruka nje msikate tamaa maisha popote dunia yetu sote
Kazana sana bro kuna watu nina mifano yao mingi wameikimbia tz lakini wanahaha kuyafuta nauli kurudi bongo. Jamani maisha bongo ni rahisi sema wabongo sisi wavivu na hatuna uthubutu. Wengi waoga wa maisha na kujitia usister du na ubrotherman wakati hatuna kitu
 
Ndio maana nimesema wewe ni masikini nilipokua nafanya kazi za kuajiriwa za uhasibu kama wewe nilikua masikini ndio maana nasema wewe sio level yangu kuajiriwa nimeacha 2005..siuzi vitu reja reja nasambaza vitu kwa hao wanaowauzia upo katika kundi la watu masikini amini nachokuambia...

Sawa boss, nisamehe nimekosa mimi...
 
Umenena vema
watanzania wachache sana tunapongezana kwa kufanya vizuri. Majority waliopo ććm wamejaa unafki tu.

lawama zote kwa John
Hahaha dah polen san ndugu zng. Vumilien yatakwisha tu maana kila lenye mwanzo lina mwisho. Waswahili wanasema hakuna marefu yasiokuwa na ncha
 
Nilikuwa nina tamani sana kujaribu maisha nje ya afrika na ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu.
Nimejaribu kuondoka Tanzania toka mwaka 2015 bila mafanikio mwaka 2017 nikafanikiwa kwenda kujaribu maisha Dubai nikitegemea nitapata ajira sema nilienda kipindi cha low season sikupata ajira nikaishia kuwa dalali na visa ilipoisha ikabidi nirudi zangu bongo.
Mwaka 2018 nikaanza tena tafuta njia ya kuruka Germany au Canada.
Hatimaye Mungu ni mwema nimefanikiwa nina mwezi niko Anderson Vancouver. Maisha siyo rahisi kama nilivyokuwa nina imagine ila nina imani within a period of time yatakuwa sawa.
Kazi za kufanya zipo, sija experience ubaguzi wala nini labda kwakuwa sijichanganyi sana na bado nasoma mchezo.
Wanaotaka kuruka nje msikate tamaa maisha popote dunia yetu sote
Mkuu Njoo inbox 2ongee kwa mapana
 
Hongera sana, Ila ukiwa hapo Vancouver jaribu kumtafuta Drake umpe salaam, mwambie bado tunatafakari kauli yake. " KAMA HUNA GARI HUNA SABABU YA KUENDELEA KUISHI" .
 
Tehtehteh....

G. Traveller kaza buti hadi unafika Canada naamini ulikuwa na malengo yako...

Usikatishwe tamaa na wanaokuambia umeingia cha kike. Aaah wapi upo sehemu sahihi.....hizo fursa ulizozitaja za kazi anza nazo.....Dunia ni yetu sote. Maisha ukiona hauyafurahii Tanzania unaamsha.

Kila sehemu ina fursa zake.
 
Wao walijenga nchi zao nyie mnaenda kufanya kazi kwao, mnakwama wapi mkijenga nchi yenu maana maji yapo, madini yapo, ardhi ipo, usalama upo nk
Wao ndo walianza kuja kwetu na ndo walipoharibu kila kitu
 
Mimi nakupongeza sana kwa kufanikiwa kuondoka.Sasa ndoto yangu ipo pale pale.CANADA NITAFIKAJE?
 
Nenda kapate uzoefu wa nje, sio vibaya coz unapata kitu kipya kwenye ubongo. Tulienda na tukarudi, home is best hata pawe namna gani, ila ukijipanga utarudi home kivingine and life will be better.

Usisahau kutuambia jinsi utavyopamisi nyumbani.
 
Dunia Ni kitu Cha ajabu iache hivyo hivyo .Mtanzania mwenzetu anapanda ndege kuwa amechoka maisha Tanzania na Afrika anaenda kutafuta maisha Canada angani anapishana na ndege imebeba wacanada wa kwmpuni ya madini ya Barrik wanakuja kutafuta fursa Tanzania baada ya kuona kule haziko.Life is a paradox.Tunakutakia maisha mema canada
Ndiyo maisha yalivyo, nimezaliwa huko juu milimani kabisa lakini nimekuja town kutafuta fursa, wapo walioenda huko nilikotoka wameona fursa kibao, wanalima tangawizi and they make money like hell.

Hatuwezi kujifungia wote kwenye kapu moja, let others explore opportunities in other parts of the world.
 
Wabongo kwa ujuaji? aisee... hizi fursa naziskiaga miaka mingi sana.. kwa nini uchumi unadorola kama kweli Africa na Tanzania kuna fursa?

Wabongo wengi tuna roho mbaya na wivu, mtu hajawahi cross border yeyote lakini ana negative kibao mara utaosha vyombo, mara utakua bek3? Hivi wote wanaoenda huko Canada wanaishia kujuta?
 
Back
Top Bottom