Hatimaye Ndugu wa Aqulina Akwilini wakubali kuchukua mwili wa marehemu

mi mchaga kwa hili ............ mungu tubariki wachaga wote
Sometimes inabidi ata kutaja hili kabila inatupasa tubadili na majina huko nchini hali imekuwa mbaya sana . Ila kama tumetangulia basi tumetangulia they should run if they want catch up our race. Rest in peace Akwii .
 
Uchunguzi gani? Risasi imempiga kichwani na ubongo umemwagika na kioo cha nyuma ya gari kuna tundu la risasi,kuna uchunguzi gani tena? Au Sielewi?
Wanataka kuchunguza kama hiyo risasi ilitoka kwenye SMG ya askari polisi au ilitoka kwenye SMG ya CHADEMA.

Kwani huwajui hawa.
 
Unataka wachikuwe mwili,wakazike,halafu baadae ije ripoti "ALICHOMWA NA KITU CHENYE INCHA KALI".
Acha wasubiri maana,washampoteza tayari.
Kama ni mm ninayetakiwa kusoma hiyo ripoti ya "ALICHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI". ningegoma na kujiuzulu. Siwezi ongea uongo mbele ya jamii na Mungu, ni dhambi mbaya sana.
 
Pengine ushauri wa hawa wazazi waliopoteza watoto wawili waweza wasaidia


Kuna kitu kinaitwa kanuni za maumbile hapa Duniani,mwenyezi Mungu anatutaka sisi binadamu tuzitumie ili kutoyaweka maisha kwenye rehani, ndio maana ukitaka kujenga nyumba imara lazima utumie vipimo sahihi kama hautofata ushauri huo wa kitalaam ukapata madhara unawezaje sema MUNGU AMEAMUA? lakini kama umejitahidi kufata kanuni na bado kifo kikatokea ndio hapo tunasema tayari lilishapangwa.Mfano mzuri ukiwa unajenga jingo la ibada yaweza kuwa msikiti au kanisa, kasha ukashindwa kufata kanuni za ujenzi bora,baadae jingo hilo likapata madhara hapo ni wewe umeshindwa kufata kanuni za maumbile, mwingine anaweza jenga jingo ambalo sio la ibada tena yaweza kuwa la kufanyia uhalifu labda Guest House lakini akafata kanuni , jingo hilo litadumu kwa muda mrefu sio kwa sababu Mwenyezi Mungu anaridhia yale machafua yanayofanyika mule hapana , ila kwa sababu aliyejenga amefata kanuni za maumbile. Kwa hiyo sio kila jambo tusimtupie Mwenyezi Mungu tu, sisi wanadamu tunawajibu wa kufata kanuni za maumbile ya Dunia.
 
Wakishasubiri hizo Siku 14 ndiyo Marehemu Ndugu yao atafufuka na kuendelea na maisha yake? Hatari moja kubwa ninayoiona hapa ni kwamba tayari Familia inaanza kuingiwa na ' Kirusi ' cha Kisiasa huku ' wakidanganywa ' na wanaotaka kuwafanya ngazi yao ya Kupandia na ya Kipropaganda ya Kisiasa kisha baadae waharibu kila kitu.

Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu ambaye hajaguswa na Kifo hiki cha Akwilina Akwiline ila naona kama vile kuna ' kambinu ' fulani kanataka kutumiwa na baadhi ya Wanafamilia kwa kujifanya wanakuwa wagumu na wanashinikiza jambo fulani ili mradi tu wapate ' attention ' kubwa na chochote kitu kutoka Serikalini ili ile Kauli ya '' Kufa Kufaana ' itimie.

Ni busara tu ndiyo inahitajika katika hili na siyo kuanza kuonyeshana ' mabavu ' katika hili jambo kwa kwenda Kuchukua Mwili wa Mpendwa Wetu na taratibu zote za Maziko zifanyike ili Marehemu akapumzike na maisha yaendelee.

Ushauri pekee ambao naweza kuutoa kwa Serikali ni kwamba wajiahidi kadri wawezavyo Kuubeba huu Msiba lakini ikiwezekana basi Familia yake ambayo inaonekana ni duni Kimaisha na iliyokuwa ikihangaika Kumsomesha Akwilina Akwiline ifanyiwe jambo jema tu la hata kuanzishiwa Mradi / Biashara huku ikitunzwa kwa ukaribu kama sehemu kubwa ya kuwafariji.

Nimalizie tu kwa kusema CCM na CHADEMA na Wananchi wengine wote kwa sasa tuweke tofauti zetu pembeni na tuhifadhi ' mihemko ' yetu ila tushirikiane kwa hali na mali kufanikisha Msiba huu unamalizika na tuache kuanza kuwagawa Wanafamilia kwa hizi Siasa zetu na Wanafamilia waache kuanza kuwa na harufu ya ' Kutekwa ' Kisiasa na Kianaharakati na kutaka kuutumia huu Msiba kama ' Mtaji ' wa baadae wa Kiuchumi.

Yangu ni hayo tu Kimtazamo ila R.I.P sana Mdogo wangu Akwilina Akwiline.
achakuchukulia poa na kirahisi namna hiyo familia wanataka kujua nani kamwua mwanao na kwanini kwa kutumia kitu gani, ilikuweka kumbukumbu ya marehemu sawa hata kwa wadogo zake baadaye,ni kweli hatafufuka hata baada ya hiyo siku14.ijulikane kama ni serikali imemwua au nani kwa maandishi
 
The familly of the victim may be weaker than the police but God will pay back! Huwezi kudhulumu ukabaki salama
 
Kwa nini mpaka sasa HAWAJAMWAJIBISHA Afande Mambosasa na Mkurugenzi wa Kinondoni?.
 
Washauriwe vizuri, wasizidi kujitia simanzi, wakauchukue mwili wazike, hakuna litalobadili lililotokea.

Binti ameshateseka vya kutosha, akapumzishwe kwa amani.
Mnafiki wewe. Na lazima utakuwa unatoka uko wa wachawi.
 
Back
Top Bottom