Hatimaye NCCR yafikiria kumsamehe David Kafulila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye NCCR yafikiria kumsamehe David Kafulila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Jul 11, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  MGOGORO baina ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila na Uongozi wa chama chake cha NCCR-Mageuzi, umeelekea kupata suluhu baada ya chama hicho sasa kuamua kumsamehe.

  Mvutano huo uliosababisha mbunge huyo kijana kuvuliwa wadhifa wa Ukatibu Mwenezi na baadaye yeye na wenzake watano kuvuliwa uanachama, uliibuka mwishoni mwa mwaka jana baada ya kudaiwa kuzungumza mambo ya ndani ya chama katika vyombo vya habari.

  Kufuatia uamuzi huo Kafulila alifungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo, ambapo mahakama ilitoa agizo la kusitisha maamuzi hayo mpaka kesi hiyo ya msingi itakapomalizika, hivyo kumfanya Kafulila kuendelea kuwa mbunge.

  Taarifa zilizolifikia Gazeti hili jana zinaeleza kuwa pande hizo mbili zimeona ni muhimu kuafikiana na kurudi katika meza ya mazungumzo nje ya mahakama ili kukiimarisha chama hicho.

  Zilieleza kuwa suala hilo ni moja ya ajenda zilizojadiliwa katika kikao cha Halmashauri Kuu kilichofanyika wiki moja na nusu iliyopita baada ya kuibuliwa na mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

  Akizungumza na Mwananchi, Katibu mkuu wa chama hicho, Samwel Ruhuza alisema Kafulila ameomba msamaha na kusisitiza kuwa hivi sasa amebadilika huku akipinga vikali kuwa suala hilo lilijadiliwa katika kikao hicho.

  
“Suala hili halikujadiliwa kabisa katika Nec iliyoketi hivi karibuni, ndio maana haikuwa ajenda kubwa,” alisema Ruhuza.

  Licha ya kutokuwa tayari kueleza msamaha huo uliombwa kwa maandishi au kwa maneno, Ruhuza alisema, “Msamaha ni msamaha na jambo hili nisingependa kulieleza kiundani zaidi kwa kuwa litaamuliwa na vikao vya chama, pia limeshafika mahakamani.”

  Aliongeza kuwa kwa sasa kesi ya suala hilo ipo mahakamani na kusisitiza kuwa hata siku moja chama hakiwezi kuacha kusikiliza msamaha wa mtu.

  “Sisi tumeupokea na unaweza kujadiliwa ama kutojadiliwa kulingana na kikao kitakavyoamua, ila nisingependa kulielezea zaidi suala hili tusubiri kwanza tuone” alisema Ruhuza.

  Kafulila na wenzake akiwemo aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa tiketi ya chama hicho , Hashim Rungwe walivuliwa uanachama kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam Desemba mwaka jana.

  Mapema juzi, Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alisema suala hilo linawezekana lakini asingependa kulizungumzia hadi awasiliane na wanasheria ili lisimletee utata.

  Huku akipinga kuwa suala hilo lilijadiliwa katika kikao hicho, Mbatia alisema, “Hakuna kitu kama hicho, ila tukizungumza inawezekana, lazima niwasiliane na wanasheria ili isije ikaniletea utata";

  "If you i'll give me a call next week (Kama utanipigia wiki ijayo) nitakuwa kwenye nafasi ya kukujibu hilo." Alisema.

  Kwa upande wake Kafulila alisema hana kikwazo chochote kama chama chake kitaamua hivyo na kwamba atakuwa tayari kulifuta zuio aliloliweka mahakamani na kuzungumza nje ya mahakama.

  Alisema anaamini katika siasa kuna wakati wa kukwaruzana na kukosana lakini mazungumzo yanakuwepo na kusameheana.

  "Hata Israeli na Palestina hukosana mara kwa mara na mazungumzo hufanyika ili kufikia mapatano,"alisema Kafulila na kuongeza;

  "Wakitaka mazungumzo yawepo hata ile kesi niliyofungua mahakamani nitaifuta."

  Mwishoni mwa mwaka jana ulizuka mgogoro mkubwa kati ya Kafulila na chama chake na kusababisha afukuzwe uanachama.

  NCCR-Mageuzi kilimfukuza Kafulila ambaye awali alikuwa kada wa Chadema na makada wengine sita.

  Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam na kutawaliwa na vurugu.

  Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”

  Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki , Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe hao wakisema kwa sauti ya juu.

  Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.

  Kitendo hicho cha kufukuzwa uanachama kilimfanya mbunge huyo kukimbilia mahakamani ambako alipata amri ya Mahakama Kuu ya kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa chama chake kumvua uanachama.


  Amri hiyo ya Mahakama Kuu ilitolewa siku chache baada ya Kafulila kufungua kesi namba 218/2011 akipinga uamuzi huo na kuomba zuio la utekelezaji wake hadi kesi yake ya msingi itakapomalizika.

  Katika maombi yake, Kafulila aliitaka Mahakama itengue utekelezaji wa uamuzi huo wa chama chake ili aendelee kuwa mwanachama na mbunge wakati kesi ya msingi ikiendelea.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wagombanao..................
   
 3. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ajifunze kuheshimu sheria......haiwezekani ukawa juu ya chama ukaendelea kuvumiliwa......
   
 4. a

  afwe JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mwenyekiti hasira zimeisha baada ya kupewa ubunge!
   
 5. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Nafikiri sasa mheshimiwa mwenyekiti hasira zitakuwa zimekwisha. Kwani wote wapo ngoma droo wanafaidi keki ya taifa kupitia mjengo wa dom.
   
 6. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hatua nzuri. Ila mwandishi rekebisha, Ally Omari hakufukuzwa.
  Aidha, ni Lubungila (sio Lugungila). Huyu na wenzake ndio wameanzisha CHAUMMA
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ni kukua kwa demokrasia.kafulila ana michango mizuri sana bungeni na anakubalika jimboni kwake
   
 8. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  "Utusamehe makosa yetu KAMA nasi tunavyo wasamehe Wanaotukosea" Big up NCCR wabaya wwenu ni Magwepande tu hao tutawasamehe wakisha toka madarakani! CHADEMA nanyie wasameheni wale Madiwani watano Arusha tusonge mbele katika kuwabana Magwepande wasiendelee kupola utajiri watu!
   
 9. D

  DOMA JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Je Ikulu ikimuuliza mwenyekiti tukuvue wewe ubunge au wewe umvue kafulila atachagua lipi?
   
 10. d

  dav22 JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  walikuwa bado wanakifikiria tu??
   
 11. d

  dav22 JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mmmh hawezi kukubali wakati mwenyewe yupo anakula pipi....alafu cku hizi Mbatia hasikiki kabisa au ni baada ya kupata ulaji wa bungeni??
   
Loading...