dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Heshima kwenu wakuu,
Nimesikitika kusikia Mwenge umeanza kutumiwa katika kubomoa upinzani Tanzania, Je ndo malengo ya huu Mwenge?
Sisi zamani tulikaririshwa wimbo wa Mwenge ukakaa vichwani mwetu kama sara ya Baba yetu uliye mbinguni. “Sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Umulike nje ya mipaka yetu. Ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini. Ulete upendo mahali ambapo pana chuki na ulete heshima mahali ambapo pamejaa dharau”.
Lakini leo hii mambo ni tofauti kabisa. Unatumika kutugawa, kueneza chuki na kuondoa matumaini. Je ni kweli Mwenge ni Tool ya CCM?
Leo nmeona John Heche akilalamika kwamba wanasiasa wametumia Mwenge kuwaambia wananchi wasimchague tena. Hapa ni ujumbe katumiwa.
"Mh Mbunge Mwenge uko hapa Borega hawana sera, sera yao ni kukutukana wewe wanasema maendeleo haya sio wewe uliyeyafanya ni pesa ya serikali, wanasema usichaguliwe tena maana wewe unakamatwa kila siku, wanasema wewe ni kama jambazi wanakusema wewe tuu mpaka wananchi wachache waliopo wamepigia kelele bahati nzuri wengi ni wanafunzi wametolewa darasani, anaewaongoza kukutukana ni DC"
Nimepokea ujumbe huo kutoka kwa mwananchi.
Hii si sawa.