Hatimaye mkenya amewatambua wenzake aliyeshilikiana nao kumteka Dr.Ulimboka. wakiwa wamefariki

...NIna maoni tofauti kidogo na wengi waliochangia uzi hii. Kwanza niweke wazi kuwa sikubaliani na muanzilishi wa Uzi. Lakini hata hivyo, tukubaliane kuwa wote humu tunajua utendaji kazi wa Siri-kali yetu na vyombo vyake vya Intelijensia.
Tusiondoe kabisa uwezekano wa kuimbiwa wimbo huu siku ama wiki mbili tau zijazo kwa sababu watu wamebanwa na wnatafuta mahali pa kuchomokea! anything could be said...
Tusimbane sana muanzilishi wa Uzi. Tutoe muda kidogo kusikilizia, after all, Saa inaweza kuwa mbovu lakini mara mbili katika kila masaa 24 inaonyesha saa ya kweli! Nawasilisha....!
 
mh! ndugu yangu kama vyanzo vyano vya habari ndio vimekupa hii taarifa basi nimatumaini yangu taarifa unazo post humu sio za uhakika!!!!!!!!!!!!!!!1
 
wakuu naomba niweke mkazo kwenye maana ya neno TETESI, yawezakana ikawa kweli au lah! ya2pasa tuwe na subira watanzania.
Taarifa za kiintellengincia zilifika jeshi la police kwamba watuhumiwa walikuwa wanaelekea Zanzibar kwakutumia chombo hicho cha majini. ndio maana jeshi la police wakishirikiana na mshatikiwa aliyepatikana wakaamua kwenda nae ili kama ni taarifa sahii au lah baada ya kuangalia zile maiti zilizo opolewa, na mambo yakawa hivyo
Mkuu, kuna tatizo kubwa la uelewa hapa ndani. Nafikiri watu
wamemezwa na hasira za kisiasa na kusababisha umakini kupungua,
sio kila kitu lazima uchangie vitu vingine unasoma na kutafakari
au kusubiri kama ulivyosema, Kwa upofu wa fikra zao wamekuhukumu kama
muhusika ni wewe. Niko pamoja nawe nami nasubiri.
 
Tangu lini polisi wa bongo akawa great thinker. Karibia wote ni form 4 failures.
A
metokaje mahabusu na kwenda kuangalia maiti,je alipewa taarifa kuwa watapanda meli? na kwanini wasingewakamata kabla ya kupanda meli wakati wakiwa DSM? nani aliyemweleza kuwa ktk ile meli waliokufa mojawapo ni hao jamaa zake?

Hapa plan hii ni ya kukurupuka kama wasanii wa bongo films. Hakuana hata akili ya ki interegencia hapa. pooooooooleni KOVA, SIRIKALI na Washauri wenu!
 
Najisikia kutoa litusi ngoja nipite tu maana na kamvua ndio hako kanaanza....mama nanihiii...
 
Huyu mleta thread hii hamnazo kabsaaa, hizi commedy kafanyieni kwenye blog za kitoto huko bana mnabore, mfungwa toka lini akaenda kutambua maiti ya meli? nini kilisabababisha aende huko? hata mtoto mdogo anajua huo ni upuuzi tu!
 
swali..mtuhumiwa aliyeko mahabusu alipataje nafasi ya kwenda hospitali walikolazwa maiti kwaajili ya kuwatambua??? Doooh Asee...hiii nayo kali
 
kweli hii tetesi. Watu wa humu wanavisa sana, yani jitu linajua wazi kuwa hicho kitu ni kigumu afu bado linapost.
 
Kwani mnasubiri nini kumfikisha mahakamani kama tetesi zenu zinawaelekeza alihusika kumteka na kumjeruhi Dr.Uli?! Hamwoni hamumtendei haki huyo kijana? Tunajua utendaji kazi wa jeshi letu, kule Serengeti ilichukua nusu wiki kuwapata wahalifu wa tukio la kupora watalii lakini hili la kutekwa kwa Dr. Uli siajabu likachukua vizazi sita kama si karne!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom