Hatimaye Mkapa aikana Kiwira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye Mkapa aikana Kiwira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 8, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hatimaye Mkapa aikana Kiwira

  RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa amevunja ukimya na kutoa kauli kuhusu tuhuma zinazomkabili za kununua mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, akisema: "Hayo ni maneno ya watu; wameyazusha kwa manufaa yao wenyewe.”

  Mkapa, ambaye amekuwa hajibu tuhuma za kashfa zinazomuandama na hasa ya umiliki wa mgodi huo, alitoa kauli hiyo jana mbele ya waandishi wa habari huku akisisitiza kauli aliyowahi kuitoa kuwa hana hisa katika mgodi huo na wala hajawahi kumiliki hisa kwenye mgodi huo ambao sasa upo mikononi mwa serikali.

  Akizungumza baada ya kumalizika kwa mada kuhusu uongozi bora kwa rika zote Afrika ambayo alishiriki kama mchangiaji, Mkapa alisema hajui kwa nini wala sababu za kuzushiwa hayo.

  Mkapa alisema anashangaa na hajui sababu za yeye kuundiwa kashfa hiyo ambayo imekuwa gumzo miongoni mwa jamii hata ndani ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanania.

  "Sijui kwa sababu gani... na mimi nashangaa. Hata nyinyi wana habari mmeandika sana hayo, lakini nasema sina ‘share’ (hisa) katika mgodi wa Kiwira,” alisema Mkapa.

  Kama hiyo haitoshi rais huyo mstaafu aliyeongoza Tanzania kwa miaka 10, Mkapa aliwataka waandishi wa habari kujiridhisha zaidi kwa kwenda kusoma nyaraka za umiliki wa mgodi huo ingawa hakuweka wazi.

  “Mmeandika sana hayo, nasema sina share Kiwira, ninyi nendeni mkasome vizuri,” alisema rais mstaafu Mkapa.

  Hata hivyo Mkapa alihoji kuwa ikiwa kwenye mgodi huo kulikuwa na mradi wa kuzalisha umeme, uliishia wapi na kuwataka waandishi wa habari kuhoji hilo huku akisisitiza kuwa hana hisa katika mgodi huo

  "Kama ule ulikuwa mradi wa kuzalisha umeme, cha kuuliza hapa uliishia wapi; ulizeni; mimi sina share yoyote Kiwira," alisema Mkapa

  Kwa muda Mkapa amekuwa katika kashfa ya kuhusishwa na umiliki wa mgodi huo akishutumiwa kwa kujiuzia kwa bei ya kutupa chini ya thamani yake halisi akishirikiana na mkewe Mama Anna pamoja na aliyekuwa waziri katika serikali yake, Daniel Yona.

  Sakata hilo la umiliki wa mgodi wa Kiwira lilisababisha baadhi ya wabunge, hasa wa kambi ya upinzani na baadhi wakiwa wa CCM, kudai mabadiliko ili kuwezesha Mkapa afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

  Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro alilifikisha sakata hilo bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2008, akidai kuwa kwa kushirikiana na mkewe, pamoja na Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini mwaka 2004, walianzisha kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa mgodi huo kwa kificho.

  Kimaro alidai kuwa ingawa thamani ya mradi huo ilikuwa ni zaidi ya Sh4 bilioni, ilikubaliwa mgodi huo uuzwe kwa Tanpower Resources kwa Sh700 milioni, lakini hata ikalipwa Sh70 milioni tu.

  Hata hivyo aliongeza akidai kuwa mwaka 2006 Mkapa, Anna na Yona, waliingia mkataba wa kufua umeme na Tanesco kwa makubaliano ya kulipwa Sh46milioni katika kila siku , pasipo kujali kama umeme umefuliwa ama la.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuna usiri mkubwa sana katika mikataba ya kiserikali hapa Tanzania...Kitu kama mgodi(rasilimali ya taifa) unakuwa na utata wa mtu anayemilikishwa, si ni aibu sana hii?...Kama Ben anakataa, na hakuna document za kuthibitisha kuwa ni yeye, basi atawashinda waandishi kirahisi!...
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Na bado...tutaona mengi maana tunadharau natural laws which govern the existence of this world. Ukweli siku zote hujitenga na uongo. Mkapa inawezekana alikuwa anashauriwa vibaya au alijishauri vibaya kwa kukubali kuchezea dhamana ya kukaa ikulu. Sasa imefika sehemu anatafuta kusafisha jina lake. Ila ambacho hataweza kufanya ni kubadili ukweli kuwa yaliyotokea yametokea.
   
 4. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kwanini anakataa sasa hivi baada ya mgodi kurudishwa serekalini???? mbona Pinda alikiri bungeni kuwa ni wa Mkapa
   
 5. K

  Kasimba New Member

  #5
  May 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani ni muda tuu! kilakitu kitakuwa wazi, lets wait and see. not only that we are gonna see even the hiden ones
   
 6. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wanatuchezea akili zetu kama watoto wadogo.. Hizi ni zama za ukweli na uwazi. Sio Wadanganyika tena.
   
 7. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Why now? It's sickening!
   
 8. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninajiuluza lengo la habari hii iliyoletwa hapa sasa na ambayo imeandikwa na Mwananchi. Je habari hii ina lengo la kumuokoa Kikwete dhidi ya hasira za wafanyakazi ambao amewadharirisha kuwa hahitaji kura zao na wala hataboresha maisha yao hata ingekuwa miaka minane ijayo?
   
 9. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Why now? the question is why not now? Ushaidi wote ushapotea..ukiona wamekaa kimya hujue majina na mafile yanapotea tuu pale Brela. Ndo Tanzania yetu hio..
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hivi yule Mkapa wa BRELA bado yupo pale pale BRELA?
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  liar liar liar liar...na zile biashara alizofanya akiwa Ikulu alizifanya na nani?...sikufanya biashara nikiwa Ikulu nendeni mkasome....hana hata woga wa kusema uongo. Alikuwa wapi siku zote kujibu tuhuma...why now fisadi?
   
 12. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkapa is playing with our brains------------come on men just concede what is a problem, concede and ask for forgiveness, usije kufa na dhambi hii kubwa, najua wewe bwana Ben ni Mkristo mzuri tu, acha bana utaenda motoni? watch out by ourself, hell is waiting for evils and liars.
   
 13. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #13
  May 8, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda jina "Mkapa" halionekani kwa orodha ya wenye hisa. ANBEN - kampuni yao (Mkapa na mkewe) ilikuwa na hisa! ANBEN ilijiondoa katika hisa za Kiwira...waliuza hisa zao, nini?
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  HApa tusubiri mengi yanayokuja
   
 15. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Shame upon him!
   
 16. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #16
  May 10, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  What's wrong Mkapa kuwa na share Kiwira?
   
 17. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Wewe ni %$#&^XX@@###!:angry:
   
 18. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #18
  May 10, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  TzPride,

  I'd assume that the masked text in your reply is an insult you cannot post online.

  I know you are intellectually way better than that. You can definitely answer the simple question "What's wrong Mkapa kuwa na share Kiwira?". Don't you?

  Cheers,

  Mlenge
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Good question. Na kama ana shares mbona anakana? What's wrong with Mkapa admiting to having shares in Kiwira?
   
 20. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #20
  May 10, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  "When you hear someone saying 'good question' it means he does not have an answer" -- G. U.

  Jasusi, ikiwa mkapa ana share au hana ni irrelevant, swali, la kifalsafa, ni kwa nini iwe nongwa Mkapa kuwa na hisa Kiwira? Once we are done with that, we can discuss whether he indeed have hisa or not.

  Technically, Benjamin Mkapa anaweza asiwe na hisa Kiwira, ila inawezekana akawa na kampuni / share kwenye kampuni inayomiliki Kiwira. Still the main thing is, what's wrong kwa Mkapa kuwa na hisa Kiwira?

  Mlenge
   
Loading...