FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Habari!
Marekani iko mbioni kuutumia mfumo wa ulinzi wa anga wa "Iron Dome" kwenye vituo vya kijeshi katika nchi kadhaa za Ghuba kwa mara ya kwanza. Marekani ilinunua mfumo wa Iron Dome kutoka Israel baada ya makubaliano kati ya nchi hizo mnamo mwaka 2019.
Kulingana na ripoti na vyanzo ndani ya Israel, Israel imethibitisha kuiruhusu Marekani kuweka mfumo wa Iron Dome kwenye vituo vyake vya kijeshi katika nchi kadhaa za Ghuba, maeneo mengine ya bara la Asia pamoja na barani Ulaya.
Hili linafuatia baada ya Israel kutia saini makubaliano ya uhusiano na Falme za Kiarabu na Bahrain mnamo Septemba 2020. Hata hivyo, kambi gani haswa zitakazowekwa mfumo wa Iron Dome katika nchi za Ghuba bado hazijawekwa wazi. Kuhusiana na hili, tuendelee kuvuta subira, tutapata kufahamu panapo muda muafaka.
Itafahamika kuwa, Iron Dome ni mfumo wa ulinzi wa anga ulioundwa na kampuni ya Israel ya Rafael (Rafael Advanced Defense Systems) na kujumuishwa kwenye jeshi la Israel tangu mwaka 2011. Mfumo huu umekuwa ukitumika kwa ajili ya ulinzi dhidi ya roketi na makombora ya masafa mafupi.
Kama tuna kumbukumbu, basi tutakumbuka matukio kadhaa ya mashambulizi ya makombora ambayo yamekuwa yakiathiri eneo la Ghuba hususani nchi ya Saudi Arabia, hali iliyopelekea kuanzishwa kwa mpango mahususi wa kukabiliana ama kuyathibiti mashambulizi haya.
Pia, haya yanajiri baada ya uwepo wa ripoti mbalimbali za kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa mifumo ya ulinzi wa anga ambayo imekuwa ikitumika hususani ule wa Patriot hasa pale unapojaribu kukabiliana ama kuzilenga shabaha zenye kusafiri katika kimo cha chini ama kwa lugha nyingine, low-flying targets.
Mfumo wa Iron Dome unatajwa kuonesha uwezo mkubwa dhidi ya hatari hizi, mfumo unaotazamiwa kuukata huu "mzizi wa fitina" ambao umekuwa ukiiathiri Saudi Arabia na maeneo mengine ya Ghuba kwa ujumla.
Mchakato umeanza. Lakini, tutarajie kitu gani baada ya kusambazwa kwa mfumo huu wa Iron Dome katika eneo hilo?
Huu ni muendelezo wa yale ambayo tumekuwa tukiyajadili. Pia, waweza pitia hapa:

Mfumo wa Iron Dome wa Israeli kuukata 'mzizi wa fitina' Saudia?
Habari! Baada ya matukio mbalimbali ya mashambulizi ambayo yamekuwa yakiiathiri Saudi Arabia ikiwemo miundombinu za mafuta, kumekuwa na mpango mahususi wa kupandikiza mfumo wa ulinzi wa anga hususani dhidi ya makombora ya masafa mafupi na ndege zisizo na rubani, mfumo wa Iron Dome unaozalishwa...
www.jamiiforums.com