Hatimaye mchakato wa kuzindua rasmi Tawi la CHADEMA umekamilika

amba.nkya

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
446
131
Harakati ya mabadiliko ya kweli huanza kama wazo la mtu mmoja na kutoa ushawishi na msukumo kwa wengine kama kikundi na mwishowe jamii kwa ujumla ikiunga mkono wazo husika.
Itakumbukwa kuna Post moja nilibandika hapa JF yenye kusudio la kuanzishwa Tawi la CHADEMA kwa lengo la kuimalisha CHADEMA at grass root level ili kuleta maendeleo ya dhati kwenye nchi yetu.
Nashukuru kwa baadhi ya wanajamvi walionipa support juu ya mchakato huo.
Kati ya taratibu za kuanzisha tawi ni kuwa na wanachama 30, lakini tangu kuanza kwa zoezi la kuhamasisha wakazi wa eneo husika idadi imefika zaidi ya 120, hivyo kukikidhi mahitaji ya kuanzishwa kwa Tawi hilo ambalo litakuwa Mavurunza, kwenye kata ya Kimara, jimbo la Ubungo. Tawi hilo litazinduliwa wakati wowote mapema mwezi ujao Januari, 2011 kutegemea ratiba ya viongozi wa Chama.

Nawasilisha………
 
Back
Top Bottom