Hatimaye Maombi ya kumwombea Rais Magufuli yaanza kujibiwa

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wana JF kweli maombi yana nguvu. Kwa muda mrefu sana wengi wamekua wakilalamika kuwa rais Magufuli hapendi kusoma written speech na mara nyingi anapenda kuongea kutoka kichwani hasa hata katika sherehe rasmi.

Hii ilimfanya rais wetu KUTELEZA mara nyingi katika semi zake na kuacha wengi wakishangaa na wengine kukasirika na hata wengine kutomwelewa kabisa. Lakini naona maombi ya Watanzania yanaanza kujibiwa MOJA MOJA.

Mfano mzuri ni katika ziara ya rais Zuma wa Afrika Kusini alipotutembelea. Rais Magufuli alionekana na akazungumza huku akionekana PRESIDENTIAL.

Kwanza namsifu kutumia KIINGEREZA na KISWAHILI. Kiingereza chake kilikua IMPECCABLE/Kizuri sana.

Rais ALIZINGATIA hotuba iliyokua imeandikwa na hivyo kuepuka MATAMSHI ambayo yangeleta utata. Written speech yake aliyoisoma iliandikwa vizuri sana. Hata ilipombidii kwenda OFF CUFF/Kando na speech iliyoandikwa bado aliongea kwa sauti ya upole kama RAIS.

Wataalam wa body language watakubaliana nami kuwa kila alipokua akiinamisha kichwa kuelekea mkono wake wa kulia alikua akisisitiza UMUHIMU wa jambo fulani. Na alipopunguza TONE/Sauti yake, ilikua ni kuonyesha wajumbe waliokuwepo kuwa HE MEANT BUSINESS. Katika speech hiyo sidhani kama kuna mtu alitoka hapo akiwa na maswali ama kutoelewa chochote.

Wana JF naamini huu ni mwanzo wa maombi ya watanzania kujibiwa. Tuendelee kumwombea maana maombi hubadilisha mambo. Hata kongamano ndogo ndogo za INDOORS za wanasiasa hasa za waupinzani huenda nazo akaziruhusu maana hapatakosa sikio la serikali yake katika kila kongamano na hivyo kujua nini kinaendelea pasipo kuleta taharuki na migongano isiyo na maana kati ya wapinzani na serikali maana serikali ina MKONO MREFU kujua mambo na kuzuia mambo mabaya KABLA HAYAJATOKEA.

La mwisho tuzidi kumwombea ili tunapokuwa na MAJANGA YA KITAIFA kama vile mafuriko ama majanga yeyote RAIS MAGUFULI awe WA KWANZA KUTOA MANENO YA FARAJA NA MATUMAINI KWA WATANZANIA walio affected na kujaribu kutuo msaada mahali serikali inapoweza.

Naamini maombi yanaanza kujibiwa.

Mungu ibariki Tanzania na Rais Magufuli.
 
Haa chezea lugha zote sio kimombo pamoja na kuandikiwa alikuwa anatamka maneno kama mtoto wa pre-form one Kiufupi huyu Kipara hakustahili kuwa Rais wa nchi
Thauth Africa /sauth æfrikä/ Simu yangu haina option ya /Th/ sound na other phonetic symbols.Bado anahitaji apate Linguist mzuri ampe course ya proficiency and articulation...Though you can't teach an old dog new tricks.
 
Maombi yangu bado hayajajibiwa...Mimi naomba daily atoke madarakani so hayajatimia hadi siku yakitimia nitarudi hapa kuripoti.
Maombi kama hayo huwa HAYAJIBIWI.
Maana kila uongozi hutoka kwa Mungu.
Samehe and move forward!
 
Thauth Africa /sauth æfrikä/ Simu yangu haina option ya /Th/ sound na other phonetic symbols.Bado anahitaji apate Linguist mzuri ampe course ya proficiency and articulation...Though you can't teach an old dog new tricks.
Jamani Waswahili na kutafuta makosa tu?
Juzi juzi mlikuwa mnasema HAJUI kiingereza leo kaongea Kii ngereza perfectly,
lakini bado hamridhiki.

Na watazania sisi Watanzania wengi wetu tuna tatizo la neno "THE" Mara nyingi tulalitamka "ZE" "Ze people" "Ze sing" akimaanisha "The thing" etc.

Kwa kifupi. Most Tanzanians speak ENGLISH full of Swahili or MOTHER tongue accents. Kiingereza kilichojaa LAFUDHI ya KISWAHILI ama ya MKOA alikotoka.
Msikilize
Muhaya,
Msukuma,
Mujita and
to make the matters WORSE msikilize MCHAGA ama MKURIA akiongea kiingereza utafikiri ANAIMNBA WIMBO. Unabaki unajiuliza huyu ni Prof. Mzima lakini anaongea Kiingereza kama lugha ya nyumbani. Jamani TUSICHEKANE
Rais aliongea safi sana mkuu.
 
Back
Top Bottom