Hatimaye mabaki ya roketi ya China yatua bahari ya hindi

Kibumbula

JF-Expert Member
Mar 26, 2018
3,681
3,346
Mabaki ya roketi ya China yametua kwenye bahari ya hindi magharibi mwa nchi ya Maldivies pasipo madhara yoyote kwa binadamu kama China yenyewe ilivyosema.Naona USA kabaki hoi.Chanzo cha habari kwa mashirika yote ya habari ni kutoka China kwenyewe.

=====

Mabaki ya roketi ya China yalipuka na kuanguka Bahari Hindi​

Roketi ya China Yajiachanisha na Kuanguka Katika Bahari Hindi

- Kumekuwa na wasiwasi wiki nzima kuhusu mahali mabaki ya roketi ya Uchina yataanguka
- China ilisema mabaki hayo yalianguka Bahari Hindi mwendo wa saa nne na dakika 24 asubuhi saa za Beijing (saa kumi na moja na dakika 24 asubuhi saa za Afrika Mashariki) mnamo Jumapili, Mei 9


- Mabaki hayo yenye tani 18 ni sehemu ya roketi ambayo China ilirusha angani wiki chache zilizopita imekuwa ikizunguka bila kudhibitiwa


Kiwango kikubwa cha mwili wa roketi ya china kimeanguka katika Bahari Hindi siku ya Jumapili, Mei 9, China imetangaza.

Mabaki ya roketi hiyo yameanguka kufuatia wasiwasi na penyenye wiki nzima kuhusu mahali yangeanguka.

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali nchini China vikinukuu Kituo cha masuala ya anga cha China, kiwango kikubwa cha mabaki ya roketi hiyo yenye tani 18 kilichomeka na kuharibika kilipoingia anga za chini.

Mabaki hayo ni sehemu ya roketi ambayo China ilirusha angani wiki chache zilizopita imekuwa ikizunguka bila kudhibitiwa

Iliripotiwa awali kuwa mabaki hayo yalitarajiwa kuanguka duniani bila kudhibitiwa Jumamosi, Mei 8.

Hata hivyo, watalaam wa masuala ya anga walipuzilia mbali hofu kuwa chombo hicho kinaweza kulipuka kwenye makazi ya watu wakisema kuwa kitaangukia sehemu nyingine ya maji duniani.

China pia ilikuwa imekanusha ripoti ya kuwa mtepetevu kwa kuruhusu roketi hiyo kuanguka ikisema ina uhakika kwamba chombo hicho kitaangukia sehemu nyingine ya maji ya kimataifa.

Mnamo mwaka 2020, mabaki ya roketi hiyo aina ya Long March 5G yaliangka nchini Ivory Coast na kuharibu makazi kadhaa lakini hakuna yeyote ambaye aliripotiwa kujeruhiwa.
 
China walisema kuwa chombo chao hakitaleta madhara na kitaungua kabla ya kutua duniani na kwa kiasi kikubwa kitatua baharini.Na imekuwa hivyo hakika.Na wao ndio waliokiona chombo chao kilikoangukia.
 
Mabaki ya roketi ya China yametua kwenye bahari ya hindi magharibi mwa nchi ya Maldivies pasipo madhara yoyote kwa binadamu kama China yenyewe ilivyosema.Naona USA kabaki hoi.Chanzo cha habari kwa mashirika yote ya habari ni kutoka China kwenyewe.
Hebu thibitisha uhoi aliobaki nao marekani maana kuna ligi zinaanzishwa as if unapiganisha majogoo mawili
 
pia alisema kuwa hana mpango wowote wa kukizuia kwani ana mambo mengi ya kufanya.Rejea mada ya mdau jana hapahapa jukwaani.
 
Mabaki ya roketi ya China yametua kwenye bahari ya hindi magharibi mwa nchi ya Maldivies pasipo madhara yoyote kwa binadamu kama China yenyewe ilivyosema.Naona USA kabaki hoi.Chanzo cha habari kwa mashirika yote ya habari ni kutoka China kwenyewe.
Tuwekee ka video tuone hayo mabaki yakishuka mkuu
 
Sehemu kubwa ya roketi iliharibiwa ilipoingia tena kwenye anga, lakini vyombo vya habari vya serikali viliripoti kwamba mabaki ya roketi yaliangukia magharibi mwa visiwa vya Maldives siku ya Jumapili.

Kumekuwa na siku za kubashiri juu ya roketi inaweza kutua wapi, na maafisa wa Marekani na wataalam wengine walionya kuhusu kuanguka kwake na uwezekano wa kutokea majeruhi.

Lakini China ilisisitiza kuwa hatari ilikuwa ndogo.

Idara ya anga za mbali ya Marekani , wakati huo huo, ilisema tu kwamba roketi "ilikuwa imeingia tena juu ya Rasi ya Arabia". Haikuthibitisha sehemu ya kutua iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya China, ikisema badala yake kwamba "haijulikani ikiwa mabaki hayo yameathiri ardhi au maji''.

Huduma ya ufuatiliaji Space-Track, ambayo hutumia data ya jeshi la Marekani , ilisema roketi hiyo ilirekodiwa juu ya anga la Saudi Arabia kabla haijaangukia Bahari ya Hindi karibu na Maldives.

Chanzo: BBC News
 
Back
Top Bottom