Hatimaye luhanjo amedodoshwa ktk kinyang'anyilo cha makao makuu ya wilaya mpya ya wanging'ombe

Mngendalyasota

Senior Member
Jan 22, 2011
171
48
WanaJF,
Ktk hali ya vuta ni kuvute hatimaye kambi ya Luhanjo yenye madiwani 6 (kata 6) wa tarafa ya Wanging'ombe (total population 53,000)waliokuwa wanapendekeza makao makuu ya wilaya mpya ya Wanging'ombe yawe kijijini kwa Luhanjo (Wanging'ombe) wameshindwa kwa mbinde dhidi ya madiwani 11 (kata 11) wa tarafa ya Mdandu na Imalinyi (total population 200,000+) waliokuwa wanapendekeza makao makuu yawe kijiji cha Igwachanya ambacho kipo ktkt ya wilaya hiyo mpya. Katika kikao hicho cha baraza la madiwani wilayani Njombe nusura kivunjike hasa baada ya baadhi ya madiwani kutaka kurushiana makonde kutokana na kupingana kimtizamo. Tofauti hii ilitokana na kwamba wapambe wa Luhanjo wakiongozwa na mkurugenzi wa halmashauri ndg Mohammed Mkupete walitaka kupendelea kijiji cha Wanging'ombe ambacho wengi wanasema hakikidhi kuwa makao makuu ya wilaya hasa kwa kuwa si ktkt ya wilaya hiyo mpya.
 
huu upumbavu wa kuongeza wilaya mpya unanikera kuliko kitu chochote. wilaya zilizopo wameshindwa kuziboresha wanazidi kutuongezea mzigo wa kuhudumia mijitu ambayo haina hata tija kwa taifa. just imagine hapo lzm kuwe na dc na mijitu kibao ya kisiasa for nothing. We have to make changes so as to avoid such daily nonsenses of JK regime. Sata has started by switching off such DCs and RCs titles!
 
Na mwingine wa kuongezea majimbo. Nadhani ingependeza za serikal iistopshe kuongeza majimbo na wilaya kwa miaka japo 10.
 
Na mwingine wa kuongezea majimbo. Nadhani ingependeza za serikal iistopshe kuongeza majimbo na wilaya kwa miaka japo 10.
kweli kabisa...hii nchi haitaendelea kwa kigawa vipandevipande. hata kama itaamuliwa eti ukubwa wa kila wilaya iwe sawa na vijiji viwili bila dhamira ya kweli kwa hao wanaojiita watawala wetu hatutaweza kupata maendeleo. mnazidi kugawa wilaya na mikoa na majimbo ili kupatiana vyeo kama takrima kwa kufanikisha wizi wenu. shame on u!!!!!!
 
Luhanjo kumbe mwenyeji wa kijiji karibu na makambako? Maana nilipoenda Mbeya baada ya makamboko kwenda Mbeya niliona mahala kama kuna ukame vile wakaniambie ni Wanging'ombe.
 
Luhanjo kumbe mwenyeji wa kijiji karibu na makambako? Maana nilipoenda Mbeya baada ya makamboko kwenda Mbeya niliona mahala kama kuna ukame vile wakaniambie ni Wanging'ombe.

Mkuu ni hapo hapo mbele kidogo ya Makambako. Kama unaelekea Mbeya kushoto karibu na barabara kuna shule ya sekondari (sijui ya kata) inaitwa Wanging'ombe.
 
Haya matatizo kweli, hivi kweli Tanzania, nchi ya dunia ya tatu, yenye bajeti tegemezi, isiyo na umeme wala maji safi kwa watu wake lakini bado kila kukicha ina starehe ya kuongeza mikoa, wilaya, majimbo na Wabunge wa Viti maalumu katika hali hii ya uchumi? hakika huyu mtoto Tanzania sio riziki.
 
Nilishawahi sema kuwa suala la makao makuu ya wilaya ya Wanging'ombe liachiwe balaza la madiwani kwani niliamini litatenda haki. Kijiografia na kimiundombinu Igwachanya ni mahali sahihi kuwa makao makuu ya wilaya. HONGERA MADIWANI KWA KUFANYA MAAMUZI SAHII KWA MAENDELEO YA WILAYA YETU.
 
Jamani wana JF huko wanakosema IGWACHANGYA ni kweli panaweza pakawa katikati lakini chakujiuliza panamiundombinu gani kwa wazalendo ambao watahitaji huduma kutoka huko???

Ninavyojua mimi kuja WANGING'OMBE ingekuwa karibu zaidi kwa watu wengi ambao wangehitaji huduma kwa haraka kuliko hapo walipoamua kupaweka si kweli kwamba (its not convincing) hapa kuna personal interest na sio public interest...
 
Isoliwaya wanging'ombe kuna miundombinu safi kuliko hata huko Mkoani NJOMBE ambapo wangeweza kuitumia ile iliyokuwepo na shughuri zingeendelea sema hapa wanataka kuwaandikia watu proposal ya office mpya2

kha!!!! twifwa twilola.
 
Igwachanya ndio center suala la Miundo Mbinu sio issue itaenda with time unakumbuka Kilolo badala ya Ilula?
Luhanjo alipigania sana makao yawe wangi ila nadhani wengi wape Igwa NDO IWE MAKAO MAKUU YA WILAYA yeye ataambulia jina tuu
 
Si wamtengenezee tu wilaya yake ya Wanging'ombe yenye kata 6, kama walivyomtengenezea Pinda mkoa wake wenye wilaya 2? Hata Zanzibar sijawahi kusikia mkoa wenye wilaya 2. Lakini Tanganyika kwa Utawala wa JK imewezekana!!
 
Ubarikiwe. Nenda Rudi Salama Umefanikiwa - Nakumbuka maneno ya Willy Gamba

Dah!umenikumbusha mbali sana hicho kitabu cha NJAMA cha willy gamba nilisoma mwaka 1993 nikiwa primary kipindi hicho mshua alikua na vitabu kibao vya Ben Mtobwa ndo ulikua uridhi wangu km nilivyo na speed ya light kuwatch series now days
 
Jamani wana JF huko wanakosema IGWACHANGYA ni kweli panaweza pakawa katikati lakini chakujiuliza panamiundombinu gani kwa wazalendo ambao watahitaji huduma kutoka huko???

Ninavyojua mimi kuja WANGING'OMBE ingekuwa karibu zaidi kwa watu wengi ambao wangehitaji huduma kwa haraka kuliko hapo walipoamua kupaweka si kweli kwamba (its not convincing) hapa kuna personal interest na sio public interest...

Wanging'ombe unaifaham vizuri?kimaendeleo wameshindwa hata na kijiji cha ILEMBULA kiko mbele kidogo ya wanging'ombe wana hospital ya uhakika,nyumba za kulala wageni hata madhari yake huwezi kulinganisha na hiyo wanging'ombe ya kina Luhanjo na Mangula
 
Back
Top Bottom