Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

Tz boy 4tino

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,598
1,815
-Libya ile nchi iliyokuwa mfano kwa nchi za Afrika.
-Libya iliwahi kuwa nchi tajiri zaidi barani Afrika.
-Libya nchi iliyokuwa ikitegemewa katika bajeti ya AU.
-Libya ndo nchi pekee iliyowahi kuwekeza ndani ya bara la Afrika zaidi ya dola billioni 200 katika kipindi kifupi.
-Libya ndio nchi ambayo ilikuwa kimbilio la watu weusi wa nchi za Afrika Magharibi hasa WaNigeria katika harakati za kutafuta unafuu wa maisha.
-Libya ndio nchi iliyosaidia nchi za Afrika kupunguza gharama za kupiga simu, kutuma sms, na intaneti . Libya ilifanya hivyo kwa kununua satellite kwa niaba ya bara zima la Afrika kabla hapo nchi za Afrika zilikuwa nchi za ulaya mamilioni ya Euro kila mwaka.

Lakini toka kupinduliwa kwa utawala wa Muammar Gadaffi mwaka 2011 nchi ya Libya imebaki kuwa uwanja wa mapambano, soko la biashara haramu, huba ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mpaka sasa June 2020 , Ndani ya ardhi ya Libya kuna majeshi ya Saudi Arabia, UAE, Misri , Qatar , Urusi na Uturuki kila mmoja akipambana kuweka kiongozi atakayeendana na maslahi yao.

Hili ni funzo kwa nchi za KiAfrika kuwa makini sana na ushauri wanaopokea kutoka nje, miaka 10 tu iliyopita wananchi wa Libya waliishi kama wafalme.

1)Maji bure 2)Umeme bure 3) Bei ya Mafuta ilikuwa sawa na tshs 200 kwa litre 4)Hamna kodi ya nyumba 5)Elimu bure hadi chuo kikuu na kwa wale waliopendelea kusoma nje pia walilipiwa na serikali 6) Serikali ya Libya ilitoa takribani $ 60,000 karibu milioni 150 kwa kila wanandoa wapya ikiwa ni pesa ya kuanzia maisha.
7) Mwanamke aliyejifungua alipewa dola 5,000
8) Pia endapo mlibya atapata tatizo la kiafya ambalo haliwezi tibika nchini kwake alilipiwa gharama zote za matibabu nje ya nchi na Serikali.
9) Libya ndo nchi iliyokuwa na reserve Kubwa barani Afrika na haikuwa na deni la hata senti. Reserve ya Libya ilikuwa Dola Bilioni 150. N.K.

Libya kabla ya kifo cha Gadaffi .....

4E0F61D0-1E1D-4A34-B275-50565BE7E88B.jpeg
97D004F1-1B30-4513-B65E-E89611B9E860.jpeg
CEAF0F58-EB17-488E-B485-AFE2E160F14A.jpeg
9308E190-3849-49C8-9C46-78CEF85F61BB.jpeg
D2985AB6-08D5-4E18-84A9-5BDB85625443.jpeg
97D004F1-1B30-4513-B65E-E89611B9E860.jpeg
CEAF0F58-EB17-488E-B485-AFE2E160F14A.jpeg
9308E190-3849-49C8-9C46-78CEF85F61BB.jpeg
D2985AB6-08D5-4E18-84A9-5BDB85625443.jpeg

Libya baada ya Gadaffi

2C72F781-CC6F-46E7-8136-712D6BDC950A.jpeg
C96D46D9-DF53-4CE6-A6E6-5552674FE110.jpeg
A781C21F-0895-4F22-8088-9468E76E0320.jpeg
900DA2BE-8036-4B5A-A686-60CF5B4BA3A3.jpeg
C1DB3466-67A4-4F69-ADC8-A090E93B5A6C.jpeg
42EC269A-EDF3-43F0-B27C-2EE42C66D570.jpeg
1C9556E1-B8AD-45AA-9EFA-5E89DC5114D0.jpeg
36DFC8FC-DEDD-49FE-8BCF-7B35CB99DBA7.jpeg
509A46FF-9EFE-477A-9678-776A3D298C3C.jpeg
 

Attachments

  • E0EE71F0-1BEB-4A85-B71B-0D146900E8D0.jpeg
    E0EE71F0-1BEB-4A85-B71B-0D146900E8D0.jpeg
    40.8 KB · Views: 2
Inauma lakini tatizo kubwa la viongozi wa ki Africa na hata za ki Arab ni kung'ang'ania madarakani kwa njia moja ama nyingine.

Huwezi kuwatawala watu wenye akili na ufahamu kwa zaidi ya miaka 42 na bado ukataka mwanao akurithi !!. Watakufanyia fitna tu.
Sasa hiyo fitina imewasaidia nini? Wamerudi nyuma zaidi ya miaka 42. Walibya wanajuta sana!
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom