Hatimaye kocha wa Simba kutoka Cameroon awasili na kutia saini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
KOCHA Joseph Omog ametua jijini Dar es Salaam, jana Alhamisi saa 3usiku na amepanga kutumia mifumo mitatu tofauti ambayo itairejesha Simba katika ubora wake huku Mwanaspoti ikipenyezewa figisu figisu zote zilizomng’oa Azam FC.

Kocha huyo raia wa Cameroon anapenda kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ambapo anakuwa na straika mmoja mbele pamoja na viungo wawili wakabaji.

Kwa mujibu wa mfumo huo wa Omog kiungo mmoja wa kati huwa haruhusiwi kuvuka sehemu ya kati kwani, majukumu yake makubwa ni kukaba.

Kocha huyo anapendelea pia kutumia mfumo wa 4-3-3 ambapo, anakuwa na washambuliaji watatu mbele wote wakiwa na uwezo wa kufunga.

Katika kikosi cha sasa cha Simba Omog atakuwa akiwatumia Laudit Mavugo, Blagnon Frederick na Mohammed Ibrahim kwa pamoja.

Hata hivyo, katika mifumo yote hii Omog atahitaji kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba ambapo Simba italazimika kuongeza nguvu kumbakisha Justice Majabvi ama kusajili kiungo wa kariba yake.
 
...huyu kocha alivyokuwa Azam sikumbuki alifanya lipi la maana!, bado tuna safari ndefu sana!, yaani sasa tumekuwa wakuchukua "rejects" kuanzia wachezaji mpaka makocha!!
 
...huyu kocha alivyokuwa Azam sikumbuki alifanya lipi la maana!, bado tuna safari ndefu sana!, yaani sasa tumekuwa wakuchukua "rejects" kuanzia wachezaji mpaka makocha!!
sijawahi kumuelewa huyu,ila tusubiri tuone,naona simba wamechukua kocha na katibu toka azam
 
Bonge la kocha ila simba hatuna miundombinu na figisu figisu nyingi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom