Hatimaye Kim Jong Un wa Korea Kaskazini awasili Urusi kwa treni kukutana na Rais Vladimir Putin

kendy

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
266
494
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amewasili katika mji wa bandari wa Vladivostok nchini Urusi kwa mkutano wake wa kwanza kabisa na Rais Vladimir Putin.

Kremlin imesema kuwa viongozi hao watakutana mjinii Vladivostok siku ya Alhamisi na watazungumzia masuala ya usalama katika rasi ya Korea hasa "tatizo la nyuklia".

Kim anatafuta washirika wapya baada ya mazungumzo yake na rais wa Marekani Donald Trump kutibuka, wachambuzi wanasema.

Bw. Trump na Kim walikutana mjini Hanoi mapema mwaka huu kujadili mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini, lakini mkutano huo uliisha bila viongozi hao kukubaliana.

Tunafahamu nini kuhusiana na mkutano huo ?
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini havijathibitisha wakati na mahali mkutano huo utakapofanyika.

Lakini bendera za Urusi na Korea Kaskazini tayari zinapepea sehemu fulani katika mji wa pwani wa Vladivostok nchini Urusi ambako mkutano huo unatarajiwa kufanyika.
Presentational white space

Kiongozi wa Korea Kaskazini ameripotiwa kusafiri nchini Urusi siku ya Jumatano na kutoka ndani ya treni yake ya kibinafsi katika mji wa mpakani wa Khasan.

Alisalimiana na wanawake wa Urasi waliyokua wamevamilia nguo za kitamaduni kuashiria sherehe ya mapokezi yake.

Pande zote mbili zinataka nini ?
Mkutano huu unachukuliwa na wengi kama fursa ya Korea Kaskazini kuonesha washirika wake wakuu baada ya mazungumzo yake ya nyuklia na Marekani kuvunjikamapema mwaka huu, anasema mwandishi wa BBC Laura Bicker.

Taifa hilo limemlaumu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kwa kuchangia kuvunjika kwa mkutano wa mwezi Februari mwaka huu.

Mapema mwezi huu Korea Kaskazini ilitaka Bw. Pompeo aondolewe katika mazungumzo ya nyulia baada ya kumlaumu kuwa "anazungumza upuzi" na kuomba mtu "makini zaidi" kuchukua nafasi yake.

Mkutano huo pia ni fursa kwa Pyongyang kuonesha hatma yake ya kiuchumi ya siku zijazo hategemei Marekani, mwandishi wetu aliongeza.

Bw. Kim huenda akaishinikiza Moscow kulegeza vikwazo dhidi ya taifa lake.

Wadadisi wanaamini mkutano huu utatoa fursa nzuri kwa Urusi kuonesha ushawishi wake katika rasi ya Korea.

Rais Putin amekuwa akisubiri kwa hamu kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini kwa muda mrefu.

Kremlin imeonekana kutengwa katika mikutano iliyopita ya Trump na Kim.

Urusi sawa na Marekani na Uchina inapinga wazo la Korea Kusini kuwa taifa lenye uwezo wa knuklia.

Maafisa wa ngazi ya juu wa Kremlin wanapania kuona hali ya taharuki inapunguzwa katika eneo la rasi ya Korea.

Mkuu wa sera sera za kigeni za Urusi Yuri Ushakov, amesema kuwa hali imetulia katika eneo hilo katika miezi ya hivi karibuni.

"Urusi ina mpango wa kusaidia kadiri ya uwezo wake kuimarisha uhusiano mzuri katika kanda hiyo," aliambia wanahabari siku ya Jumanne.

Urusi iliwahi kushirikishwa katika mazungumza ya mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini.

Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Kim Jong-il, alikutana na rais wa Urusi wa wakati huo Dmitry Medvedev mwaka 2011.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Korea Kusini ipo haja ya "kushauriana" kuhusu usalama wa rasi hiyo.

Korea Kaskazini imekuwa ikiendelea na shughuli zake za nyuklia.

Mapema mwezi Aprili taifa hilo lilidai kuwa limefanyia majaribio ''silaha yake mpya''- inayodhaniwa kuwa kombora la masafa mafupi.
1080353

1080354

1080355

1080365

1080368

1080370

Vladimir Putin na Kim Jong-un waahidi mahusiano thabiti
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na rais wa Urusi Vladimir Putin wameahidi kuboresha mahusiano katika mkutano wao wa kwanza kuwahi kufanyika.
Wawili hao walisalimiana kwa mikono katika kisiwa cha Russky karibu na mji wa bandari wa Vladivostok, mashariki mwa Urusi.
Ikulu ya rais wa Urusi ya Kremlin imesema kuwa watajadili mpango wa kuacha matumizi ya nuklia lakini bwana Kim anasemekana pia yuko huko kuomba msaada baada ya mazungumzo na Marekani kutozaa matunda.
Rais wa Marekani Donald Trump na Bwana Kim walikutana Hanoi mapema mwaka huu lakini wakashindwa kufikia mapatano yoyote.
Kiongozi wa Korea Kaskazini alikaribishwa kwa upendo na maafisa wa Urusi alipowasili Jumatano.
Bwana Kim alipokelewa kwa burudani ya bendi ya jeshi, kabla ya kuingia ndani ya gari akiongozwa na walinzi wake a,nao wamezoweleka sasa kwa kukimbia kando ya gari lake wakati linapoondoka.
"Nimewasili Urusi kwa moyo wa upendo wa watu wetu, na kama nilivyosema , natumai ziara hii itakuwa ya mafanikio na ya maana," Bwana Kim aliieleza televisheni ya Urusi mapema baada ya kuvuka mpakakatika mji wa Khasan.
"Nimatumaini yangu kuwa wakati wa mazungumzona rais anayeheshimika Putin, nitaweza kujadili kwa kina masuala yanayohusiana na utatuzi wa swala la rasi ya Korea, na kaendeleza mahusiano yetu ."

1080858

1080856
 
Nabado tu huyy kiduku atahangaika Sana ili nchi iwe super power ni kazi ngumu kumiliki modern war apparatus ( nyenzo za kisasa za kivita) haimaanishi wewe una power tiyari Kuna kitu kinaitwa kura ya turufu( veto) hii ukishaipata nchi yoyote unaiwekea wikazo isipokuwa hizi nchi ndio uwezi kamwe( 1.USA 2.RUSSIA 3.CHINA 4.UK 5.GERMANY 6.FRANCE 5.TURKEY 6.ISRAEL ) Hapa kisuku suoni kabisa bado mtoto mdogo Sana
 
Kwa maoni yako mtoto mdogo sana, ila kwa nchi zilizomzunguka na uwezo wao wakisuper power basi huwa akitest madubwanashko yake huwa Kunatokea matetemeko ya ardhi huwa kuna tafrani, na huyo mnaemwita super power huwa anabwekabweka sana ila action ni 0

Mkuu kuwa sirias kidogo!!
 
Mbona una mihemuko mkuu? Kwani umeambiwa anagombea hiyo veto? yeye anaendelea na project zake. Marekani ndo wanamshobokea
 
Kwa maoni yako mtoto mdogo sana, ila kwa nchi zilizomzunguka na uwezo wao wakisuper power basi huwa akitest madubwanashko yake huwa Kunatokea matetemeko ya ardhi huwa kuna tafrani, na huyo mnaemwita super power huwa anabwekabweka sana ila action ni 0
Yaaa huo ndo ukweli. Huwa jamaa anafanya mambo yake lakini hao super power wanapiga kelele kama mbwa koko.
 
Nabado tu huyy kiduku atahangaika Sana ili nchi iwe super power ni kazi ngumu kumiliki modern war apparatus ( nyenzo za kisasa za kivita) haimaanishi wewe una power tiyari Kuna kitu kinaitwa kura ya turufu( veto) hii ukishaipata nchi yoyote unaiwekea wikazo isipokuwa hizi nchi ndio uwezi kamwe( 1.USA 2.RUSSIA 3.CHINA 4.UK 5.GERMANY 6.FRANCE 5.TURKEY 6.ISRAEL ) Hapa kisuku suoni kabisa bado mtoto mdogo Sana
Uko kishabiki Sana mkuu
 
Uturuki kumbe ni mnouma
 
Back
Top Bottom