Hatimaye Kikwete Afanya Kweli

Mzee Mwanakijiji,

I do not buy this nonesense!, alikuwa wapi siku zote? kuzuia sasa faida yake ni nini wakati tayari nyumba zote zilizotakiwa kuuzwa zimeuzwa? Habu nitajieni ni kiongozi gani wa zamani ambaye alitaka kununua nyumba ameshindwa? Nia na madhumuni ya kuuzwa kwa nyumba ilikuwa kuwapatia viongozi wa zamani nyumba, na hilo limeshatimia tayari sasa huu mkwara ni wa nini kama sio uongo?

Look at this, BM amenunua ile nyumba ya Sea View, JM amenunua ile nyumba ya See View, JK mwenyewe amenunua, Sumaye amenunua, Kawawa alijengewa bure, Msekwa amenunua, Siwale amenunua, Jumbe amenunua, Mwinyi amenunua, Msuya amenunua,

Warioba tu ndiye aliyekataa, lakini anashirikianaje na mwizi Mahalu? Wakati mmoja Warioba alikuwa anataka kuulazimisha ubalozi wetu NY umlipie rent mtoto wake yule wa kike June Warioba, ambaye hata kuandika jina lake tu ni taabu lakini alikuwa na bonge la scholarship kule DC, ninasema hivi kwa sababu siku zote huyu mzee anapenda kujiosha kuhusu rushwa na power, kumbe sio kweli!

Wazee hii serikali inadanganya kuhusu nyumba ukweli ni kwamba tayari wazee wote wa CCM walishapata nyumba ndio maana sasa wanasimamisha, NONESENSE!
 
Mzee Es,
wangu hapa umetupa madongo kishenzi lakini utanisamehe kusema kwamba June Warioba kabuntas?... Noo bro, June darasani kichwa kile kimetulia na kasoma bila kulipiwa toka huko alikoanza. Sema ukitoka darasani hapo tena habari nyingine!..
 
Mzee Bob,

Miaka yote June aliyokaa shule DC, degree iko wapi? Sisi tulikuwa tunasoma na kufanya kazi ili kujilipia maisha na watu kama yeye walikuwa kazi mwisho wa mwezi kwenda kukusanya posho pale ubalozini,

At the end sisi wote tuna degree yeye na wenziwe watoto wa vigogo, hakuna kitu! Unajua Bob ilibidi serikali ya US kupitia USAID iingilie kati na kusimamisha malipo hayo kwa watoto wa vigogo, ambao walikuwa wanakaa kwenye Luxurious apartments wakati sisi tunafukuzana na panya, ndipo wote wakarudishwa, Bob hakuna kati yao hata mmoja mwenye angalau Associate Degree!

Sasa yuko pale kwenye Law Firm ya Mahalu na baba yake, hebu nisaidie anfanya nini? Eti anatangaza biashara, za nani hakuna kitu, anyway the issue hapa na Mzee JK na nyumba, hilo ninasema ni another Nonesense ya kutafuta umaarufu watanzania ni lazima tuwe makni na serikali yetu mpya ya umaarufu!
 
MzeE Es,
Kusema kweli mimi nashindwa kumlaumu JK ktk swala hili na nitaeleza kwa nini!.
Tukumbuke tu pindi alipoingia madarakani, swala hili na ongezeko la mishahara kwa wabunge yalifikishwa kwake baada ya bunge kuendelea kuyaunga mkono..
Malalamiko ya wananchi wote yamesaidia sana kufkia yeye kutoa uamuzi ambao unapinga maamuzi ya wenzake hata kama wapo waliokwisha chukua nyumba ama mishahara hiyo chini ya utawala wa Mkapa. Anachofanya hapa ni marekebisho tu ya sera ambazo zimekwisha pita kama muswada. Kurudisha nyuma zote za zamani, hili swala jingine na kisheria sidhani kama inakubalika.
Sheria zote huanza kutumika pale mzee mzima kaangusha wino, nyuma ya hapo labda swala lililofikishwa kwake ni kutaifisha upya nyumba zote za serikali. Hii sio kazi rahisi na mara nyingi huondoa uaminifu wa serikali ktk maamuzi yake na baadaye kutumika (on record) kama mwelekeo ama serikali isiyokuwa na msimamo, mavunja sheria n.k. Jambo ambalo linaweza kabisa kuchangia kuwafukuza hata wawekeshaji.
Je matakwa ya wananchi ni yapi?... nyumba hizi zirudishwe... sawa lakini JK alituambia kabla ya uchaguzi kwamba hatarudisha nyumba zilizokwisha chukuliwa. Hii ndio ahadi yake na wananchi tulimpa kura zetu zote. Yaani Wa-TZ wamekubaliana na malengo yake ktk kuiongoza nchi. Yawezekana mimi na wewe hapa ni kati ya kundi ambalo halikumpa kura, tumesimama upande wa pili.
Mshikaji, June anayo digree, sema hakumalizia masters yake, nakumbuka alifanya kazi VOA na kazi hiyo anaiweza. Pia kumbuka Warioba hakuwa akifanya tena kazi serikalini na mwenzetu mjamaa alikunywa maji ya uhuru... hakutoka na kitu zaidi ya elimu yake.
Kusema kweli, navyofikiri mimi hiyo sheria ya kutosomesha watoto wa wakubwa hali wamekwisha ingia darasani ni maonezi na pengine roho za kikorosho.
Sheria ile ingetumika toka pale Mkapa alipoweka sahihi na sio kusimamisha hata kwa wale waliokwisha ingia masomoni kabla ya sheria hiyo. Kulingana na siasa za Kibongo hapa kuna watu walikuwa wakitafutwa tu. Ndiyo yale ya Nyerere, Nyerere hakusomesha watoto wake ama kutumia nafasi ile, leo hii kila mtu anamwona mjinga na mpuuzi.. hata mimi sikupenda kabisa kiongozi kuwaacha watoto wake bila elimu na urithi unaolingana na nafasi yake.
Kwa maana hiyo nampongeza sana saana Karume na matunda yanaonekana. Hakuna kabisa kitu kinachoitwa binadamu wote sawa!
 
Mzee ES, mimi nilikuwa shabiki wa Mkapa just kutokana na habari za magazetini, lakini jinsi JK anavyoanza kufanya haya mambo naanza kujiuliza hivi Mkapa alikuwa ni Rais wa nchi gani? Nafikiri kama kuna mtu ambaye Nyerere anajutia kutupa Watanzania ni Mkapa. Angalau Mwinyi ilikuwa ni majaribio ya utawala bila Mwalimu!! Mimi nafikiri Rais afanya hatua moja zaidi. Kama kuna kiongozi yeyote aliyenunua nyumba za serikali zaidi ya moja, basi warudishe hizo nyingine serikalini!!! Wachague ni ipi wanataka kuendelea kuwa nayo, na hizo nyingine zirudishwe kwenye matumizi ya serikali au ziuzwe kwa wafanyakazi wa kati!!

Halafu atuhakikishie kuwa hizo nyumba mpya walizopewa Mawaziri haziauzwa kwao baada ya uchaguzi ujao. Hizo zibakie kuwa ni nyumba za serikali.
 
Mzee Bob,

Elimu ni kwa watoto wenye uwezo wa kusoma kwani elimu sio kwa wote, kuna mtoto wa Mwalimu Magige peke yake ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusoma kwani wengine wote sio siri huo uwezo hawakuwa nao, sasa hata kama Mwalimu angejitahidi kiasi gani haikusadida kitu, halafu kumbuka kuwa wao jina lilikuwa linatosha kuwapa shule yoyote ile ndani na nje ya bongo kwa hiyo labda Mwalimu hakuwa na mali lakini Elimu hapana ni makosa ya watoto wenyewe,

Kwa mfano, Msekwa hakumsomesha mtoto wake huyu wa Foreign amejisomehsa mnwenyewe kwa ajili ya jina kapata shule Urusi na akaweza kupata kazi hapo protocl foreign, Mwinyi hakumsomesha Hussein, ni yeye mwenyewe aliyejisomesha Uturuki, sasa kwa sababu ya jina ni waziri, Vitalis hakusomeshwa na Kawawa, amejisomehsa yeye mwenyewe lakini baadaye jina limemsaidia kuwa mbunge, Swedi amejisomesha mwenyewe ila jina la baba lilimasaidia kuwa balozi UN, na sasa mbunge, William hakusomeshwa na JM amejisomesha mwenyewe kule NY sasa ndipo jina la baba linaingia kwani yuko njiani kurudi naye kupewa ubunge na baadaye atakuwa tu waziri no question about it, Januari amejisomesha mwenyewe kule US ndipo baadaye jina la baba Makamba ndio limemsogeza kuwa aide wa mzee JK,

sasa hii ni mifano michache ambayo wale wote wanaomlaumu Mwalimu kuhusu watoto wake kutokuwa na maendeleo wanapaswa kuieelewa na the fact kuwa wangejisomesha au angalau wangekuwa na uwezo wa kusoma, jina la baba yao lingewasaidia kwenda kokote wanakotaka, lakini kama huna uwezo wa kuiweza elimu jina haliwezi kukusaidia kitu ndio maana kina BM wamejitahidi kila njia kuwapa nafasi watoto wa Mwalimu kama Rose na Makongoro, lakini wasingweza kuwapa uwaziri kwani sio siri kuwa huo uwezo hawana, kutokana na kutokuwa na Elimu,

Karume watoto hawakusoma, isipokuwa wamebahatika kuwa katika mazingara yanayoruhusu kuwa viongozi bila ya kuwa na elimu ya kutosha, Ammani ndio kwanza anatafuta Degree pale Open University lakini ni rais wa ZNZB, kuhusu watoto wa viongozi na elimu mimi ninasema wapitie system yetu na watimize masharti yake kielimu ndipo majina ya baba zao yaingie kati sio kupata F kila siku halafu wanapewa nafasi nje za kusoma ndio maana USAID ilibidi waingile kati kwani walifahamishwa kuwa hawa watoto wa akina BM walikuwa ni mizigo kwa shule na kuziba nafasi wza wnegine tu, hakukuwa na kuonewa kwani kuna waliobaki wenye uwezo wa kusoma kama wa Mgaya, Chacha, JM, Ntagazwa, Mwambulukutu, ambao waliweza kujisomesha wenyewe mpaka mwisho, sasa hawa wengine waliorudishwa ni kwamba si kwamba walionewa hapana ni kwamba hawakuwa na uwezo wa kusoma hawa kina June, kina Magani hawakuwa na huo uwezo sio siri ukubwa wa wazazi wao usingeweza kusaidia kitu na unapaswa kutosaidia kitu, wasome kama sisi masikini au warudi nyumbani kama mtoto wa Rupia aliposhindwa kusoma tu akarudi nyumbani mapema na kuingia kwenye biashara za baba yake, na wengine wote warudi kwenye biashara za baba zao walizotuibia wananchi hela za kodi,

Back to the issue, suala la nyumba JK alipaswa kulisimamisha pale tu alipoingia, kama vile Bush alivyosimamisha sheria iliyopitishwa na Clinton ya serikali ya US kulipia abortions kwenye nchi zingine, hakuhitaji bunge wala kamati ya tume, ndio maana tunasema kuwa kuna walakini na hii issue bongo na nyumba, kwani lengo lake la kuhakikisha kuwa vigogo wote wana nyumba, lilitokana na marehemu Mnauye kufariki akiwa hana nyumba ikabidi mzee Makamba amfadhili aibu, ndipo vigogo walipomjia juu BM kuwa lazima wajengewe au wauziwe na serikali, sasa ninasema lengo limetimia ndio maana limesimamishwa, sasa huo ni uhuni wa siasa sio siasa au ni siasa za umaarufu tu yaani za short term fame, hazina faida yoyoyte kwa wananchi au taifa,

Mwanzoni nilikuwa na matumaini na mzee JK, lakini sasa nimeshanza kushituka kuwa ni yale yale tu, dalili nimeshaanza kuziona ila great ni kwamba Mtandao umeshaanza kuwa nyufa! Habari nilizonazo ni kwamba wanchama wengi wa mtandao wameanza kulalamika kuwa wametumia hela nyingi mno kumsaidia JK lakini uwezekano wa kurudisha hela zao unaonekana kutokuwepo na wengine wanadai Mzee JK amewatelekeza, ninajua kuwa kwenye kikao kimoja cha mtandao karibuni Mzee JK aliwatumia ujumbe kuwa ".........Mimi ni rais wa Tanzania nzima nimeupata kwa kuupigania kwa jasho langu, na sina ubia na mtu yoyote katika huu urais.............", sas politically what this means kwa bongo?

Ni kwamba soon tutasikia mifarakano ambayo itawafanya watoe siri zao katika kulumbana na kupakana matope, katika kutoa siri zao watatusaidia kujua madhambi yao kwa nchi na hata jinsi walivyovunja sheria zetu katika kutafuta power ambayo wameipata lakini ni clear kuwa competence inagomba, guys hawana ubavu wa kupambana na matatizo ya nchi yetu, ninasema hawana! Sasa Watanzania tuendelee tu kupigana na maisha yetu kama siku zote individually serikali hamna kitu, wewe rais wetu anasafiri na watu 50 katika hali hii ambayo nchi yetu imesimama kabisaa kiuchumi! Rais wetu hataki maswali ya kweli kwenye mikutano na wabongo nje? Why? anajua kuwa wabongo wa nje wanajua kinachoendelea na hawana sababu ya kumuogopa kumuuliza.

Haya another 10 years ya kurudi nyuma zaidi, ndio faida ya kuchagua serikali maarufu bila record, bila historia ya kuonyesha ila tu ushikaji tu hakuna kazi wala siasa ila ushikaji, sasa tutalipia for the next 10 years,

Mungu aibariki hii bongo!
 
Mzee ES,

Kuna kipindi wakati wa kampeni za uchaguzi kama utakumbuka tukiwa BCS nilikuwa critical sana wa JK , Mimi nilishajua ya kuwa JK awezi kuwa kiongozi mzuri kwa sababu ameingia pale kiujanja ujanja , mambo wanamtandao waliyomfanyia salim yatawa haunt milele ! kitendo cha kutumia rangi ya mtu katika kampeni ni cha kinyama na wala hakina nafasi katika jamii yetu ya leo.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuongoza nchi na genge , unapoongoza genge unaweza kusema lolote lakini kwenye Nchi watu tutakupima kutokana na matokeo ! JK amekuwa kama kasuku anazungumza sana bila vitendo anasema taboresha hali ya wafanyakazi wakati huo huo pato la taifa linazidi kupungua , sasa swali langu ni atawezaje kufanya hivyo ?

Mimi bado nimesikitishwa sana na kitendo alichokifanya pale DC , kwanza kukimbia maswali na kutudanganya kama watoto kuwa atarudi mwezi wa tisa na tutakuwa na nafasi ya kuuliza maswali kusema ukweli lazima viongozi wetu waache uswahili.


MZEE ES ,

Mwisho nakuomba sana sana kama unamjua mtu yote anayefanya kazi kwenye magazeti ya IPP , waambie bwana mtandao wao unaboa !!! kwani imekuwa kama sehemu ambayo JK anatumia kurusha propaganda zake kila siku wanamsifia JK !!!
 
Tausi,

Yaani ninasikitika kusema kuwa you were right, Salim tulimkataa karibu Watanzania wote as far as I am concerned kwa sababu hata baada ya uchaguzi hatukupiga sana kelele kuhusu kuonewa kwake, politically wabongo wengi hatukupendelea kuwa rais mwarabu, na hiyo ilikuwa dhana kubwa among viongozi wa juu wa nchi na hasa wa CCM na upinzani pia,

Ninajua watu kama Chief Fundikira, Ndesamburo, walishaanza kampeni za chini chini mapema sana kumpiga vita Salim kutokana na uarabu wake, the matter of fact watu kama Ndejembi aliyekuwa ndiye mkuu wa kampeni ya Salim, alishaitwa na mzee Ben mapema na kuambiwa "...acha kupoteza muda wako, nchi hii haitakuja kutawaliwa na mwarabu......", Ben alikuwa tu anamfikishia salamu za viongozi wengi wa nchi kuanzia upinzani mpaka CCm,

I personally, had a problem na Salim kwamba ingawaje alisifika na dunia hakuwa na chochote cha kuonyesha, yaani sifa zake zilikuwa hewa, halafu the fact kwamba alikuwa ndiye mentor wa Bandora ambaye ni Mrundi, lakini akampromote mpaka kuwa balozi wetu Lagos hii ingekuwa nchi za West ingekuwa scandal kubwa sana kwa Salim na angeacha siasa kabisaa, halafu record yake kule Adis ndiyo iliyomshitaki zaidi kwa watu kama sisi ambao tunaelewa yote aliyoyafanya kule ambayo sytem ya bongo ilikuwa inamfuatilia kwa makini kila anachofanya, hatuwezi kuyasema yote kwani ni aibu na the fact kwamba baada ya kushindwa Dodoma aliamua kujitoa kabisaa na siasa za bongo, ila angeleta makelele then yangesemwa,

halafu I do not care what, I was not ready kuongozwa na mwarabu mimi binafsi, sasa kama ni ujinga wangu ok I will take it yaani unaweza kusema lolote nitakubali tu lakini kuongozwa na mwarabu, HAPANA! Sasa kambi ya JK walifanya a great job kuwa-eliminate all the threats, kwa sababu Lowassa alipaswa kuwemo ili kupunguza nguvu za JK, JK alitishia CCM kuwa angetoka na kuingia upinzani, ni kweli angewasumbua CCm lakini asingeshinda, NO way! At one point alimu-offer adui wake mkubwa JM kumuachia nafasi ya kutawala kwa masharti kwamba yeye awe PM na iwe term moja, nilifikiri ilikuwa the best understanding kutoka kwa JK na kambi yake, lakini kambi ya Jm hapa ilikosea sana kukataa, at this point Bm alikuwa hajaamua kumsaidia nani, ni uchaguzi wa mwenyekiti wa vijana wa CCM ndio ulioanza kumsogeza Bm karibu na JK, pale kijana wa JM Nape alipopigwa mweleka, na from there on JK hakuangalia nyuma tena ukawa ni umafia tu na ukweli ni kwamba JK alikuwa na hela nyingi mno, kumbuka kuwa hata baada ya uchaguzi bado alibaki na shillingi billioni ishirini,

Katika huu umafia akambadili hata BM mawazo na kumsadia, kilichomsaidia JK kushinda ni the fact kwamba kwanza toka tupate uhuru Tanzania hatukuwa na tabia ya kuwatayarisha viongozi warithi, halafu tulijijengea tabia ya kuamini kuwa kiongozi anatakiwa kuwa suprise sio yule anayetajwa kila wakati, kitendo cha Ben kuweza kuwa rais mbele ya majina mazito yaliyokuwa yakitajwa ilikuwa ndio hasa chanzo cha tulipo sasa, kwani katika hii vurugu ya uchaguzi Watanzania tulifikia mahali tukasema kuwa mtihani ni mgumu kwa hiyo lazima Ben aingilie kati kutuchagulia kiongozi anyefaa, na yeye unakumbuka kwa kiburi akatuambia nitawa-suprise! Tukafurahia kuwa rais wetu amesikia kilio chetu, na kweli akatupatia JK kama alivyoingizwa yeye na Mwalimu, sasa ni juzi tu kina Butiku wameshituka kuwa kama Ben angekuwa kiongozi mzuri toka then ilikuwaje hakuwahi kuwa PM?

It is too late ndugu zangu, tumekwama na hatuna pa kwenda! Hatuwezi kwenda UN au the Hague, Mzee JK ninasema ni yala yale tu, rais wa kuikomboa nchi yetu anatakiwa aamue kuwakumbatia wananchi kabla ya viongozi wenziwe, lakini anytime tunapata rais ambaye tunajua mapema kuwa nani na nani watakuwa viongozi, tumeingiza wine mpya kwenye chupa ya zamani,

Kuhusu IPP, huku nyumbani tunafahamu kuwa walishakuwa compromise siku nyingi yote hayo ni mbinu za Mengi kujihami asilipishwe madeni!
 
Mimi Mugishawe nasema kwamba swala la Salim kuwa Rais wa Tanzania was out of question hakuwa na sifa hata moja ya kuwa Rais na hana cha kutueleza kama mfano wa kumfanye awe na heshima mbele ya Tanzania na Africa kama kiongozi shupavu.KUongozwa nw aMwarabu could have been a tragedy maana Watanzania tupo na uwezo wa kuongoza tunao .

Kikwete Mimi sitasema sana nangoja miezi 6 hapo nitakuwa na la kusema ila mwelekeo wake bado una utata mkubwa .
 
Mugishagwe
Kuhusu uongozi wa JK, sidhani kama kuna utata wowote. He is not for real PERIOD! Sikiliza hotuba zake, angalia conferences:domestic and foreign. Nothing genuine.

Nahisi tatizo linalotukabili wengi ni kwamba tunashindwa kuamini kama kiongozi tuliyedhani anaweza kufanya makubwa kwa taifa, ndiyo anayofanya haya......NOTHING! Empty promises.......
 
Mimi sio kwamba nilikuwa namtetea Salim , ninachopinga mimi na nitakachoendelea kupinga ni vigezo vilivyotumika kumnyima huyu bwana Urais ! Jamani kilichofanywa na wana mtandao ni discrimination mbaya kabisa inayogusa rangi ya mtu . Jamani lets put ourselves in salim position and tell me how would you have felt ?

Watanzania wamepata kile walichostahili , JK sio kiongozi ambaye tulikuwa tunafikiria atatupeleka katika promised land . Kwanza anajaribu kufanya mambo mengi sana wakati mmoja . Pili bado huyu bwana ajatambua role yake kama rais , aingii akilini kwa rais kusikia jambo na kisha kulirukia , polisi kapigwa risasi kesho yuko muhimbili kumpa pole , simahanishi kwamba ni jambo baya lakini kuna watu wengi sana wanaweza kwenda hospitalini .

Tatizo kubwa watanzania tunatumia mioyo yetu katika kufikiri , watu wengi wanampenda JK kwa sababu tuu anajichanganya ! Lakini ukiwauliza jee huyu mtu mnaijua track record yake tangu akiwa wizara ya fedha , wizara ya nje na hata wakati akiwa kule nachingwea kama katibu wa chama ? watu tisa kati kumi watakuambia wanaijua ila watasema wakati huo hakuwa rais ndio maana hakufanya mambo mengi ya maendeleo kitu ambacho ni cha uongo " Totally insane".


Jamani mimi baada ya JK kutangaza baraza la mawaziri ambalo ni kubwa kuliko yote katika historia ya Tanzania na kutengeneza baadhi ya wizara simply kwa ajili ya kuwapa wanamtandao ajira nikajua IT'S OVER.

MZEE ES

Nimesoma magazeti mengi naona siku hizi Emmanuel Nchimbi hawamuiti Dr tena, vipi imekuwaje ? hau ameona ishu inaenda pabaya kwa hiyo kawaomba waandishi ? Nilifurahi sana na nikaona madongo ya bcs yalimfikia.
 
Mzee Es,
samahani mkuu bado nitatofautiana na wewe ktk issue hii. Watoto wa wakubwa wote nchini wamesomeshwa na baba zao..
Naposema wamesomeshwa na baba zao nina maana kwamba kutokana na majina ya baba zao vijana hawa wamepewa nafsi za masomo nje kwa kutumia mfuko wa serikali hali vijana hawa hawakufaulu vizuri kuliko wengi Watanzania ambao hawakupata nafasi hizo. Na msisitizo wa baba zao kuhakikisha wanasoma nje ndio kilichokamilisha masomo yao nje. hakuna hata baba mmoja aliyetoa fedha zake mfukoni na wala hii haikuwa maana yangu. Nyerere alikataa kabisa kufanya hivyo (kutumia jina lake), Pili urithi sio lazima elimu kama ulivyosema. Ila mzazi kutambua kipaji cha mwanane na kumsaidia aweze kufikia malengo yake. Nyerere na wazazi wetu wengi hapa TZ hawana tamaduni hii ila wachache sana wanaojitokeza na kutamba leo hii.
Wao madai yao ni kwamba waliweza kupata utajiri ama elimu zao bila msaada wa baba zao kwa hiyo na sisi tujifunze kutafuta wenyewe...
Udhaifu huu upo tu kwa mwafrika... kwa sababu wenzetu utakuta kampuni imeanzishwa toka 1740, leo bado inaendeshwa na wajukuu na kwa ubora zaidi. Sisi waafrika baba akisha kufa na biashara imekufa. hakuna mzazi anayeuandaa mwanae kurithi isipokuwa naweza kusema wachagga.Wachagga kama sikosei mtoto wa mwisho wa kiume ndiye mrithi na wazazi hujitahidi mtoto huyo kuwa na elimu ya biashara ama mradi wa mzazi...Nadhani mfano mdogo ni Free.
Kuhusu swala la nyumba JK amekomesha zoezi la kuuzwa nyumba toka hapo alipoweka mkataba kutengua maamuzi ya Mkapa sawa na Bush kwa ile issue ya Clinton. Hata Bush hakuweza kurudi nyuma na kuwahukumu wale wote waliojihusisha ama kufanikiwa na sheria ile ikiwa chini ya Clinton. Hii ndio maana yangu.

Je, JK anafanya kazi nzuri?Kusema kweli hadi sasa bado nashindwa kumhukumu kwa sababu sijaona mapungufu zaidi ya hiyo baraza la mawaziri. Mikataba na ahadi zake anazifanyia kazi. hakuna kati yetu anayefahamu nini atarudi nacho toka huo msafara wake, na kama tutamhukumu kwa sababu hiyo basi hapo sina la kuongezea. Ila tukumbuke akifanya yote kwa ahadi zake tusirudi nyuma na kusahai haya madongo yetu. Subira nadhani nmdio muhimu hapoa. Tuzichambue ahadi zake na hasa zilizompa kura kisha tupime mafanikio.
hayo ya Uchaguzi CCM nadhani hatuna haja ya kuyazungumzia kwani hatuwezi kubadilisha kitu na wala sioni kati yetu anayependa kuona mabadiliko. JM kuna wengi hawampendi wal kudhani anaweza kuwa kiongozi mzuri sawa na Salim ama Sumaye. nafuu yetu kusema kweli ni huyu JK hadi hapo miaka mitano ijayo.
 
Tausi,

Mzee Nchimbi sasa hivi anatafuta ukatibu wa CCM baada ya Mangula mwakani, sasa anajua kuwa kuna watu kama Ditopile ambao nao wanatafuta huo ukatibu, na anjua kuwa it will get very ugly! Kule ndani ya bunge sasa hivi kila siku habanduki karibu na JM, lakini tayari kampeni zimeshaanza na neno kubwa against yake ni kuhusu Elimu yake, kwa hiyo ni kwa kujitayarisha ndio maana akawaomba media walitoe hilo la Dr......,

sio kwamba hana udoctor!, no anao lakini anajua kuwa una utata ndani yake, kuhusu bongo ndio hivyo tunavuna matunda tuliyopanda, mzee JK amenishangaza sana kukwepa maswali ya kweli huko nje ya nchi ambako mko nyinyi mnaoona kuliko sisi wa ndani, na nyinyi you have nothing to lose kama sisi huku, sasa ni clear kuwa maswali yenu ndio anayoyahitaji sio yetu huku ya compromise, lakini tutaendelea tu kuwapigia kelele hatuwezi kukata tamaa kwa sababu bongo ni yetu wenyewe,

kwenye baraza la mawaziri ni aibu hata kulizungumzia, ndio maana ninashauri kuwa wabadilishane na makatibu wakuu wa wizara ambao wengi wao ni wataalamu wa kweli, watu kama kina Mwakapugi, Mapunjo, Mama Nyoni, Mkama, Mutalemwa, na wengineo hawa ni wataalamu wa kweli, sasa ninashindwa kuelewa kwamba ilikuwaje akaweza kuchagua makatibu bomba akshindwa mawaziri?
 
Tausi 1 said:
Mimi sio kwamba nilikuwa namtetea Salim , ninachopinga mimi na nitakachoendelea kupinga ni vigezo vilivyotumika kumnyima huyu bwana Urais ! Jamani kilichofanywa na wana mtandao ni discrimination mbaya kabisa inayogusa rangi ya mtu.......?
........ JK sio kiongozi ambaye tulikuwa tunafikiria atatupeleka katika promised land


Tausi 1
Swala la Ndugu Salim na ati huo uarabu wake nami nakubaliana nawe, kwani huo ni ubaguzi wa ajabu na wa aina yake...Si kitu kizuri hata kidogo kwani ina maanisha kuwa kesho na keshokutwa tunaweza kumkataa kiongozi anayefaa kisa tu ati babu au bibi yake alikuwa na kijidamu cha Uarabuni, Uzungu, uhindi au hata Uchina, je nchi itaendelea kweli kama tutaendela na vigezo dhaifu hivyo?? Nimeanglia kwa kina post za badhi ya wachangiaji zikisema aah. huyo mwarabu no way!!, Pia ikaulizwa je amefanya nini nchini? Swali langu je hawa viongozi wengine mabomu wa kutupwa wemefanya nini nchini?? kama si kuingamiza zaidi nchi yetu mbayo ipo hoi bin taabani tayari?? Baadhi ya viongozi wanajulikana wazi kuwa walinadi au wananadi kila kitu kilichopo usawa wao, iwe ni benki, Tanesco, Maji nk kwa wageni wanaokuja kunyonya tu, na wanaviuza kwa bei karibu na bure je, uzalendo wa viongozi hao uko wapi?? upo kwenye rangi au matumbo yao??

Kesi ya Huyu Salim tena inanisikitisha kwaniMiaka ya 80 alikosa ukuu wa UN kisa ni mwafrica kutoka "Black Africa" yaani kusini mwa sahara...cha ajabu ni kuwa uraisi wa hiyo nchi iliyosababisha akakosa huo ukuu wa UN wanamtema tena kisa si mbongo je yeye aende wapi??

Jengine ni kuwa Nadhani tetesi zinasema baadhi ya maraisi wetu nao hawakuwa wabongo, bali walivuka mpaka na wazazi wao na kuingia nchini je uraia wao mbona haukuhojiwa?

Swala la JK kuwa ati hafai au ni bomu, nadhani hilo itabidi tusubiri baada ya miaka kumi ndo tutajua. Kwa sasa naona kaanza kwa kasi ya kuridhisha sijui hapo baadaye. kwani hata wa awamu ya tatu alipoingia nakumbuka tulimwita "Mr Clean" hakuwa na doa au dosari, sijui alianza kuharibu vipi au wapi...Bali nionavyo ni kuwa karibu kila kitu kikawa kishapigwa mnada kwa bei ya kuokota. Pia baada ya miaka kumi naona karibu vigogo wote ni mabilionea (waliokuwa kwenye timu yake nk)!!

Ikitokea kuwa kwa bahati mbaya JK akatupeleka pabaya zaidi nadhani hatakuwa wa kwanza au wa mwisho labda tu tuwe tushaingiwa na akili kuwa rangi ya mtu si tatizo bali tatizo ni uzalendao wa huyo mtu na utendaji wake wa kazi.

Si mnaona JJ Rawlings aliyekuwa Rais wa Ghana alivyoisaidia?Rangi yake haikuwa sababu ya yeye kutoindeleza nchi yake anayoipenda kama raia mwingine yeyote.
 
Mheshimiwa,

Wako Watanzania kibao wanaoweza kuwa marais wa bongo na wana uwezo na vitu vyao vimeonekana, watu kama Kaduma, Mramba, Asha Rose ni viongozi ambao wanaweza kuiongoza hii nchi na ikaelekea inakotakiwa na wakatuwakilisha mahali popote kama Watanzania, hatuhitaji waarabu, aliyesema "Mwarabu No way!" ni mimi Mzee Es na ninarudia kuwa bongo hatuwezi kutawaliwa na waarabu, UN alikataliwa na Reagan kwa sababu nyingi mojawapo ikiwa ni pamoja na uarabu wake,

Let me get this straight, waliompiga vita huko yaani Mtandao walikosea kitu kimoja tu, nacho kumtumia rais anayetoka kumpiga vita they did not have to that, kwa sababu record ya Salim ni clear kutoka CIA kuwa alihusika na kifo cha Karume, na kwamba alipelekwa na Babu Cuba na wenziwe kina Mahfudhi kufundishwa ukomaandoo kwa ajili moja tu nayo ni kuja baadaye kuipindia serikali ya ZNZB. Alipogombea UN, Reagan alipewa faili la Salim na akamuita ili akanushe yale yaliyokuwemo kwenye faili akashindwa, serikali yetu chini ya Mwalimu akjaribu kufuatilia wakaishia kupewa copy ya hilo faili, ambalo baadaye kuna mtu alili-leak kwa baadhi ya viongozi wa ZNZB, ndio maana kwenye uchaguzi wa mwaka 1985 juhudi zote za Mwalimu kumpitisha Salim ziligonga mwamba kwani ni wazanzibari wenziwe walioweka mguu chini na kumuonyesha Mwalimu lile faili ambalo lina mambo mengi ambayo mengine hatuwezi kusema ni aibu juu ya Salim, sasa kisiasa Salim alitakiwa kuanza na Zanzibar si ndiko anakotokea kwa nini asigombee urais wa huko kwanza alikotokea na baadaye agombee bara?

Watanzania sio wajinga mzee, ndio maana safari hii yale mambo ya kusema zamu ya rais wa ZNZB tumekataa na hayatarudiwa tena, kwani hayamo kwenye katiba ya nchi rais atatoka bara tu bro!

Rawlings hakuwasaidia kitu wa-Ghana, ambao mpaka leo wanaenda kulia kwenye kaburi la Nkurumah kila siku, halafu nashangaa jinsi unavyoweza kumsifia kiongozi aliyepindua nchi, kama angekuwa kama unavyosema basi angegombea kura kwani kama ni kupindua hata Salima akipindua hakuna atakaye mkataa, lakini kwa njia ya kura alikataliwa kule Dodoma, Rawlings hakugombea kura bro! na halafu hajawasaidia kitu huko Ghana, njaa ni ile ile tu kama ya bongo!

Kuhusu Mzee JK sio lazima wote tusubiri miaka kumi, NO! dalili zimeshaanza kuonekana, rais wako anapowakimbia wananchi huko NY, halafu huko DC wakapandikizwa wazee wawili kuuliza maswali ya compromise, halafu yakaruhusiwa maswali mawili tu! Something is wrong na hiyo serikali sasa hatuwezi kuachia midomo wazi hadi baada ya miaka kumi ndio maana tunaanza sasa kusema kuwa serikali mpya ina matatizo, serikali amabayo tayari imeshaanza kujigamba kwamba imeomba na kupewa hela nyingi itatufikisha wapi? Rais wa bongo anaposafiri na watu 50, mpaka nchi nyingine zinashituka sisi watanzania tukae tuuu kimya eti tunasubiri miaka kumi!

Salim ni mwarabu aliyetokea Zanzibar, basi akaanzie huko kwanza tuone lakini bara hatuwezi kuongozwa na mwarabu wakati wabongo kibao wapo wenye uwezo, hakuna ubaguzi hapa ni ukweli bongo ni ya wabongo na tupo ni sisi, wenye uwezo wapo lakini system imewanyima nafasi lakini pole pole ipo siku watanzania watadai kiongozi mwenye uwezo kwani hii tabia ya kuchaguana kwa ujanja haitadumu daima kwani kadri wanavyoshindwa kuongoza ndivyo wananchi wanajifunza, ndio maana safari hii suala la rais atoke Zanzibar lilizimwa mapema maana wanachi hawajasahu mambo ya Mwinyi, na take it from me baada ya huyu rais wa sasa wananchi hawatarudia tena kuchagua rais maarufu asiyekuwa na record!
 
Weweeeeeeeeeeeeee Choveki tulia kwanza na hadithi zako .Ama wewe ni mwana mtandao ama unajifunza mambo hapa Duniani.Mzee Es nakubaliana nawe kwa point ya Salim .Salim ni kitu gani bwana klwa Tanzania ? Salim amlaumu BWM aliyemwengua kwa kashfa za wazi huko Dodoma lakini kwangu mimi Salimu alikuwa ni Kibaraka wa Waarabu akiwemo Ghaddafi.Leo mtasema Ghaddaf ni mwana mapinduzi Hell no siyo kabisa ana malengo yake .

Salimu amekaa OAU kaondoka kwa aibu kisa anamsikiliza mwenye pesa wa Libya .Salimu alikuwa kiongozi wapi akafanikiwa jamani ? Pamoja na mengine mengi aliombwa aondoe jina lake AU na Ghaddaf alkipinga na akataka kukataa ku sponsor transformation ya AU ndipo Waafrika wa West Africa wakamwambia hawaondoi majina yao na Salimu ataumbuka akasoma alama za nyakati akaachia leo unasema Salimu wa wapi huyu ???

Es nakupinga kwa kasi kwamba Migiro na Mramba wanaweza kuongoza Tanzania usawa hapana.Migiro namwacha kwanza namchukua Mramba ambaye amejenga ubaguzi wa hali ya juu Hazina .Nenda TRA na Hazina uone alivyo wamwaga Wachaga hadi huwezi kuamini kunani huko .Mramba hafai na labda wewe useme ni mwana mtandao wa kinamna maana akina Migiro ni wana Mtandao ambao wako na Rais wa Ziara na si Rais wa Watanzania .

Nasema yes kuna watu zaidi ya Mramba na Salimu wanaweza kuongoza Tanzania nikiwemo mimi mwenyewe bwana .
 
Mzee Es na wengine! Nimefuatilia hoja zenu kwa makini, na hapa nitajaribu kujibu tu juu ya SAS.

a. Mtanzania ni nani? Je kila mtu mweusi anayeishi Tanzania ni Mtanzania? Je kila mtu mwenye kuchanganya damu si mtanzania? Kwa maoni yangu (na nadhani sheria iko upande wangu) Mtanzania ni yule mwenye kutimiza masharti yanayofahamika ya Uraia. Je SAS ni mtanzania kwa masharti hayo?

b. Je mwarabu anaweza kuwa Mtanzania kwa kuzaliwa na kwa kuchagua? Bila ya shaka! Je Mhindi anaweza kuwa mtanzania? Bila ya shaka! Tanzania na CCM wenyewe wameshakubali kuwa rangi si kitu tunao wahindi wengi na waarabu ambao leo hii wanawakilisha watu weusi kwenye Bunge!! Wamechaguliwa na watu kwa sababu ni Watanzania na wametumia haki yao hiyo. Tatizo la kukataa "kutaliwa na mwarabu" ni tatizo baya sana kwani linatokana na ubaguzi mtupu! Je Tanzania iko tayari kutawaliwa na Mchagga, Mnyakyusa, au Mhaya? Kuna watu watasema "Hapana! Hatuko tayari kutawaliwa na watu hao" Kisa na mkasa... ? ni makabila yao!!

c. Nakubaliana na wewe kwenye hoja ya SAS kwamba asitawale Tanzania kwa sababu moja tu nayo ni rekodi yake na sifa zake kama kiongozi!! Itakuwa ni kujidanganya kuwa mtu mweusi wa Tanzania basi ana uchungu zaidi na ana uwezo zaidi wa kuitawala nchi yetu! (Ushahidi unaonyesha vingenevyo). Kama SAS alikataliwa kwa sababu ya rekodi yake ya uongozi na historia yake kama kiongozi hiyo ni sawa, lakini kumkataa mtu kwa sababu ya rangi yake, ni uonevu mkubwa, kinyume na utanzania wetu, na zaidi ya yote ni kitendo cha kibaguzi ambacho watanzania tumeupinga tangu tuwe Taifa!! Ninawasihii wazee wenzangu tusianze leo ubaguzi huu... Kwa sababu mwisho itakuwa "Wahutu hawawezi kutawala nchi...let's kill em!"

d. SAS kukataliwa na Reagan, haituhusu, Reagan hakuwa Mpaka Mafuta wa Wafalme kama Nabii Samuel!! Hivi tukichagua viongozi wetu kwa kufuata baraka za wakubwa tutafika kweli? Miye binafsi sijali Reagan alionyeshwa nini kwenye faili la SAS ambaye aliwahi kuwa Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa. SAS alikataliwa na wakubwa sababu ya Uislamu wake na siyo Uarabu wake. Ndo maana hata wakati ulipofika kwa nchi za kiarabu kutoa Katibu Mkuu Mpya, hawakumtoa Muislamu bali Mwarabu Mkristu (Boutros Boutros Ghali)!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom