Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mwanza. Baada ya chama cha CHADEMA kutakiwa kufanyia marekebisho mara tatu hati ya kufungua maombi ya kesi dhidi ya Polisi, hatimaye imekubaliwa na inaanza kusikilizwa leo.
Kesi hiyo ambayo awali ilikuwa ikisikilizwa na Jaji, Mohamed Gwae sasa ikomikononi mwa Jaji, Sirolius Matupa
Awali shauri hilo lilifunguliwa Juni 10 likiwa na wadaiwa wanne likaondolewa na kuwasilishwa tena Juni 15, mwaka huu kwa kuondoa wadaiwa wawili na kuwabakiza wawili.
Katika hati ya Juni 10, ambayo ilifanyiwa marekebisho kutokana na hitaji la kisheria linalotaka walalamikiwa washtakiwe katika maeneo yao, wadaiwa walikuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kahama, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Nyamagana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Katika hati ya Juni 15, walibaki Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza na Wilaya ya Nyamagana