Hatimaye Kafulila na Mbatia Jukwaa moja kata ya Bashneti..

April

Member
Nov 14, 2011
35
21
Baada ya kuwa na mgogoro uliodumu zaidi ya mwaka mmoja, hatimaye Mh. Kafulila na Mwenyekiti wake Mh. James Mbatia wahutubia jukwaa moja kata ya Bashneti huko Babati kwenye Uchaguzi mdogo wa Madiwani.

Mkutano huo uliokuwa mkubwa sana kuwa kivutio kwa wengi, waheshimiwa hawa ilikuwa mara ya kwanza kwao kusimama jukwaa moja tangu mgogoro wa chama hicho mwishoni mwa mwaka 2011 uliopelekea wafikishane mahakamani. Ushirikiano huo waliouonyesha unatufundisha kwamba, viongozi wafike mahali watangulize maslahi ya wananchi wa Taifa wanaloliongoza kabla ya maslahi yao wenyewe, hii migongano ya kimtizamo isiwe vikwazo kwa viongozi kushirikiana panapo maslahi ya wananchi.

Big up Kafulila na Mwenyekiti!!
 
Mbatia mtu fresh sana,namkubali!,Kafulila nimefurahi kuskia mpo pamoja mungu hawasaidieni,kusamehe kupo.sasa yule Slaa kusamehe ajui kabisa kama vile hakusoma manemo ya mungu,kama yeye yuko hivya sasa sisi maamuma itakuaje!!!!
 
Mkutano huo uliokuwa mkubwa sana kuwa kivutio kwa wengi

Una kapicha japo kamoja tu ulikofanikiwa kupiga ili kuthibitisha maneno yako? manake hata ccm walituambia wamejaza watu katika mkutano wa Themi, walipokuja kuweka picha tukaishia kushuhudia shamba la mahindi badla ya mamia ya wananchi kama walivyokuwa wamejigamba.
 
Mbatia na Kafulila ni Condo.. za kiume zinazotumika na CCM kwa mtindo tofauti tofauti.
Kuna ya chocolate flavor, Pineapple flavor nk lakini ni kutoka kampuni moja inayoitwa NCCR.
 
Tujenge tabia ya kuappreciate positive attitudes sio kila mtu mamluki jamani
 
Back
Top Bottom