Hatimaye JWTZ yaingia Kibiti, Ikwiriri na Mkuranga kudhibiti na kutafuta wauaji wa Polisi na RAIA

Mkuu hao watu lazima wataleta madhara makubwa kuliko faida nakumbuka mwaka 2013 nilikuwa Mtwara ikatokea vurugu za gesi ikabidi Serikali ilete wanajeshi waikalie Mtwara kijeshi mkuu wamakonde wote walinyooka sitokuja kusahau

Siku moja wakati tupo soko kuu tuliletewa JWTZ wakiwa na Vifaru vya Kivita dhidi ya wananchi ambao hata panga hawana!!!
 
tatizo saivi nchi hii mbwembwe nyingi yaani kila mmoja anaiga kwa boss kubwa,mishembenduo kibao hili la kibiti polisi wangekuwa keen and well organised wangelimaliza mapema mno
 
Breki ndo zimewekwa na muziki ndio umewekwa sasa kitaeleweka tu nilikuwa naombea sana wapelekwe hawatakagi utani wale kazi kazi tu...
 
Mwenyezi Mungu alijaalie Jeshi letu, liweze kufanikisha wananchi wa viunga vya mkoa wa pwani hususan Mkuranga,Kibiti,Ikwiriri n.k waweze kuishi kwa amani kama watanzania wengine,

yameulizwa maswali mengi kama wanaenda kupambana na nani? mbona adui hajulikani?

lakini ni vyema mkakumbuka hata hao ndugu zetu wanaouawa hawafi kwa ugonjwa wa shinikizo la damu au Malaria, kuna watu waovu wanaokuwa ni chanzo cha Vifo vyao, maadam vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vimepewa jukumu la kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo waishi kwa usalama kama zamani,

sisi raia tunapaswa kutulia na kuunga mkono jitihada hizo, ukitaka kujua thamani ya amani pata nafasi kutembelea nchi ambazo usalama wake umekuwa wa kutiliwa mashaka, tusiruhusu hilo litokee Tanzania, siku zote mbwa mzuri hafundishwi namna ya kung'ata,Vyombo vyetu vimepewa kazi tuwape nafasi wafanye kazi, tunafahamu wameshafanya operesheni nyingi, hatarishi na ngumu zaidi ya hii nitumaini langu wataifanya vyema na sote tutaridhika,

Together we can, May the GOD bless the United Republic of Tanzania and Africa in general, Those are my views!
 
Ina maana IGP na waziri wake wa mambo ya ndani wameshindwa...
Ina maana CDF na waziri wake wa ulinzi ndio mwarobaini mpya...

Tuwatose basi hao walioshindwa!!
 
Jaman tuache kubeza Kwani hayo mauaji yameanza Leo ukiona mpka jwtz wameingilia kati basi jua usalama wa taifa. Wameshindwa police wameshindwa na kiini kimeshapatikana ndo maana ukaona nguvu kubwa inaenda kupambana soma gazeti la Leo utaona adi majina yametajwa wanaotafutwa .Ndugu ukifanya maovu ata kama binadamu wote watashindwa kukutambua basi ipo siku miti na wanyama wataongea kukufanya uonekane mbele ya hadhira kwahiyo kikubwa ni kuwaombea wafanikiwe maana walio enda uko ni Ndugu zetu kaka zetu baba zetu na watu wetu wa karibu katika jamii na kikubwa kngine tunaishi nao vizuri mtahani kwetu.
 
Mh.Rais alijua IGPMangu katulia tu,kumbe syo hvyo_Ona sasa wanavyomtesa IGP Sirro majamaa hawalazi damu
 
Uhalifu wa Kibiti ni uhalifu mgumu kupambana nao, hata JWTZ wanaweza kushindwa kutokana na kupambana na mtu usiyemjua 100%.

JWTZ ingeweza kupambana vizuri endapo adui angekua anajulikana, hatuombei yaendelee ila najaribu kuwaza endapo Jwtz watashinda tutampeleka nani?

Bora kupambana na Alshabab ambao unajua wanakambi na ngome sehemu flani kuliko kupambana na wahalifu wa kibiti
 
Time will tell, stay tuned long time since I kill M23
c354a967034c2ca5ef6b681a16632381.jpg

imani kubwa
 
hii vita wangewatumia watu wa usalama wa taifa wangewini vizuri maana wangewapeleka kama waajiliwa wa sector mbali mbali kupata data zote,Lakini hawa sdhani,
Unajuaje kama hawajafanya hayo unayoshauri?
Kupeleka jeshi ni mbinu tu.Mchezo Mzima umekamilika.
Hio ndio sifa ya jwtz.
 
Hilo gazeti limechelewa kupata habari hii, wanajeshi wakiwemo makomando kutoka 92 KJ wapo huko kitambo tu tangu askar na maafisa wa polisi wauwawe kinyama na maharamia.
Kama wameamua kuongeza nguvu tena ni vyema. Ni vizuri kupeleka jeshi la ulinzi maana ndio wenye mamlaka ya kumuua adui nyemelezi, pia mafunzo ya JWTZ yako advanced kidogo ukilinganisha na ya polisi wetu.
 
Nimekuelewa vizuri Sana. Ishu ya Kibiti inahitaji akili zaidi kuliko Wapasua matofali. Lazima chanzo kijulikane maana Kama si hivyo hawa jamaa watahamia sehemu nyingine
Maafisa wetu wana ujuzi wa mbinu za medani kuliko unavyofikiri.
Kibiti itatulia soon. Mwaka 1990 Kule Mugumu ilikuwa kama hivi. Uliza Leo kama kuna ugaidi.
 
Nina imani na Jeshi letu hili. Ninafahamu hawtakubali kuvalishwa aprons za pumpkins (colors) na bashite.
Wataendelea kushikilia bendera yetu yenye rangi nne. Ni idara pekee ambayo bado inabeba bendera yetu, na siyo bendera ya genge la wahuni kama wale wengine.


Mungu awatangulie na kuwafanikisha sana!. Rufiji kuna magaidi. Bila shaka Mungu atawashika Mkono hawa makamanda wa ukwlei, hawataua watu wasio na hatia, lakini watawatia nguvuni wahusika wote wa ugaidi huu na kuwa disarm ikiwa ni pamoja na ku dismantle kabisa genge lao kwa kung'oa mizizi yote.

Mungu awatunze na kuwaongoza wamalize kazi salama, asiwepo wa kupoteza maisha. Ninatamani kuwe na survey za anga na viona mbali ili wafanye 24 hrs surveillance kubaini movements na establishments zilzokweney misitu ya kule pamoja na baharini.

Nendeni kwa amani vijana wetu na mrudi na ushindi!. Kama jinsi Mungu aishivyo, ninawakabidhi bendera yetu iwe ndiyo nembo katika mioyo yenu!.

images


Mwende kwa Amani kwa kuwa mtashinda.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afirca, Mungu Ibariki Israel!.
Kweli watanzania wengi ni vichaa kama huyu hapo israel inaingiaje
 
Back
Top Bottom