HATIMAYE John Tendwa akubali kukutana na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HATIMAYE John Tendwa akubali kukutana na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Oct 20, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tendwa sasa anywea kwa Chadema


  Na Khamis Mkotya


  HATIMAYE Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekubali kukutana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kuwapo mvutano baina yake na chama hicho.

  Hatua hiyo inalenga kumaliza tofauti zilizopo baina ya msajili na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

  Jitihada za kutafuta suluhu hiyo inafanywa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Dk. Emanuel Makaidi, ambaye ameingilia kati uhasama huo.

  Akizungumza na Mtanzania jijini Dar es Salaam jana, Dk. Makaidi alisema anasikitishwa na uhusiano tete uliopo baina ya vyombo hivyo viwili.

  Dk. Makaidi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NLD, alisema amefungua mlango wa kutafuta suluhu baina ya msajili na chama hicho kwa faida ya taifa.

  Chadema ilisitisha uhusiano na ofisi ya msajili na kulazimika kutangaza mgogoro na kiongozi huyo kutokana na kuchukizwa na kauli yake ya kutishia kukifuta chama hicho.

  Msajili alitishia kufanya hivyo kwa madai kuwa chama hicho ndicho kilichosababisha mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel tena, Daud Mwangosi.

  Dk. Makaidi alisema licha ya kuanzisha jitihada hizo kwa muda sasa, lakini jitihada zake zimegonga mwamba baada ya kushindwa kukutana na viongozi wa juu wa Chadema.

  Dk. Makaidi alisema uwamuzi wa kutafuta suluhu hiyo ulifikiwa katika mkutano wa wadau wa siasa ulioitishwa hivi karibuni na Tendwa, ambapo Chadema haikuhudhuria.

  "Chadema na msajili wa vyama wote ni wadau wa siasa, kwa hivyo misimamo yao hii ikiendelea itakuwa haina tija kwa taifa zaidi ya kuendeleza chuki na uhasama.

  "Chadema kususia shughuli za mtu aliyewasajili, hii si sawa na pia msajili kutishia kukifuta chama tena chama kikuu cha upinzani alichokisajili mwenyewe pia nayo si sawa.

  "Kwa kutambua hilo, ndipo tunapotafuta suluhu. Tunataka wakutane wazungumze na kujadili waone namna ya kumaliza tofauti zao badala ya kila mmoja kubaki na msimamo wake.

  "Pamoja na kwamba nimeshindwa kukutana na viongozi wa Chadema, lakini nataka wananchi wajue zipo jitihada zinazofanywa za kurejesha wao," alisema.

  Hata hivyo Dk. Makaidi alisema tayari msajili huyo amekwisharidhia kukutana na viongozi wa chama hicho ili kumaliza tofauti zao, baada ya kufanyika kazi kubwa.

  "Oktoba 16 nilikwenda kwa msajili, pamoja na kumweleza kushindwa kwangu kukutana na viongozi wa Chadema, nilimwomba msajili afanye kila analoweza akutane na viongozi wa Chadema.

  "Awali msajili alipinga wazo langu akisema kuwa atawezaje kuwaita watu ambao hawamtambui. Lakini nafurahi baada ya ushawishi mkubwa hatimaye msajili alikubali.

  "Wapo watu wanaoweza kubeza na wengine wakaona kama Chadema wanabembelezwa. Hapana, katika hali kama hii ni vigumu kuiepuka Chadema katika mazungumzo.

  "Kwanza Chadema ndiyo official opposition (kambi rasmi ya upinzani) bungeni. Pia ni chama kikuu cha upinzani nchini, hakuna namna ya kuikwepa.

  "Napenda kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wa Chadema wakiitwa na msajili wakubali ombi la msajili ili kumaliza tofauti zilizopo. Kuendelea kubaki na msimamo haitusaidii kama taifa," alisema.

  Akizungumza na Mtanzania kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa.  Mnyika alisema chama chake kilikwishapeleka barua Ikulu kulalamika namna kinavyohujumiwa na kueleza kuwa wanachosubiri kwa sasa ni majibu ya barua hiyo na si vinginevyo.


  Source: Mtanzania   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nilijua tu. Ameona dhouruba kali ya M4C ambayo ilikuwa inamnyima usingizi, hasa akifikira baada ya muda wake atakuwa raia tu wa kawaida!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu mjamaa ameanza kuuhofia ukada wake wa chama cha magamba! Huwa nashangaa kwa nini hjataki kuwa neutral , Haiduru angekuwa anakaa kimya kama vile yule aliyemtangulia, George Liundi. Wakati wa vuirugu za kisiasa kati ya serikali na NCCR, na baadaye CUF, Liundi alikuwa haropoki na kupayuka ovyo kama huyu mjamaa!
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  you can smell fear in tendwa a thousand miles away..old is gold but for this old man old is bald and nothing else..
   
 5. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Safi sana Dr. Makaidi wewe yaelekea unasoma ramani za upepo utokako na kule unakoelekea. Big up kwani busara ya U-DR wako imejidhihilisha bayana bila chenga. Mimi binafsi nawashauri wapiganaji wangu wakubali ushauri huo, kumbuka mkono ukigusa mavi huwa haukatwi bali huoshwa kwa maji.
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  tungelikuwa na madaktari wa hivi hata kule ccm basi tanzania ingekuwa mbali sana ...Dr.umekuwa mkweli sana!
   
 7. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  aiseee babaangu hiyo barua yetu imekwenda ikuli gani hiiii ya magogoni au ikulu nyingine??? manake ikulu ya magogoni siiamini hata kidogo wanaweza sema imepotei barua yetu
   
 8. S

  SINDBARD Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbinu za magamba kuidhibiti cdm zinazidi kugundulika na kufeli sijui hili la udini walilolipandikiza lazima ifikapo 2015 litakuwa limekwishawamaliza
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Maigizo haya wawapelekee wasiojua kiswahili.
  Tendwa amechemka sana, afute kwanza kauli yake ya kutishia kuifuta chadema, kauli inayoonyesha chuki ya moja kwa moja.

  Amempanga mzee makaidi kanakwamba asomeke ni mpatanishi, kinachopaswa ni kumhukumu huyu joni tendwa kwa kuyatumia madaraka yake vibaya. Chadema mkiitwa na huyu kibabu mwambieni afute kwanza tishio lake, manake mkienda kabla hajafuta kauli mnaweza kujikuta mnakabidhiwa barua ya kufutwa rasmi.
   
 10. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Anyway taarifa inaonesha suluhu bado iko mbali.

  Nadhani ilipaswa kuwa hivi; kwa vile Tendwa alilianzisha basi na awe yeye wa kwanza kuitikia wito wa mpatanishi kwa kuiandikia barua rasmi CHADEMA au kutangaza kama alivyofanya awali kuwa anawaomba CHADEMA wakutane ili kujadili na kutatua tofauti zilizopo.

  Ila pamoja na hayo tutaendelea kuwa makini naye maana kaonesha udhaifu mkubwa sana kama binadamu na kama Msajili. Atapewa ushrikiano ili mambo yarudi kwenye normalized status. PERIOD.
   
 11. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Heri wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu
   
 12. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  huo ndio msimamo wa makamanda viva cdm!
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hatimaye Tendwa akubali kukutana na CDM? Ni lini Tendwa alisema hataki au hawezi kuktana na CDM?
   
 14. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ni vema viongozi wa CDM wakakutana na Msajili pamoja na yote itakuwa pia nafasi kwa CDM kumuweka sawa kwa kumpa darasa hata hiyo barua iliyotumwa magogoni apate copy.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Spin masters...
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu nadhani hiyo heading haipo sawa! Hapo wakukubali kuongea na mwenzie ni cdm na sio Tendwa maana wao ndio waliositisha ushirikiano! Sijawahi kusikia Tendwa amekataa kuongea na cdm!
   
 17. La Generale

  La Generale Senior Member

  #17
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2012
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna kukutana na huyo kilaza!dawa ni ang'oke tu kwenye hiko kiti cha usajili anachokiona ka mtaji!
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Akanushe upuuzi aliouongea kwenye media ile ile aliyotumia,na aache mambo ya ukada wake kwa CCM
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,840
  Trophy Points: 280
  Ni vyema viongozi wangu wakakubali kukutana nae hili kumaliza hili tatizo.

  Sisi sote ni ndugu!

  Na tendwa aache mchezo wa vitisho vya kitoto!
   
 20. K

  Kompis Member

  #20
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tendwa kama msajili wa nyama vya siasa nchini alipotoka na kuongozwa na jazba na ukada wake kuropoka yale aliyoropoka. Hivyo hawezi kukwepa kubebeshwa lawama hizi za kutoelewana na chama kikuu cha upinzani nchini. <br>La msingi ni yeye kukubali ukweli usiopingika kuwa alipotoka na kukurupuka na kuropoka. Kwa maana nyingine ni kwamba yeye Tendwa anatakiwa kufutwa ile kauli yake ya kutishia kukifuta CHADEMA. short of that nawasihi Chadema kutokubali kukaa meza moja na huyu kada wa waziwazi wa MAGAMBA-period!!!!
   
Loading...