Hatimaye imejulikana: Dereva wa Lissu yuko Ubelgiji, akahojiwe

Its taking too long

Hii inaipa nguvu conspirancy ya kuwa anafichwa.

1) Anaweza kuwa anafichwa ili asifichue kuwa tukio lilipangwa na CDM wenyewe for political reasons

2)Anaweza kuwa anafichwa ili asije nunuliwa na maadui wa Lissu ili asije tumika against yeye.

But huwez sema anatibiwa, anatibiwa nini,muda wote? Semeni anafichwa kwa nin?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi kabisa mkuu.Waliomficha dereva sio WAPUMBAVU hata kidogo. Ukiangalia nguvu kubwa inayotumika kumkingia kifua dereva ni kubwa mno hadi unajiuliza kuna nini?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Ilivyo mkiwa mnafanya uchunguzi na mko serious mtu hata kama yupo mwezini ushahidi utampoint tu kua ni yeye ndiye kahusika.

Nimesahau majina ya watuhumiwa lakini kuna kesi moja ndugu wawili waliua wazazi wao. Walikaa baa na wenzao mpaka usiku mida ya saa sita, wakarudi nyumbani wakafanya tukio kisha wakarudi baa.

Walitengeneza alibi nzuri tu ila uchunguzi ukafanywa na kila ushahidi ukawapoint wao
Mwisho wakakiri kosa.

Pia kuna jamaa alitoka nje ya mji. Watu wa karibu wote wakajua kua hayupo mjini. Usiku akarudi akaua na usiku huo huo akarudi mji alioaga anaenda.

Alimuua mama mkwe au mkewe sikumbuki vizuri. Hivyo kesho yake akapewa taarifa ya msiba na yeye akarudi nyumbani.
Uchunguzi ukaanza, askari walikagua gari la jamaa wakakuta windshield na wipers zina wadudu wa usiku wanaopatikana njiani ukiwa unarudi mji wake.

Yaani kama vile mji uwe Ruaha Mbuyuni halafu wadudu wakutwe wanaopatikana Iyovi.

Akaulizwa kwanini alisafiri usiku kuifuata njia ya kurudi mji wake akakosa jibu hatimaye akabreak akakiri kosa.

Hoja yangu ni kwamba, kama askari wanataka kweli kufanya uchunguzi Lisu au Dereva wake kutokuepo au kuepo haizuii kitu.
Jeshi la polisi linajiaibisha kung'ang'ania kua uchunguzi hauendi kisa wahanga hawapo.

Kama hao wahanga/ mhanga ni wahusika/ mhusika ushahidi utapoint tu.
 
Its taking too long

Hii inaipa nguvu conspirancy ya kuwa anafichwa.

1) Anaweza kuwa anafichwa ili asifichue kuwa tukio lilipangwa na CDM wenyewe for political reasons

2)Anaweza kuwa anafichwa ili asije nunuliwa na maadui wa Lissu ili asije tumika against yeye.

But huwez sema anatibiwa, anatibiwa nini,muda wote? Semeni anafichwa kwa nin?
naona una nia ya kujifunza basi hebu tumia muda wako kusoma post traumatic stress disorder soma kwa undani wake
 
Mbunge Tundu A.M.Lissu amesema kuwa dereva wake waliyekuwa wrote siku ya shambulio dhidi yake Septemba 7 mwaka 2017 huko nchini Ubelgiji.

Lissu ameyasema hayo jana alipokuwa akihojiwa na Mwandishi Mwamoyo Hamza wa Sauti ya Amerika almaarufu VoA. Studioni alikuwepo pia Balozi wa Tanzania nchini Marekani Ndugu Wilson Masilingi.

Kauli ya Lissu juu ya alipo dereva wake inamaliza fununu na ramli kihusu alipo dereva huyo. Kwakuwa imeshajulikana alipo,ni muda muafaka kwa wahusika kusuka utaratibu wa kwenda kumhoji dereva Hugo na Lissu mwenyewe atakayekuwapo Ubelgiji tarehe 20 mwezi huu.
Wahoji nani aliyeondoa CCTV na walinzi siku ya Tukio waanze hapo kabla ya kuchoma fedha za kodi kwenda Belgium.
 
dereva wa tundu lissu inajulikana siku nyingi yupo ubelgiji na amaejiriwa na chuo kikuu ambapo ndio kuna hospitali anayotibiwa lissu na anaendelea kufundishwa kifaransa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katika eneo la tukio HAKUKUA NA MTU YEYOTE?
Mimi nadhani waliotakiwa waanze kuhojiwa ni watu wa karibu waliokuwepo eneo la tukio.
maana tukio limetokea MCHANA.
lissu kabla ya tukio alitoa TAHADHARI KUNA GARI UWA LINAMFUATILIA
NANI ALIYEJALI?
kiufupi kukazana kutaka dereva ahojiwe ni KIINI MACHO.
Nissan NYEUPE utumika na watu wa serikali.ndo magari yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilivyo mkiwa mnafanya uchunguzi na mko serious mtu hata kama yupo mwezini ushahidi utampoint tu kua ni yeye ndiye kahusika.

Nimesahau majina ya watuhumiwa lakini kuna kesi moja ndugu wawili waliua wazazi wao. Walikaa baa na wenzao mpaka usiku mida ya saa sita, wakarudi nyumbani wakafanya tukio kisha wakarudi baa.

Walitengeneza alibi nzuri tu ila uchunguzi ukafanywa na kila ushahidi ukawapoint wao
Mwisho wakakiri kosa.

Pia kuna jamaa alitoka nje ya mji. Watu wa karibu wote wakajua kua hayupo mjini. Usiku akarudi akaua na usiku huo huo akarudi mji alioaga anaenda.

Alimuua mama mkwe au mkewe sikumbuki vizuri. Hivyo kesho yake akapewa taarifa ya msiba na yeye akarudi nyumbani.
Uchunguzi ukaanza, askari walikagua gari la jamaa wakakuta windshield na wipers zina wadudu wa usiku wanaopatikana njiani ukiwa unarudi mji wake.

Yaani kama vile mji uwe Ruaha Mbuyuni halafu wadudu wakutwe wanaopatikana Iyovi.

Akaulizwa kwanini alisafiri usiku kuifuata njia ya kurudi mji wake akakosa jibu hatimaye akabreak akakiri kosa.

Hoja yangu ni kwamba, kama askari wanataka kweli kufanya uchunguzi Lisu au Dereva wake kutokuepo au kuepo haizuii kitu.
Jeshi la polisi linajiaibisha kung'ang'ania kua uchunguzi hauendi kisa wahanga hawapo.

Kama hao wahanga/ mhanga ni wahusika/ mhusika ushahidi utapoint tu.
Hao wote uliowatolea mfano walikuwa wahalifu ndio maana walisakwa Kwa udi na uvumba Tundu Lisu na dereva ni mashahidi polisi hawahitaji kutumia nguvu kubwa na gharama kubwa kuwafuata waliko watoe ushahidi wao wenyewe wafike polisi watoe ushahidi.Utetezi mwingine wa kijinga mfano wewe unavamiwa na majambazi nyumbani kwako.Polisi wanakuita kukuhoji utoe ushahidi ilikuwaje unagoma unasema ningekufa je msingefanya upelelezi? Nendeni kafanyeni upelelezi wenyewe.Kawahojini majirani na mlinzi Mimi sitoi ushahidi siji polisi kituoni kuandika maelezo mkitaka ushahidi nifuateni baa nakunywa ubelgiji mje mnihoji!!!!Hakuna mpelelezi aweza endelea na upelelezi wa kesi ya kibwege kama hiyo
 
Wahoji nani aliyeondoa CCTV na walinzi siku ya Tukio waanze hapo kabla ya kuchoma fedha za kodi kwenda Belgium.
Polisi huwezi wapangia wakuhoji wapi.Tundu Lisu na dereva wao ndio wachome fedha waripoti polisi Tanzania.Ingekuwa ruksa MTU kujipangia ahojiwe wapi hakuna MTU angekubali kwenda kuhojiwa polisi MTU angesema njooni mnihoji nyumbani,guest house ,bar,hotelini nk
 
Swali ni kuwa anafanya nini Belgium? Lissu anatibiwa yeye je?

Au ndo kafichwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila watu mnajitoa akili mpaka basi !!!. Wauaji waliotaka kukutoa roho mchana kweupe hawajulikani walipo pamoja na kuwaona, wala hawasakwi, hakuna anaye guarantee usalama wako nk nk. Halafu wewe ujitokeze na aina ya usaidizi wa police wa ki Tz ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wote uliowatolea mfano walikuwa wahalifu ndio maana walisakwa Kwa udi na uvumba Tundu Lisu na dereva ni mashahidi polisi hawahitaji kutumia nguvu kubwa na gharama kubwa kuwafuata waliko watoe ushahidi wao wenyewe wafike polisi watoe ushahidi.Utetezi mwingine wa kijinga mfano wewe unavamiwa na majambazi nyumbani kwako.Polisi wanakuita kukuhoji utoe ushahidi ilikuwaje unagoma unasema ningekufa je msingefanya upelelezi? Nendeni kafanyeni upelelezi wenyewe.Kawahojini majirani na mlinzi Mimi sitoi ushahidi siji polisi kituoni kuandika maelezo mjitaka ushahidi nifuateni baa ubelgiji mje mnihoji!!!!
Kaka/ Dada umemiss point nzima.

Katika kesi zote nilizotolea mfano wahusika wa matukio hawakuhojiwa. Mfano ni nadra mtu kumuua mzazi wake especially marafiki wa mwanzo wakipoint kua ulikua nao baa.

The same kwa kesi ya pili. Nani atawaza kuna mtu anatamani kumuua mkwewe/ mkewe? Tena mtu mwenyewe yupo nje ya mji?

Kwahiyo askari walifanya uchunguzi bila hata kuwagusa wahusika. Isipokua ushahidi ndiyo ukawa unawarudisha nyuma kwa wahusika.

Katika mfano ulioutoa, average person hawezi kuwaza kua mimi nimejiibia, askari pia atawaza hivyo kwahiyo haitakua kunihoji itakua ni kuchukua maelezo ya siku ya tukio nilikua wapi, nilimuacha nani nyumbani n.k.

Kama nina CCTV wataomba waangalie. Kama picha zilinasa sura nitaulizwa kama namjua/ nawajua. Kama siwajui na wenyewe watacheki kwa wenzao kama hiyo sura siyo ngeni.

Kama wakiikosa, basi wanaiprint wanaisambaza na kufanya open investigation. Anayemjua mhusika atamtaja au atatoa leads.

Kuna kesi nyingi uchunguzi wake umefanywa wahanga wakiwa wamepoteza maisha. Na wahusika walikamatwa.
 
Meta mada unaandika ujinga na Lisu wako Kwa mini polisi watumie raslimali za nchi na pesa za walipa Kodi kumfuata ubelgiji Kwa mini huyo dereva na Lusu wake wasije Tanzania kutoa ushahidi? Hizo pesa Lisu azozurura nazo si zinatosha naulizia ya kumleta yeye na dereva wake kuja kutoa ushahidi Tanzania? Wao sio wahalifu kwenye hiyo kesi ya Lisu kupigwa risasi ni mashahidi wangekuwa wahalifu hapo polisi ingekuwa sawa kutumia mipesa ya nchi kwenda huko ulaya au kutumia ma interpol nk kuwadaka na kuwaleta nchini Kwa nguvu Kwa gharama za walipa Kodi.Wao ndio waje Tanzania sio polisi wa Tanzania waende.Polisi walishatoa taarifa mapema wakimtaka dereva aripoti polisi hakufanya hiyo Afanye hivyo aripoti polisi Tanzania
Mshahoji waliopo nchini?
 
Back
Top Bottom