Hatimaye haki imetendeka. Je, nawezaje kudai fidia kwa fedheha niliyosababishiwa?

scientificall

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
454
314
Kwanza nimushukuru Mungu kwa kuonesha haki na kutenga ukweli na uongo.

Nichukue pia fursa hii kuwashukuru wanajamvi wote hasa waliotoa mawazo, ushauri na kutoa pridiction juu ya kesi yangu. Mawazo yenu na ushauri nimeutumia kwa 100% mpaka kushinda kesi.

Kabla sijatoa nlilokusudia ngoja ntoe maelezo kiufupi juu ya kesi iiyokuwa ikinikabili......
" toka mwezi wa 3 mwaka huu. Kuna jirani alinituhumu kuwa nilimuibia computer na simu 2 jumla gharama ya tsh 950000/-

Uongozi wa chuo ulinitishia sana ili nikubali tuhuma niweze kulipa na mwisho kufukuzwa chuo kwani mshitaki alidai alinishuhudia mimi usiku nikiwa na wenzangu tuna muibia. Kwa kudhani angeweza kulipwa harakaharaka kutokana na vipesa nilivyokuwa ninavyo vya mkopo.

Mwisho mbele ya mwanasheria wa chuo nilikana na kesi yangu ikapelekwa polisi na kuwekwa mahabusu siku 4 na kisha kupandishwa kizimbani katika mahakama ya mwanzo.

Kesi hii iliniathiri sana kisaikolojia kwani hata mtaani iliniaribia sifa kwani mshitaki alikuwa akintangaza kuwa mimi ni mwizi. Iliniuma sana mpaka ikapelekea mimi kuumwa na kuharibika kwa ratiba zangu za masomo kipindi chote cha kulindima kwa kesi.
Kesi ilichukua miezi 2.5 kuisha mpaka 1.6.2018 kesi ilihukumiwa kama ifuatavyo

" mshitaki umeshindwa kuithibitishia mahakama juu ya mshitakiwa, hivyo mahakama imejiridhika kuwa mshitakiwa huna hatia yoyote, hivyo basi kuanzia sasa mshitakiwa uko huru"........hapo ndo tulitoka nje na kuondoka.

USHAURI WENU:
1.Ni vipi ninaweza kufungua mashitaka ya kuomba fidia maana huyu mtu kanifanya niishi na stress ambazo sijawahi zipata.
2. Je akikata rufaa kwa kukosa kwake ushahidi inaweza mfanya ashinde kesi? .

Naombeni ushauri kwani huyu mtu kansababishia madhara ya kiakili na ghara zisizo za lazima.
 
Duh chuo kuna mambo acha tu jamaa aliibaga laptop semister ya kwanza chuo tuko Chet kaja nayo tena diploma ya pili semister ya pili tukamdaka kipigo chake nazani kile cha mbwa koko nikidogo
 
Kamwaga mboga na wewe mwaga ugali, mburuze mahakamani akulipe fidia ili siku nyingine asiwe anakurupuka..
 
Naombeni ushauri kwani huyu mtu kansababishia madhara ya kiakili na ghara zisizo za lazima.
Kiongozi, kufuatana na kosa uliloshtakiwa nalo na mlolongo wa kesi nzima hapo dai gharama ya kesi tu. hakuna kingine unaweza kudai na ukafanikiwa kulipwa au ukashinda zaidi ya gharama uliyotumia katika kesi hiyo (kama gharama zipo).
 
Ninaomba kujua, kwani jukwaa la sheria ukipost huko ni wanasheria tuu wanaona?mfano nikirefresh siwezi kuona posti yake?
Hapana hata mtu mwingine anaweza kuona ila inakua ni rahisi Uzi wako kuonekana na wenye profesheno hiyo!

Halafu inakua kuna mpangalio mzuri kiasi kwamba Hata huko mbeleni mtu anaweza pata Tatizo kama lake Kwahiyo akanyooka jukwaa la sheria kuona wanadau walishauri nini!

Naona mamod wameshamsaidia kuhamishia jukwaa husika
 
mpeleke mahakamani mfungulie kesi nyingi nyingi
kama kukufedhehesha
gharama za kesi zirudishwe
kosa la kimtandao kama alikuwa anatumia simu kusambaza sifa mbaya
na nyingine nying angalau zifike kama kumi hivi ili aite adabu, watu kama hao nina uchungu nao.....mtie adabu siku nyingine asirudie kabisa
 
fungua kesi ya madai kwa kukuharibia reputation yako especially kuna kitu kinaitwa defamation in tort then utapata haki yako
 
Back
Top Bottom