Hatimaye Dr. Slaa amjibu Nape, aingizwa 'King'?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Nape ni kijana ambaye mara nyingi kama siyo zote huwa mropokaji na hana khoja ya tija ni mtazamo ambao ni sahihi kabisa.

Nape alipodai viongozi wengi wa cdm wana kadi za ccm na huzilipia michango ya kila mwaka kimyakimya ungelitegemea cdm aidha kumpuuzilia mbali au kumpa mojawapo ya majibu yafuatayo:-

a) ccm wamekuwa mstari wa mbele kupokea kadi za wanachama wa upinzani ambao wameamua kujiunga na ccm badala ya kuzirudisha kwenye vyama husika kama kadi tajwa zinavyoweka bayana juu umiliki wa kadi husika. Kwa hiyo ccm kutarajia viongozi wa cdm kuzirudisha kadi za ccm kwa ccm ni unafiki. ccm ionyeshe njia kwa kurudisha kadi zote tajwa za vyama vya upinzani walizokabidhiwa khalafu ndiyo ije na maswali ya kuulizia kadi zao zilizoko upinzani.

b) Kama Nape anao ushahidi wa hilo angeliripoti kwa msajili wa vyama vya siasa kwa sababu ni makosa ya jinai kuwa mwanachama wa chama cha siasa zaidi ya kimoja.

c) Nape atoe ushahidi kwa tuhuma zake juu ya malipo ya michango husika kabla hajajibiwa.

Kwa kuchelea kutoa majibu tajwa na kukiri ana kadi ya ccm na kuwa anaienzi kikamilifu, Dr. Slaa kaingizwa "kingi" na Mpayukaji Nape kwenye nyanja zifuatazo:-

i) Je Dr. Slaa anaweza kuienzi kadi ya ccm kwa kuwa mwanachama mfu au kwa kuwa mwanachama hai kwa maana ya kulipia michango husika kila mwaka?

ii) Je kwa kuienzi kadi ya ccm ambayo ni mali ya ccm huku kila nafasi ikijitokeza Dr. Slaa hupokea kadi za ccm kutoka kwa wanachama wapya wa cdm ambao wanatoka ccm haoni yeye ni mnafiki? Dr. Slaa kadi yake kumbe kaibana lakini za ccm anapokea badala ya kuwaasa nao wazienzi au hata basi kubaini masilahi ya muda mrefu aliyonayo juu ya kadi husika........... badala ya kuzipokea kadi za ccm huku yeye binafsi ana masilahi mazito ya kuienzi kadi tajwa tena kimya kimya.

iii) Kwa kukiri kadi anayo na kuwa anaienzi anaonyesha jinsi ambavyo alivyo ndumila kuwili na kutia mashaka makubwa kama yeye siyo askari mamluki ndani ya cdm ambayo ccm humtumia kuidhoofisha badala ya kuimarisha. Mfano hai ni pale ambapo alidai ana ushahidi JK kaiba kura zake na hakupaswa kutangazwa Raisi lakini hadi leo kabana kimya na huo ushahidi (Kama kweli upo au kauli ya asiyekubali kushindwa) kama siyo kula sahani moja na mahasimu wake kisiasa ni nini?

iv) Kitendo cha kuwa na kadi ya chama ambacho Dr. Slaa siyo mwanachama kinakiuka masharti yote ya kadi hiyo sasa kama haheshimu masharti husika hivi sheria zetu kweli angelizithamini kama angelishinda uraisi?

v) Upeo wa Dr. Slaa nao unatia mashaka sana kama mitazamo hii haikumpitia kichwani kwake kabla hajatoa majibu husika na kutathmini athari zake.

Kweli upinzani tz ni kulitumika tumbo; kama ilivyo ccm, na ndiyo maana Dr. Slaa kabla hajakubali kugombea uraisi alihakikisha cdm inaingia mkataba naye kumlipa sawa na mbunge nafasi ambayo hatakuwa nayo kwa miaka mitano (2010-15) na hivyo kuleta upendeleo usiyo wa lazima ndani ya waajiriwa ndani ya cdm....Kumbuka "Some animals are equal but others are more equal than others"............Orwellian principle
 
kwa hiyo CCM inamuhesabu kama ni mwanaccm,yaani ni kati ya wale milioni 5!
 
Ndiyo slaa ni active member na analipia ada zote za wamachama huko anazuga tuuu kwa ushahidi njooni mjengoni mpewe data zote.na c slaa tu lipumba,hamad,zito,mbowe wote ni wanaccm
 
pumba tupu prdsha za m4c duu mnataman mwaka uish mapema nakuambia na bado m4c with no apologic
 
Dr Slaa sasa kadi ya CCM unakaa nayo ya nini wakati wewe upo Chadema. Mbona wale wanarudisha kadi kwenye mikutano yako uambii wakae nazo kama kumbukumbu.
 
Dr Slaa sasa kadi ya CCM unakaa nayo ya nini wakati wewe upo Chadema. Mbona wale wanarudisha kadi kwenye mikutano yako uambii wakae nazo kama kumbukumbu.

acha umbumbumbu .... una gubu la chadema wewe
 
ccm1.jpg
 
Dr Slaa sasa kadi ya CCM unakaa nayo ya nini wakati wewe upo Chadema. Mbona wale wanarudisha kadi kwenye mikutano yako uambii wakae nazo kama kumbukumbu.

Maanzi kayanza, kwani kadi nini? weye mbona una vya watu vingi!
 
Hakuna uzushi hata ukikasirika lakini kaa ukijua Dr Slaa bado anayo kadi ya CCM.

Thread uzipendazo hizi ha ha ha. Jembe la CCM Online. Mkuu vipi hapa naona HUDAI USHAHIDI
 
mh!!! kweli nimeamini watu wako kwa ajili ya kuyatumikia matumbo yao na si wananchi kama wanavyohubiri,we kama kiongoz makini kadi mbili za NINI??????
 
Je Nape naye analipia kadi yake ya CCJ? Maana Nape Sitta, Mwakyembe walipovuliwa gamba na Mpendazoe kuwa walianzisha chama cha Jamii (CCJ) hadi kesho hawajawahi kutoa majibu yanayoingia akilini.
 
Thread uzipendazo hizi ha ha ha. Jembe la CCM Online. Mkuu vipi hapa naona HUDAI USHAHIDI

Mtoto wa kiume unapenda sana kucheka...mie nachangia thread nyingi na majukwaa mengi nipo...naona mzimu wa Ritz, unazidi kukutafuna na bado.
 
Last edited by a moderator:
Pro-Chadema ebu kuweni mfano wa Dr Slaa kadi zenu za CCM zitunzeni.
 
Mwanangu Yericko Nyerere punguza hasira hadi unaongea kichina. Umewahi kusoma kitabu cha Tzu te ching? Kitafute utafaidika sana.
 
Back
Top Bottom