Hatimaye Dkt. Mwaikali akabidhi mali za Kanisa la KKKT

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
1,191
3,028
Hatimaye aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde Usharika wa Ruanda, Dk Edward Mwaikali amekabidhi ofisi na mali, yakiwamo magari 10 kwa askofu mpya, Geofrey Mwakihaba.

Makabidhiano hayo yalifanyika juzi katika usharika wa Ruanda, chini ya uangalizi wa askari polisi wakiongozwa na Ofisa Operesheni, Johanes Bitegeko na waumini wa kanisa hilo.

Kukabidhiana mali kunahitimisha mvutano uliokuwapo kwenye Dayosisi hiyo ambao ulichagizwa zaidi baada ya Dk Mwaikali kuvuliwa uaskofu na Mkutano Mkuu wa Dayosisi ya Konde uliofanyika Machi 22, mwaka huu.

KUKABIDHI
Mara baada ya Dk Mwaikali kukabidhi mali za Dayosisi hiyo, alizungumza kwa ufupi kuwa tayari amekabidhi mali zilizotakiwa, lakini akaahidi kuzungumza kwa mapana juu ya jambo hilo atakaposhauriana na mwanasheria wake.

“Niongee nini, nimeshakabidhi, nimeshauriana na mwanasheria wangu naomba mnipe muda zaidi, naamini Juni 22 tutakapokuwa tunakabidhi kila kitu ndipo nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza,” alisema Dk Mwaikali.

KAULI
Kwa upande wake Askofu Mwakihaba alisema majukumu yake makubwa ni kurudisha mali Makao Makuu Tukuyu na hatua hiyo ni utekelezaji wa shughuli zake, lakini akiweka wazi kuwa ni maandalizi ya makabidhiano rasmi yatakayofanyika Juni 22, mwaka huu.

Alisema kuwa waliamua pia kufanya haraka kufuatia matamko kadhaa ya kuhamisha kanisa, huku akimshukuru Dk Mwaikali kwa kukubali kuachia mali na kwamba, iwapo ameamua kutoka moyoni itakuwa bora sana.

IBADA
Askofu huyo aliyesimikwa Juni 5, aliongeza kuwa Jumapili ya wiki hii anatamani kuendesha ibada kwenye Kanisa la Ruanda alipokuwa Dk Mwaikali na kwamba kama hatakuja yeye, basi atakuja mwingine kama yeye.

Naye Askofu mstaafu katika kanisa hilo aliyempisha Dk Mwaikali, Dk Israel Peter alisema wanashukuru zoezi kwenda vizuri tangu mwanzo kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali na vyombo vya dola na kwamba, hadi sasa mgogoro umeisha.

Askofu huyo aliyehudumu kwa miaka 16, alisema kuwa mgogoro huo umewafundisha mengi, ikiwamo kumchunguza na kumuandaa mtu kabla ya kumpa majukumu kuanzia hatua za chini.

“Zoezi lililobaki tumemuachia aliyekuwa Katibu wa Kanisa kuainisha mali zote zilizopo kisha kukabidhiwa Juni 22,” alisema.

Baadhi ya waumini waliojitokeza kwenye tukio hilo la makabidhiano, Joseph Mwajanga na Amina Haule walisema hatua hiyo imeonesha ukomavu wa pande zote na sasa amani irejee hapa kanisani kwa kuwa wanamtumikia Mungu.

“Hizi tofauti ziishe, japokuwa huenda kuna upande umeumia kwa yaliyotokea ila tuungane kwa pamoja katika kuendeleza dini yetu, haya tuyasahau tuanze upya wote tunamtumikia Mungu mmoja,” alisema Mwajanga.
 

mkupuo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,648
1,463
Ukiona serikali (Kaizari) inaingizwa ktk uendeshaji wa dini yoyote, jua hakuna dini hapo. Iweje polisi wawepo kwenye makabidhiano badala ya kukabidhiana wenyewe kwa wenyewe kiroho safi?
 

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,882
4,383
Dhambi tunazo za kutosha,, ila kwa hili sakata hawa watu wameonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu!!

Hawa ndiyo wale Bwana Yesu aliwasema siku hiyo atawakataa!!
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom