Hatimaye CCM yatimiza ahadi; Bajaji za Wagonjwa zapokelewa rasmi

Hiii thread ni uongo hapo ni dr mponda na dr mtasiwa ambao hawako tena wizara ya afya..ungesema from our files.....!!
 
Huyu JK na serikali yake ni upuuzi mtupu. Yeye anajitembeza angani kila siku kwenda kukokotwa majuu. Wamama na watoto wetu ndiyo wa kudanganyia bajaji. Too late!
 
hayo ndiyo mawazo mgando ambayo yanatoa na kuendeleza ukandamizaji kwa wananchi kweli bajaji kwa kina mama?huu ni uthalilishaji labda apande kwanza mama salma
 
Yaani hamuoni aibu??? Hamna dhamira ya dhati ya kumkomboa mwanamke ndio maana mkaona bajaji ni size yao. Hamkufikiria barabara na miundombinu ya Tz ilivyo, hamkufikiria upepo, jua na mvua kwa mama mjamzito.

Ufisadi mtupu! Mnachojali 10% zenu ktk mradi huo! Tena afadhali hata design ya mwanzo aliyoibuni Prof. Mwakyusa alipokuwa Waziri wa Afya, bajaji hizo zilikuwa more spacious ambapo nesi, vifaa vya huduma vilikuwa na nafasi. Lakini alipokuja fisadi mama Blandina Nyoni alikwenda mwenyewe kufanya mazungumzo na kampuni hizo na kubadilisha design baada ya kukatiwa kitu kidogo. Matokeo yake ndio huto tubajaji twenu. Dhambi hiyo iwe juu yenu na vizazi vyenu!
 
WEKA PICHA BASI TUONE HIYO BAJAJ INAFANANAJE, ISIJEKUWA NI KUBWA KULIKO JEEP! nIMEFUATA HADI UKURASA WA NANE SIONI BAJAJ-AMBULANCE
 
mmh!dola 6000 kwa hicho kipikipiki kimoja,nanusa harufu ya ufisadi au ndo mambo ya zabuni??bajaji 400 si zinaishia mbagala tu,kuna wanawake wangapi wanapata ujauzito..wao wanatembelea mavx
$6000 is too much kwa hicho kipikipiki. hapo cha juu kinaweza kuwa zaidi ya mara tatu ya bei halali.
 
ni 4WD? Au zitafanya kazi kiangazi tu tena sehem zisizo na vumbi/mchanga mwingi.
Haziwezi kuwa 4WD kwa sababu zina matairi matatu. most likely zitakuwa 2WD, na hatujui pengine zikawa zinatumia mnyororo kati ya hayo matairi ya nyuma. hazina nafasi ya kutosha kwa muhudumu na zitakabiliwa na hivyo vikwazo ulivyovisema hapo juu pengine na zaidi. nadhani hazitamudu, anyway acha wa-test tuone matokeo yake.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe. Tanzania si mara ya kwanza hizi pikipiki kutumika kama alternative ambulances. Kuna special coverage niliona CNN jinsi zilivvyoweza kupunguza vifo vya kina mama wajawazito Southern Sudan.

Read more about them here from an old UK guardian article Could motorbikes cut deaths in childbirth in Africa? | Katine | guardian.co.uk

tatizo ni bei walionunulia. wangeweza kupata better deal than that.
Anyway wanasemaga mali ya umma hailiwi bila mradi, hicho ndicho walichokifanya hapo. Cha juu kikuuubwa.
 
Balance yake ikoje? Mgonjwa anakingwaje wakati wa hali ya mvua? Ajali za pikipiki zimeongezeka sana nchini, waendeshaji wa pikipiki hizi wamepata mafunzo gani?

Balance yake hovyo kabisa, taarifa kutoka huko vijijini zinasema wakati wa kuziendeshsha ni shida sana kukata kona kwenda kushoto (upande wa kitoroli/machela). Ziada ni kuwa yasemekana Ujenzi wamezinyima kibali cha kupata plate number kwa hiyo kuna sakata. Natumaini walioko huko mikoani na wilayani watachangia zaidi kuhusu hizi motorcycle ambulances.
 
hizo bajaji tuliambiwa kila moja ilinunuliwa $8,500 sasa bei yako imetoka wapi

tuma picha hapa tujadili kwani tulioziona hizo bajaji katika wailaya nyingi wameshindwa kuzitumia na wamezitelekeza hazina mwenyewe. kwanini rushwa imekupofusha na kuleta ushabiki badla ya kusema kweli

Mleta mada kajichanganya, bei ni US $ 8,500 kila moja, siyo hiyo bei anayotuambia mtoa mada. Rejea item 28 katika thread zza awali za JF: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/221725-ufisadi-wa-blandina-nyoni-huu-hapa.html,
 
Mbona zimekwisha sambazwa mawilayani lakini hadi leo wilaya nyingi wameshindwa kuzitumia kutokana na muundo wake na jinsi ya kuzitumia kwani zitampa wakati mgumu sana mwendeshaji ambaye nadhani ni mganga wa kituo cha kutolea huduma.

ha ha ha so project failed
 
mgonjwa hadi anafika hospital si atakuwa ameshafariki na upepo na vumbi
 
Mpango wa Serikali iliyouanzisha wa ununuzi wa Pikipiki za kubebea wagonjwa ili kuzuia vifo vya wakinamama na watoto katika maeneo ya vijijini. Serikali inakusdia kununua Pikipiki 400 ambazo zitasambazwa maeneo mbalimbali hapa nchini.

Pikipiki maalum iliyotengezwa na Kampuni ya E Ranger ya Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kubebea wagonjwa ili kudhibiti vifo vya mama na watoto. Pikipiki hizo kila moja imegharimu Dola za Kimarekani 5,900.

Si vibaya kwa serikali kutekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wananchi. Badilisha heading hapo juu, ni kodi za watanzania siyo hela za ccm.
Huo ni ufisadi wa hali ya juu sana kwa bajaji kugharimu Tsh.9,440,000, wakati bei ya halali ya bajaji ni kati ya Tsh.3,600,000 mpaka Tsh. 4,000,000
 
Sio Bajaji ni pikipiki zilizoundwa katika muundo wa kubuni baada ya jamaa kuota ndoto, Tafakali ndugu matumizi yake Barabara za vijijini ni nyembamba kuna visiki, Nyoka, baadhi kuna wanyama wakali je mama mjamzito atafika salama? Je na muundo wa pikipiki hizo ni rafiki kwa mtumiaji?
View attachment 67667
 
tatizo ni bei walionunulia. wangeweza kupata better deal than that.
Anyway wanasemaga mali ya umma hailiwi bila mradi, hicho ndicho walichokifanya hapo. Cha juu kikuuubwa.
Vyote ni tatizo Bei pia matumizi yake ni magumu kwa hiyo kwa kauli halisi hazitaweza kutumika kutokana na muundo wake ambao sijawahi ona duniani na kama zikifanikiwa kutumika tutaziingiza kwenye maajabu saba ya duniani
 
Mpango wa Serikali iliyouanzisha wa ununuzi wa Pikipiki za kubebea wagonjwa ili kuzuia vifo vya wakinamama na watoto katika maeneo ya vijijini. Serikali inakusdia kununua Pikipiki 400 ambazo zitasambazwa maeneo mbalimbali hapa nchini.

Pikipiki maalum iliyotengezwa na Kampuni ya E Ranger ya Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kubebea wagonjwa ili kudhibiti vifo vya mama na watoto. Pikipiki hizo kila moja imegharimu Dola za Kimarekani 5,900.

Hebu tutoleeni u****a wenu hapa, bajaj kwa dola 6000/=? Kha.... Harufu kali ya ufisadi!
 
Si vibaya kwa serikali kutekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wananchi. Badilisha heading hapo juu, ni kodi za watanzania siyo hela za ccm.
Huo ni ufisadi wa hali ya juu sana kwa bajaji kugharimu Tsh.9,440,000, wakati bei ya halali ya bajaji ni kati ya Tsh.3,600,000 mpaka Tsh. 4,000,000

Ni dengu hizo $$ Ukilinganisha na wanazobakiza kuzila na kuziwekesha Benki Nchi za Nje ni hatari... Wewe Unanunua BAJAJ; Unajua zinatoka wapi mmmm INDIA mabingwa wa kuhonga na utapeli... kwahiyo toka kiwandani ni wizi MPAKA kufika kijijini ni WIZI... kwanini Wasiende JAPAN ? Mbona Nyerere Alikuwa analeta Matreta ya MASSEY FERGUSON na JOHN DEERS angalia vijijini kote utayaona hayo Matreta hata wazee wanayajua; NDEGE nyerere alikwenda kununua BOEING alirline huko SEATTLE; MELI MV BUKOBA aliileta toka NORWAY hakuwa na second class stuff...
 
Back
Top Bottom