Hii kitu imenidisturb sana kusema ukweli.
Hii gari ni $3,400, $2,000 chini ya hizo mochuari on wheels!! Huu ni upuuzi wa hali ya juu!!
Hii ambulance ni $6,500 just $600 more.
Mitsubishi DELICA SPACE GEAR CHAMONIX 4WD - Japan Partner
1990 NISSAN CARAVAN AMBULANCE Japanese used cars on sale , Import from Japan at Autorec Enterprise,LTD
Ahadi za Kikwete (CCM)
1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua albino- Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21.Kulinda Muungano kwa nguvu zote-Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
28.Kununua "bajaji" 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za Sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
36.Kulinda haki za walemavu- Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa mpaka Singida-Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
44.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
45.Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
46.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
47.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
48.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
49.Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
50.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
51.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
52.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
53.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
54.Kutokomeza malaria 2015-Bunda, Mkoa wa Mara
55.Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo, Iringa
56.ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
57.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
58.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
59.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
60.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbamba-bay Ruvuma
61.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) –Ruvuma
62.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
63.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
64.Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
65.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
66.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
67.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
Ahadi namba 28 aliyoitoa iringa imeenza kutekelezwa, hebu tutizame na hizo nyingine utekelezaji wake ukoje?
AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...
- Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
- Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
- Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
- Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
- Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
- Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
- Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
- Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
- Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
- Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
- Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
- Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
- Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
- Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
- Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
- Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
- Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
- Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
- Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
- Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
- Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
- Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
- Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
- Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
- Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
- Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
- Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
- Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
- Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
- Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
- Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
- Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
- Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
- Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
- Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
- Kulinda haki za walemavu - Makete
- Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
- Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
- Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
- Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
- Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
- Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
- Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
- Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
- Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
- Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
- Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
- Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
- Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
- Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
- Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
- Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
- Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
- Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
- Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
- Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
- Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
- Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
- Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
- Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
- Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
- Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
- kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
- Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
- Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
- Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
- Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
- Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
- Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
---2005 Alikuja na Maisha bora kwa kila Mtanzania,hili halina ubishi lilikuwa ni changa la macho kwa Watanzania,Kama haitoshi akasema anawajua kwa majina wala rushwa,lakini hatuoni hata mmoja aliyemchukulia hatua===hii ni kutaka sifa na popularity.
---Juzi amekuja na mpya ya kumpatia kila mwanafunzi Computer ambayo iko connected kwa internet, it's high time now kwa watanzania kuhoji uwezo wa RAIS wetu,ni kwamba anafanya Wa Tanzania ni wapumbavu sana kiasi kwamba hawawezi ku reason kuwa hilo sual haliwezekani???
Hata kwa wanafunzi tu wa vyuo vikuu hilo suala halitekelezeki leo anatuambia ataanza na shule za msingi,umeme ni tatizo..hivi jk anajua kuwa its only 10% ya wa Tanzania wana access na umeme na 0.05% ya watanzania ndo wanaweza kutuima computer na wana access na internet,hata kwa nchi ambazo zimeendelea kuzidi sisi hilo suala halipo,,yeye anataka kuhadaa Wa Tanzania aili aendelee kubaki madarakani!!!!!me nadhani pia JK na uwezo mdogo sana wa ku reason ndo maana hata hafikirii kuwa suala kama hilo watu wenye akili timamu hawawezi kusadiki,inahitaji mtu mwenye akili za mwenda wazimu kuamini ahadi kama hizo.
Mnajiropokea tu, nendeni Vijijini Mkaone Hali halisi Wajawazito wanavyotembea kwa Miguu na Wengine wanajifungulia njiani, chini ya miti nk Wakielekea Vituo vya Afya kilomita kadhaa kutoka Zahanati za Vijiji. Wenye Uwezo huko Vijijini hukodi Magari, wasio na Uwezo wanabeba wajawazito kwa Machela za kienyeji na Baiskeli za Kawaida hadi Wengine wanafia njiani. Waliobuni na Kuzitengeneza Pikipiki hizi wana Akili na Huruma zaidi ya hawa waliojiingiza kwenye Msafara wa "Great Thinkers" wakati kazi Yao ni Kuponda kila Jitihada zinazofanywa na Serikali za kuAlleviate matatizo ya Vijijini. Basi waambieni ndugu zenu Walioko vijijini kwenu wasio na Usafiri Wasizipande waendelee kutembea kwa Miguu! sie Wanyonge zitatufaa sana, KWENDENIZENUNI!!
Nasubiri viongozi wa UVCCM wajitokeze kuja kutoa pongezi!