Piki piki za kubebea wagonjwa zimeanza kuwasili toka SA. Hili wakati JK akisema wakati wa kampeni nilidhani :blah: za siasa tu, kumbe amepania...hii ni hatari kwa wagonjwa:confused3:
Mpango wa Serikali iliyouanzisha wa ununuzi wa Pikipiki za kubebea wagonjwa ili kuzuia vifo vya wakinamama na watoto katika maeneo ya vijijini. Serikali inakusdia kununua Pikipiki 400 ambazo zitasambazwa maeneo mbalimbali hapa nchini.
Pikipiki maalum iliyotengezwa na Kampuni ya E Ranger ya Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kubebea wagonjwa ili kudhibiti vifo vya mama na watoto. Pikipiki hizo kila moja imegharimu Dola za Kimarekani 5,900.
Kweli kabisa waone matokeo ya kupigia makofi vitu visivyo na maana tena nashauri moja iwe kwenye misafara ya Spika na Kikwete.Duh! Moja ipelekwe ukumbi wa bunge. Waziri au mbunge akipata dharura ya kimatibabu apakizwe kwenye hicho kitanda cha bajaj, tena naomba Mungu kiwe kipindi cha masika au vumbi kali.
ehh!! ilisiku akizimia itumike au kashaenda kwa Babu Loliondo....Kweli kabisa waone matokeo ya kupigia makofi vitu visivyo na maana tena nashauri moja iwe kwenye misafara ya Spika na Kikwete.
uko sawa kabisa mkuu...Nakumbuka wakati wa kombe la mataifa Afica lilipofanyika naijeria kama sikosei hivi vibajaji vilitumika.
Mpango wa Serikali iliyouanzisha wa ununuzi wa Pikipiki za kubebea wagonjwa ili kuzuia vifo vya wakinamama na watoto katika maeneo ya vijijini. Serikali inakusdia kununua Pikipiki 400 ambazo zitasambazwa maeneo mbalimbali hapa nchini.
Pikipiki maalum iliyotengezwa na Kampuni ya E Ranger ya Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kubebea wagonjwa ili kudhibiti vifo vya mama na watoto. Pikipiki hizo kila moja imegharimu Dola za Kimarekani 5,900.
Gari la wagonjwa linakuwa na vifaa vya utabibu pamoja na paramedic ambaye anaanza kutoa huduma ya kwanza kabla mgonjwa hajafika hospitali. Atafanyaje katika hiyon pikipiki? Ujinga kweli huo. watu wanaongea karne ya 20 sis bado tunajivunia kuingia karne ya 17. Nyeye alifundisha kuwa We Must run while they walk. Sisi badala yake tunasimama kabisa wakati wenzetu wanakimbia.