Hatimaye CCM yatimiza ahadi; Bajaji za Wagonjwa zapokelewa rasmi

mmmh? kuna usalama hapa? sasa si unaweza kumuua mgonjwa kabisa hapa kabla hajafika hospitali? ivi wat about remote areas zinafika kweli? kuna takwimu/reviews zozote juu ya pikipiki hizi mahali zilipotumika na ubora wake? naona ka janja ya watu hapa, pikipiki 400 vs mil 90 mkopo wa wabunge....
 
hiviiiiiii hapo mgonjwa anatundikiwaje drip? what if yupo mahututi na anahitaji msaada wa haraka kwenye hizo "ambulance" kuokoa maisha yake? inakuwaje hapo?
what if mama ana kifafa cha mimba au complication yoyote ya mimba au baada ya kujifungua?..... huu ni utani.........
 
Hivi hizi pikipiki zitapita katika barabara zipi huku kwetu KAVIFUTI?? Labda ni za hukohuko Dar.......
 
Gazeti la mwananchi leo limemnukuu waziri wa afya akidai serikali imenunu bajaji kwa dola 5900 sawa na shilingi milioni 9 za tanzania! Bajaji sasa inauzwa shilingi milioni 4 hivyo shilingi millioni 5 kila bajaji au billion 2 kwa bajaji 400 zimekwapuliwa na wajanja!
 
mmh kazi tunayo..sijajua zimeagizwa kutoka wapi bt kwa huku india bei ya autorickshaw with a four-stroke compressed natural gas (CNG) engine ikiwa imelipiwa tax na insurance inarange kati Rupees 70000-hadi 85000..sasa inategemea na unanunua kwenye state gani na kama utachukua nyingi bei inashuka...so hiyo hela ni sawa na mil 2-hadi mil 2.5 za kibongo...!!!sasa hata kama utajumlisha gharama za usafirishaji sidhani kama zitafikia mili 9...anyway
 
Mimi kinachonishangaza ni kuwa watu wanashangaa ahadi ya CCM imetekelezwa to the letter; CCM na mgombea wake hawakuwaahidi Suzuki Vitara au hata Tata; hawakuawaahidi magari ya wagonjwa katika kila tarafa. Waliwaahidi vibajaji 400. Na watu walishangalia na kwenda kupiga kura kuwachagua wakijua kabisa wataletewa vibajaji. Tuliohoji hilo na kukebea tulionekana ni "wapinzani".

Sasa ahadi imetimizwa watu wanaanza kung'aka! Sielewi kwanini.

Wana CCM wawe wa kwanza kufurahia na binafsi ningependekeza vipikipiki hivi vitumike kuwabeba wapiga kura wana CCM kwenda mahospitalini kwani nina uhakika ifikapo 2015 tutakuwa na wapiga kura wachache zaidi kutoka CCM. Msiniulize kwanini.

Kigumu chama cha mapinduzi!!! na wote waitikieee KIGUMUUUUUU!
Hongera JK kwa kutimiza ahadi to the dot!
 
Hizi Pikipiki ni majeneza :
1. Ikipata ajali mathalani kupinduka na kuungua moto, mgonjwa aliyefungiwa humo atapona?

2. Mvua ikinyesha mgonjwa si atakufa kwa kuzama?

3. Mama mjamzito atalala vipi chali humo?

4. Barabara za vichochoro za vijijini zitapitika au ndio zitatumika mijini tu?
5.Kama zitatumika mijini vipi usalama wa barabara zetu?
 
Gazeti la mwananchi leo limemnukuu waziri wa afya akidai serikali imenunu bajaji kwa dola 5900 sawa na shilingi milioni 9 za tanzania! Bajaji sasa inauzwa shilingi milioni 4 hivyo shilingi millioni 5 kila bajaji au billion 2 kwa bajaji 400 zimekwapuliwa na wajanja!

Sina uhakika sana kama kuna ufisadi but looking on what others did inaonekana kuna mafanikio kwenye hili la motorcycle ambulance kwa kanzia tunaweza kutoa benefit of doubt....Lakini angalizo ni kuwa haitoshi tu kuwa na hizi bajaj lazima kuwe na improvement kwenye uadilifu wa wafanyakazi wa healthcare, upatikanaji wa dawa na watalaamu vilevile huko vijijini kwenye dispensary na vituo vya afya.

View attachment AMDD_20August_202008_202nd_20part.pdf

Could motorbikes cut deaths in childbirth in Africa? | Katine | guardian.co.uk

IRIN Africa | SUDAN: Biking for safer childbirth | Sudan | Children | Gender Issues | Health & Nutrition

nawashukuru sana wakatoliki kwa sababu toka miaka ya 70 kuna ambulance kijijini kwetu na hospitali ya mission.. Kwa hawa watakaopanda vibajaji basi nawaombea kila la kheri. But i can see ccm wanajichimbia kaburi.. Sasa mbona wamepiga picha pikipiki mbili au moja sijui..hizo ndio 400? Or thts politics
 
Huu ni mradi wa mtu nawaambia.....shame on our leaders,more shame on us tunaonyamaza na kukodolea majicho tu bila kusema kufanya lolote......simple mathematics hela hiyo ya kununulia hizo pikipiki si wangeaza hata na ambulance 150 au 100 tu.....hii si dhihaka kwa wamama wajawazito hivi serikali yetu imeundwa na wanaume tu,hakuna hata mwanamke mmoja aliye pata kuwaambia jinsi uchungu unavouma na mazingira ya kipikipiki hicho??Bora tuendelee kutembea na mguu tukifika mahali vimetuzidi tunakaa chini na kupumzika.....hivi mshauri wa muheshimiwa ana akilifupi kiasi hiki akashindwa hata kutazama kwa macho uwiano wa barabara na vijipikipiki vyao??si ajabu ni msaaba si tunaambiwa zimenunuliwa.....mmh inauma!!!!!
 
pikipiki ya dola 5900 ??hivi hizo pesa zinashindwa kununua gari ndogo na ikaweza kubeba wagonjwa jamani??
mbona naona ni kama matumizi mabaya tu pesa??
5900==6000 usd ni pesa nyingi sana jamani kwa hizo bajaji.
Noo nooo I stand to be corrected.
 
Haingi akilini kununua pikipiki kwa dola 6000 na ongeza gharama za usafiri,kwanini wasinunue ambulance zilizotumika kwa nusu wa hiyo bei ? nimeziona Dubai,Japan na Singapore,hapa akili haijatumika kabisa kwenye barabara za lami zinaweza tumika lakini vijijini na barabara mbovu mjamzito au mgonjwa mahututi ni kuwaumiza tu.

Huu udwanzi sasa jk ameanza
 
nimekusoma magee ,sio siri hayo ni matusi tena ya nguoni kabisa.
kwani gari ndogo gaharama ni kiasi gani basi,mbona kwa hiyo pesa wangeongezea kidogo tu..
yaani Tanzania ni kazi bure kabisa...
im so sad
Huu ni mradi wa mtu nawaambia.....shame on our leaders,more shame on us tunaonyamaza na kukodolea majicho tu bila kusema kufanya lolote......simple mathematics hela hiyo ya kununulia hizo pikipiki si wangeaza hata na ambulance 150 au 100 tu.....hii si dhihaka kwa wamama wajawazito hivi serikali yetu imeundwa na wanaume tu,hakuna hata mwanamke mmoja aliye pata kuwaambia jinsi uchungu unavouma na mazingira ya kipikipiki hicho??Bora tuendelee kutembea na mguu tukifika mahali vimetuzidi tunakaa chini na kupumzika.....hivi mshauri wa muheshimiwa ana akilifupi kiasi hiki akashindwa hata kutazama kwa macho uwiano wa barabara na vijipikipiki vyao??si ajabu ni msaaba si tunaambiwa zimenunuliwa.....mmh inauma!!!!!
 
Hizi Pikipiki ni majeneza :
1. Ikipata ajali mathalani kupinduka na kuungua moto, mgonjwa aliyefungiwa humo atapona?

2. Mvua ikinyesha mgonjwa si atakufa kwa kuzama?

3. Mama mjamzito atalala vipi chali humo?

4. Barabara za vichochoro za vijijini zitapitika au ndio zitatumika mijini tu?
5.Kama zitatumika mijini vipi usalama wa barabara zetu?

wala usiongee sana, bora unyamaze tu.
sasa ataka kucha kusikia siasa kabisa maana naona nitapata pressure zaidi.
 
Duh! Moja ipelekwe ukumbi wa bunge. Waziri au mbunge akipata dharura ya kimatibabu apakizwe kwenye hicho kitanda cha bajaj, tena naomba Mungu kiwe kipindi cha masika au vumbi kali.
 
hv maranyingi mpk mtu apandishe kwenye gari la wagonjwa si anakua mahututi kwaiyo anahitaji uangalizi,sasa kwa hapo sioni sehemu ya kuwweka hata drip au kumuweka nesi sizan kama hiki litapunguza vifo watakufa tu mana na brbr zetu zilivyo mbovu hawa wagonjwa watachelewa kufika hspt na kwa sbb hakuna nesi pembeni watakufa tu,

ndo mana watz hatuendelei yan maswali mazito tunatoa majibu mepesi hv kweli mtu anafikili eti kununua hizo pikipiki ndo vifo vya kina mama vitaisha??????????????????????????ama kweli sisi hamnazo kbs
 
Back
Top Bottom