barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,323
- 29,584
I
Inafutika lindi na mtwara inaenda ibuka arusha, mbeya na Kilimanjaro!Kufuatia kushindwa kwa Serikali ya CCM kushikwa na kigugumizi cha kuwaamuru wanunuzi woote wa korosho kutekeleza utaratibu wa kusafirisha korosho msimu huu wa 2020/2021.
Kabla ya kuingia kwa awamu ya tano madarakani, serikali zilizopita zilikuwa na utaratibu wa kuhakikisha kuwa korosho inayozalishwa mkoa wa Mtwara na Lindi zinasafirishwa nje kwa kupitia bandari ya Mtwara.
Hii iliwasaidia wakazi wa Mtwara hasa wachukuzi, kina mama nitilie, wenye ma hotel, Guest house, ma baa, maduka, bodaboda, tax, wenye maghala, wenye majumba kujipatia kipato kutokana na kuwapangisha wanunuzi bidhaa zao.
Leo hii Serikali ya CCM inawaacha wana mtwara na njaaa huku wakiona mazao yao yakipita kwenda bandari ya Dsm.
Wana Mtwara na Lindi hiki ni kipindi chetu kuionyesha CCM kuwa wamechoshea na maonevu ya CCM kwa kuikataa kwenye uchaguzi wa mwaka huu.