Hatimaye CCM walitwaa Jimbo la Nassari, John Pallangyo apita bila kupigwa

John Pallagyo aliyekuwa anagombania Ubunge katika Jimbo hilo kupitia CCM amepita bila kupingwa baada ya Wagombea wenzake 10 kukosa sifa, Msimamizi wa Uchaguzi, Emmanuel Mkongo ametangaza

Jimbo la Arumeru Mashariki lilitangazwa kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADAMA, Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge kwa kutokuhudhuria Mikutano mitatu ya Bunge

Nassari baada ya kuvuliwa Ubunge alifanya taratibu za kwenda Mahakamani na kufungua shauri la kuomba kufungua kesi ya msingi ya kumtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kutengua uamuzi wake lakini jitihada zake ziligonga mwamba
======

Arumeru. Mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pallagyo amepita bila kupigwa katika nafasi hiyo baada ya wagombea wenzake 10 kushindwa kukidhi vigezo.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Emmanuel Mkongo amesema hayo Leo Ijumaa Aprili 19, 2019 wakati akitangaza matokeo baada ya upitiaji wa fomu zilizowasilishwa .

Mkongo amesema jumla ya wagombea 11 walichukua fomu na kati yao, watatu hawakurudisha na saba fomu zao zimebainika kutokidhi vigezo.

Amesema wapo ambao hawajalipa fedha ya dhamana ya kugombea ubunge ya Sh50,000, kukosa wadhamini na kurejesha fomu ya kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Akizungumza baada ya mkurugenzi kumtangaza kuwa kapita bila kupingwa, pallagyo, amekishukuru chama chake kwa kumuamini na amesema atahakikisha anafuata nyayo za Rais John Magufuli katika utendaji kazi.

“Pia nitamkumbusha Rais ahadi yake aliyoitoa ya ujenzi wa barabara ya kilometa tano za lami jimboni humo na nitahakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano ndani ya muda mfupi,” amesema.

Naye Mmoja wa wagombea kutoka chama cha Demokrasia Makini, Saimon Ngilisho ameunga mkono uamuzi huo huku akikiri kukosa wadhamini kutokana na wananchi kukatishwa tamaa na wapinzani kujiuzulu kabla ya muda wao kufika, hivyo kusababisha kukosa sifa za kugombea.
Barabara sasa itajengwa maadamu mbunge ni wa ccm
 
Tunampongeza kwa ushindi huu Kijana aliwadharau sana wana Arumeru haiwezekani hata mimba walienda kujaziana marekani akala bata miezi 9 wana Arumeru wamfurahie tena hadi sasa hajawaomba msamaha kwa Kitendo cha Kihuni alichokifanya kwa wana Arumeru.

Sijawahi kuona Mbunge anafukuzwa kwa Utoro.
Ona hili stomach defender linavyoongea kama muuza birian
 
Mi nife wapi mzee pesa zinazidi kuongezeka Familia inazidi Kuongezeka magari na Nyumba vinazidi kuongezeka investment zina hali nzuri sana yaani ni raha sana kama huishi kwa Ujanja ujanja hapa Tanzania.
Mtu ajisifu ila husifiwa
 
Mi nife wapi mzee pesa zinazidi kuongezeka Familia inazidi Kuongezeka magari na Nyumba vinazidi kuongezeka investment zina hali nzuri sana yaani ni raha sana kama huishi kwa Ujanja ujanja hapa Tanzania.
pole Mzee wa misifa
 
Huyu John Palagyo si yule anayetuhumiwa kwa ufisadi kwa kupitia kampuni yake ya bima? CCM bana ... time will tell
 
[/QUOT

Mwanza alikuaga na Branch akamuweka mdada flan mashallah asee vijana tulikuwa tunapokezana tu
 
John Pallagyo aliyekuwa anagombania Ubunge katika Jimbo hilo kupitia CCM amepita bila kupingwa baada ya Wagombea wenzake 10 kukosa sifa, Msimamizi wa Uchaguzi, Emmanuel Mkongo ametangaza

Jimbo la Arumeru Mashariki lilitangazwa kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADAMA, Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge kwa kutokuhudhuria Mikutano mitatu ya Bunge

Nassari baada ya kuvuliwa Ubunge alifanya taratibu za kwenda Mahakamani na kufungua shauri la kuomba kufungua kesi ya msingi ya kumtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kutengua uamuzi wake lakini jitihada zake ziligonga mwamba
======

Arumeru. Mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pallagyo amepita bila kupigwa katika nafasi hiyo baada ya wagombea wenzake 10 kushindwa kukidhi vigezo.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Emmanuel Mkongo amesema hayo Leo Ijumaa Aprili 19, 2019 wakati akitangaza matokeo baada ya upitiaji wa fomu zilizowasilishwa .

Mkongo amesema jumla ya wagombea 11 walichukua fomu na kati yao, watatu hawakurudisha na saba fomu zao zimebainika kutokidhi vigezo.

Amesema wapo ambao hawajalipa fedha ya dhamana ya kugombea ubunge ya Sh50,000, kukosa wadhamini na kurejesha fomu ya kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Akizungumza baada ya mkurugenzi kumtangaza kuwa kapita bila kupingwa, pallagyo, amekishukuru chama chake kwa kumuamini na amesema atahakikisha anafuata nyayo za Rais John Magufuli katika utendaji kazi.

“Pia nitamkumbusha Rais ahadi yake aliyoitoa ya ujenzi wa barabara ya kilometa tano za lami jimboni humo na nitahakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano ndani ya muda mfupi,” amesema.

Naye Mmoja wa wagombea kutoka chama cha Demokrasia Makini, Saimon Ngilisho ameunga mkono uamuzi huo huku akikiri kukosa wadhamini kutokana na wananchi kukatishwa tamaa na wapinzani kujiuzulu kabla ya muda wao kufika, hivyo kusababisha kukosa sifa za kugombea.
 
Ila yeye mwendawazimu, mwizi, fisadi, mtenda maovu mbali mbali nchini ndiye mwenye sifa za kugombea!

Another evidence of a FAILED STATE.
Yaliyopo na yajayo yanasikitisha na kufikirisha. Tunaelekea nchi ya kufikirika. Tujikumbushe kitabu cha Tambueni Haki zetu.
 
Duu mnaoba lijamaa hamlijui maana halijafanya kampen linawambia me ndo mbunge wenu waTz tumekua wajinga sana
 
Jamaa ni kama ameenda akawaambia wana Arumeru "Mimi ndiye mbunge wenu" Full ubakaji wa live!
 
Haya ni maandalizi tu, 2020 utasikia Magufuli amepita bila kupingwa baada ya wagombea wote wa upinzani kukosa sifa.
Tunailaumu ccm tu bure, hawa jamaa was upinzani mkiwachagua kabla hata mda wao haujaisha utawasikia wanaamia ccm ati kuunga juhudi, huu uKm*** sana,

I better not vite in 2020 kwa sababu baada ya mda wataamia ccm
 
Back
Top Bottom