Hatimaye Burundi kuchagua Rais mpya leo, Mei 20 baada ya Nkurunziza kuongoza kwa miaka 15

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
HATIMAYE Uchaguzi Mkuu wa Burundi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na jumuiya ya kimataifa, utafanyika kesho, huku ukielezwa kuwa ni mwanzo mpya wa demokrasia katika nchi hiyo iliyokubwa na changamoto mbalimbali za kukosekana utulivu wa kisiasa na kijamii.

Wakati uchaguzi huo ukifanyika, wachambuzi wa masuala ya siasa, kijamii na kidiplomasia, wameshauri serikali mpya itakayochaguliwa kuandaa mjadala mpana wa kitaifa utakaowezesha kubaini matatizo na changamoto za wananchi ili kuzifanyia kazi, pamoja na kuunda tume ya maridhiano itakayoshirikisha makundi yote katika jamii kama ilivyofanya Kenya baada ya kutokea mivutano ya kisiasa.

Serikali hiyo mpya, pia inatakiwa kumaliza migawanyiko ya kikabila na kikanda ili kuifanya Burundi kuwa nchi yenye umoja, amani, uzalendo na utaifa kwa kila raia.

Uchaguzi wa Burundi unaofanyika, huku kukiwa na tishio la maambukizi ya virusi vya corona, ambapo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ikisema haitapeleka waangalizi wake kutokana na masharti yaliyotolewa na serikali ya nchi hiyo kuwa waangalizi watatakiwa karantini siku 14 ambazo zitamalizika wakati uchaguzi huo umeshafanyika.

Tume ya uchaguzi nchini humo, imesema waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa hawataruhusiwa kusimamia uchaguzi huo kutokana na changamoto ya maambukizi ya virusi vya corona.

Mchambuzi wa masuala ya siasa na diplomasia, Abbas Mwalimu, alisema ni kiashiria cha kuelekea demokrasia ya kweli katika nchi hiyo licha ya kuwapo kwa changamoto ya shinikizo ya masuala mbalimbali kutoka jamii ya kimataifa.

“Inaonekana bado kutakuwa na changamoto katika amani kutokana na masuala ya kisiasa, lakini ni vema watakaoshika madaraka kuhakikisha nchi inakuwa na amani kwa kuitisha mjadala wa kitaifa ili kuwezesha wananchi kueleza changamoto zilizopo zinazosababisha vurugu za mara kwa mara.”

“Lakini pia ni vema kuunda tume ya maridhiano kama walivyofanya Kenya baada ya migogoro ya kisiasa ili kuondoa tofauti zilizopo, huku kukiwa na msimamizi wa tume hiyo anayekubalika na pande zote,” alisema.

Alitaka EAC kutumia uwezo wake kuimarisha usalama katika nchi hiyo ili kuwapo na utulivu wa kisiasa na ukanda huo usiathirike na kusambaa kwa silaha au machafuko mengine.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Faustine Bee, alisema uchaguzi ni njia sahihi ya kukomaza demokrasia, kupunguza misuguano ya kisiasa na kurejesha mahusiano ya kimataifa.

“Kuhusu waangalizi wa kimataifa kuzuiwa, hatuwezi kufahamu msingi wake, kwani mbali na kuhofia maambukizi ya virusi vya corona, kuna waangalizi wengine si wazuri,” alisema na kuongeza kuwa, pamoja na yote hayo, waangalizi wa uchaguzi huru ni muhimu kwani watatoa taarifa kuthibitishia kama ulikuwa huru na haki au la.

Alitaka serikali itakayoshika madaraka kuondoa migawanyiko ya kikabila na kikanda ili kujenga nchi yenye amani, uzalendo na utaifa kwa kila raia wa nchi hiyo.

Katika taarifa yake wiki iliyopita iliyokuwa na kichwa cha habari, ‘Kusitishwa kupeleka waangalizi kutoka EAC katika uchaguzi Mkuu Burundi mwaka 2020, , Katibu Mkuu wa EAC, Liberat Mfumukeko, alisema jumuiya hiyo imesitisha kupeleka waangalizi wake kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.
 
Quarantine fourteen days ya waangalizi wa uchaguzi ambazo zitaisha uchaguzi ukiwa umekwisha

Hii sarakasi sijawahi kuiona kwenye muvi yoyote iliyowahi kuigizwa na kina jackchen, van dame , Jet lee wala muvi yoyote ya kijasusi ya kina james bond au matt damon :D:D:D:D:D
 
Ni muda wa Kila nchi kusimama kivyake bila shobo za mabeberu, muda sio mrefu Africa tutasimama kwa miguu yetu na kutoa misaada kwa baadhi ya nchi nje ya Africa
 
HATIMAYE Uchaguzi Mkuu wa Burundi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na jumuiya ya kimataifa, utafanyika kesho, huku ukielezwa kuwa ni mwanzo mpya wa demokrasia katika nchi hiyo iliyokubwa na changamoto mbalimbali za kukosekana utulivu wa kisiasa na kijamii.

Hii aya unasema uchaguzi kufanyika kesho, kichwa cha habari uchaguzi kufanyika leo !! Ipi sahihi?
 
Wakileta ujinga wakaanza vurugu tena sisi bongo tunapata ajira kwenye mashirika ya kimataifa ya wakimbizi..
Kwahio choice ni yao , wafanye mambo kwa utaratibu waenjoy uhuru wao au walete vurugu waje bongo kuishi kwenye tents huku sisi tukifaidika na ajira.
 
Bado Mali za wizi tutanunua wabongo
 
Back
Top Bottom