Hatimaye bondia kutoka Ufilipino avalishwa gloves zenye rangi ya bendera ya Tanzania ya jiwe Tanzania ya viwanda

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
504
1,666
Live hapa kutoka uwanja wa taifa mabondia Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay wanavuliwa gloves zao zenye rangi nyeupe nakuvishwa zenye rangi ya bendera ya taifa la yeye mbarikiwa mtukufu alietukuka jiwe kweli kweli, na huku bondia Hassan Mwakinyo akionekana kuwekewa dawa katika gloves zake.

Namshukuru yeye aliye juu jiwe mwamba kwelikweli kwa kuruhusu ulozi utumike hadharani na sasa nasema Mwakinyo apigwe.
 
Kiukweli kwa aliyeshuhudia mpambano huu ameona jinsi mpambano ulivyokwenda. Labda wajuzi mtusaidie sababu iliyopelekea Hassan Mwakinyo kuibuka mshindi.
 
Unaona hata ushangiliaji ni wa kusuasua sana, hata Mwakinyo mwenyewe hanafuraha na ushindi wake.
 
Mleta mada hujui mchezo wa ngumi kaangalie marudio kisha uje utoe huu uchafu wako.

Ngumi za mfilipino zilikuwa hazina maana yoyote ile katika pointi, pia tizama ngumi za mwankinyo zilikuwa zinalenga kichwani.

Ngumi sio kupiga piga tu ili mradi, kuna maeneo muhimu ya kupiga.
 
Binafsi, nimeshuhudia pambano tangu mwanzo mpaka mwisho. Mwakinyo amezidiwa pointi na Mfilipino.

Mwakinyo kupewa ushindi sio kweli Mfilipino alimzidi karibu kila raundi. Tuwe na haki pambano hili Mwakinyo ameshindwa kwa pointi ingawaje amejitahidi sana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom