Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
Wakuu habari!
Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA) hatimaye limepata Sekretariet iliyokamilika na hivyo kuwa na Uongozi uliokamilika.Kikao Cha Kamati Tendaji Cha BAVICHA kilifanyika Siku ya Jumamosi tarehe 12 Nov Mjini Dodoma.Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Wenyeviti wa BAVICHA wa Mikoa,Viongozi Vijana wa Chama Taifa,Wawakilishi Watano wa Wabunge Vijana na Wawakilishi Watano wa Madiwani Vijana.
Katika Uchaguzi huo uliokuwa na mchuano mkali,wafuatao walichaguliwa;
1. Katibu Mkuu wa Baraza hilo Bwana Deogratius Munishi
2. Naibu Katibu Mkuu Bara wa Baraza hilo Bi Esther Daffa
3. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar bwana Suleiman Maabad
4. Mratibu wa Uhamasishaji au Katibu Mwenenzi wa Baraza hilo Bwana Rafiki Rufunga
5. Mwekahazina wa Baraza Bwana Mrisho Ramadhani
Mbali na Uchaguzi huo Kikao hicho pia kilijadili Hali ya Siasa nchini na mambo mengineyo.
Aluta Continua.
Hongera sana Munishi.
Hongera kanda ya kaskazini.
Hongera mkoa wa Kilimanjaro kutoa kiongozi.
Uzi ule ule