Hatimaye BASATA imewaruhusu wasanii Diamond na Rayvanny kuendelea na Tamasha lao la Wasafi Festival.

Freelancer Wakala

JF-Expert Member
Feb 6, 2016
1,193
825
Habari wakuu!!
Lile sakata la Diamond Platinumz na Rayvanny na Tamasha lao lilofungiwa hatimaye BASATA wamewaruhusu nchini Kenya na Comoro.
Ambapo rufaa yao itajadiliwa February mwakani 2019.
Katika Ratiba yake Diamond na Tamasha lake la Wasafi Festival tarehe 24 desemba 2018 wako Kenya uko mji wa Embu na kabla ya kuamia Jiji la Mombasa 26 desemba 2018.
Na kuelekea show ya Comoro 28/12/2018 na kumalizia Nairobi 31 desemba 2018.
Diamond na Rayvanny walifungiwa 18 desemba 2018,wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali tangu kuanza kwa Tamasha la Wasafi Festival ikiwemo kuimba wimbo wa Mwanza Nyegezi ambao umefungiwa.
Hongera BASATA kwa uamuzi huu waliochukua.
#HawaaminiWanachoKiona.
#MchezoUsiuchezeeWewe
#Kabisaaaa
 
Hii nchi bwana!
Mbona walikua wanaendelea kupromote tamasha lao kama kawaida bila kujali kama wamepigwa kufuli na basata?

Kipindi kile Shonza amekomaa na roma masikini hadi huruma!
 
Dady is coming, jiwe na bashite wanamuhitaji mondi kwenye kampeni za 2020, ndiomaana hata juzi mwakyembe alipoulizwa kuhusu kufungiwa kwao alijiweka pembeni
 
Hatimae vita ya basata na diamond platnum mshindi aibuka, diamond platnum...... Mchezoo usiuchezeee wew hii nchi inawenyewe.....
 
Huwezi kutoa maamuzi magumu kama yale kwa kufuata ushauri wa mkeo, lazima utachemka tu.
 
Mwanazuoni mmoja wa Chuo cha sanaa Bagamoyo, amelidadavua hili swala kiundani sana, mimi nimekubaliana nae mia kwa mia. Hawa watu wana maamuzi ya kukurupuka kama baba yao lakini hawana wanalolijua.
 
IMG_7828.JPG

Barua ya Basata
 
Hii inathibitisha jambo moja kubwa.

Adhabu yao hakufanyiwa tafakari makini na wao wenyewe.

Walikurupuka, hawakuwa na utulivu wa kutosha kichwani wakati wanafanya uamuzi.

Binafsi bado najiuliza, kisheria hata kiitifaki Basata anahusika vipi kuingilia matamasha ya nje ya nchi.

Anawezaje kuingilia kamati za maandalizi za matamasha ya nje ya mipaka ya Tanzania?

Ikitokea Diamond anaalikwa Ufaransa au nchi isiyozungumza kabisa Kiswahili wala hawajui ilipo Nyegezi, bali mdundo wa muziki, bado nguvu zao za zuio zitakuwa na mantiki?

Katika hii nchi tunayo safari ndefu bado.
 
Okay huko kwenye kwenye ufanunuzi wakutafute uwanyoshee hizo sentence zao lakini mimi mlaji wa ndani wamenilinda sina shaka ati.

Hiyo Gabage wakalishe wakenya...

Huwezi kuniambia ufungue Pro-Gay Song uipige barabarani kisa eti umekua mbunifu saaana na unataka kuvuta hisia za soko la nje ya TZ lenye hela na gay wengi.

Fyekelea mbali na u-gay wako fyekelea mbali na utamaduni wa matusi hadharani...
Mwanazuoni mmoja wa Chuo cha sanaa Bagamoyo, amelidadavua hili swala kiundani sana, mimi nimekubaliana nae mia kwa mia. Hawa watu wana maamuzi ya kukurupuka kama baba yao lakini hawana wanalolijua.
 
Back
Top Bottom