Huu ni mbadala wa gari la zimamoto hasa uswazi ambako hakuna njia. Swali ni je hii bajaji inabeba maji kiasi gani?
Serikali ya Kikwete kiboko, haya sio masihara kweli??.
![]()
Jamani msiwe negative ( - hasi ) kiasi hicho – si kitu kizuri. Hapa wengi wenu mnakosoa tu na wengine mnaleta chuki za kibaguzi. Sikuona hata mtu mmoja amekuja na fikra tofauti ya kuboresha hiyo bajaj.
Mimi naona hii ni fikra nzuri ya kuanzia na baada ya matumizi utapatikana uzoefu wa kuboresha. Wote tunajua kuwa kitu muhimu sana katika uzimishaji wa moto ni kuwahi kufika na kuushambuliya. Hii bajaj itaweza kupita kwenya barabara finyu , Kufatana na bei yake nafuu zinaweza kutapakazwa sehemu mbali mbali vitongojini na kuweza kufika kwa haraka sehemu yenye moto.
Huu ndio uwezo wetu wa sasa na hii technologia ndio jawabu kwa hali yetu ya kipesa na kimakazi . tusiangaliwe wale wenye mabarabara mapana na magari makubwa ya zimamoto.
Kuwa negative sana ni kinyume na spirit of great thinkers.
Kweli bongo kila kitu kinawezekana.
tunapinga bila kufikiri...... HONGERA KAMPUNI MLIYOLETA BAJAJI KUZIMIA MOTO....! wanaopinga wanaishi masaki na oysterbay ambako kuna barabara za mpangilio, sisi kwetu MANZESE na watani zetu MWANYANYAMALA na TANDALE zitatufaa na kutusaidia.......! tena niliwashukurru nadhani DAWASCO walipoleta vibajaji vya kubeba maji kupunguza adha ya maji...! tena nawapa ushauri kwa kutoa ombi....!
ikiwezekana mtengeneze yenye uwezo wa kunyonya maji-taka kwani vyoo vyetu vinajaa na only option tuliyonayo ni kuvitapisha wakati wa mvua kwani magari ya kisasa yatakiwayo na wana-JF hayafiki huku kwetu kutikana na sisi wenyewe kujenga !