Hatimaye aliyekuwa Kigogo wa TRA Arusha asalimu amri, aripoti kazini

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
HATIMAYE ALIYEKUWA KIGOGO TRA ARUSHA ASALIMU AMRI,ARIPOTI KAZINI CHAPCHAP

MWANDISHI WETU,ARUSHA

HATIMAYE aliyekuwa meneja msaidizi wa mamlaka ya mapato(TRA) mkoani Arusha upande wa madeni ,Irene Hance amekubali yaishe na kuamua kuripoti kazini alikopangiwa wilayani Kahama na kisha kutambulishwa rasmi juzi.

Uamuzi huo unakuja zikiwa ni takribani wiki mbili zilizopita baada ya taarifa kudai kwamba kigogo huyo amekataa uhamisho kwenda wilayani Kahama ambako kituo chake kipya cha kazi kwa sababu ambazo hazijulikani.

Irene ni miongoni mwa vigogo 34 wa mamlaka hiyo waliobadilishwa kwenye vituo vya kazi nchi nzima muda mfupi mara baada ya Rais John Magufuli kumtumbua aliyekuwa kamishna wa TRA nchini,Charles Kicheeere.

Hatahivyo,tayari mrithi wa nafasi yake ,David Patrick Nyorobi aliyetokea jijini Dar es salaam ameshakabidhiwa ofisi na kutambulishwa rasmi mbele ya wafanyakazi na uongozi wa TRA siku ya jana Julai 4 mwaka huu.

Taarifa za uhakika zinadai ya kwamba Irene aliripoti wilayani Kahama siku mnamo Julai 3 mwaka huu mara baada ya juhudi zake za kuwashawishi mabosi katika ngazi za juu ili aendelee kubaki kwenye kituo chake cha zamani cha kazi kugonga mwamba.

“Alipokuwa kule makao makuu alikutana na viongozi wakubwa lakini walimweleza kwamba ama aende kwenye kituo chake cha kazi Kahama au akubali kuachia ngazi”kilisema chanzo cha habari

Meneja wa TRA wilayani Kahama,Warioba Kanire alipoulizwa taarifa za kuripoti kwa mtumishi wake hakuweza kukiri wala kukataa juu ya taarifa hizo huku akisisitiza kwamba waulizwe viongozi waliopo makao makuu ya TRA jijini Dar es salaam.

“Sasa mimi hayo siyawezi naomba uongee na makao makuu”alisema Kanire

Alipotafutwa Irene kwa njia ya simu ili kuthibitisha tarifa hizo alisema kwamba kazi anayoifanya ni kwa mujibu wa utaratibu na suala la uhamisho hilo halimhusu mwandishi kwa kuwa yeye sio afisa rasilimali watu kutoka taasisi ya TRA.

Kuripoti kazini kwa Irene kunahitimisha mjadala mpana ambao ulidumu kwa takribani wiki mbili katika mitandao ya kijamii mbalimbali ambapo baadhi ya watu wamesisitiza kwamba ni muda sasa umefika kwa watumishi wa serikali kuzingatia taratibu za kiutumishi ikiwa ni pamoja na kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwa mujibu wa sheria pindi serikali inapotangaza mabadiliko .

maxresdefault.jpg

Mwisho.
 
Punguza umbea kwa vitu visivyo na tija na uongo uongo kisa upate likes za JF.
Ulikuwepo pindi anaeleza yoote hayo huko TRA au wewe ndio genge la wakwepa kodi, au ulipigwa kibuti na huyo mrembo, au alikipokonya Mme, au alikuwa msimizi mzuri wa kazi kiasi cha kuzuia dili zako maaana siyo kwa kumganda hivyo mtoto wa kike kama huyo.
Fanya mishe zako hizo inshu za Kipuuzi mwachie Shigongo and Kampan
 
Dah...hii habari imenikumbusha yale magazeti ya udaku..ndo breaking news kama hizi
 
Hii habari naona wengi wameikomenti kama ya umbea umbea hivi a.k.a UDAKU.
 
Dada piga kazi kahama ni zaidi ya dar bado uko t.r.a wasikusumbue huwezi kusafiria nyota ya mtu hata ukimchafua kichere kaondoka Dada karipoti kituo cha kazi kipya wewe yanakuhusu nini ?
 
HATIMAYE ALIYEKUWA KIGOGO TRA ARUSHA ASALIMU AMRI,ARIPOTI KAZINI CHAPCHAP

MWANDISHI WETU,ARUSHA

HATIMAYE aliyekuwa meneja msaidizi wa mamlaka ya mapato(TRA) mkoani Arusha upande wa madeni ,Irene Hance amekubali yaishe na kuamua kuripoti kazini alikopangiwa wilayani Kahama na kisha kutambulishwa rasmi juzi.

Uamuzi huo unakuja zikiwa ni takribani wiki mbili zilizopita baada ya taarifa kudai kwamba kigogo huyo amekataa uhamisho kwenda wilayani Kahama ambako kituo chake kipya cha kazi kwa sababu ambazo hazijulikani.

Irene ni miongoni mwa vigogo 34 wa mamlaka hiyo waliobadilishwa kwenye vituo vya kazi nchi nzima muda mfupi mara baada ya Rais John Magufuli kumtumbua aliyekuwa kamishna wa TRA nchini,Charles Kicheeere.

Hatahivyo,tayari mrithi wa nafasi yake ,David Patrick Nyorobi aliyetokea jijini Dar es salaam ameshakabidhiwa ofisi na kutambulishwa rasmi mbele ya wafanyakazi na uongozi wa TRA siku ya jana Julai 4 mwaka huu.

Taarifa za uhakika zinadai ya kwamba Irene aliripoti wilayani Kahama siku mnamo Julai 3 mwaka huu mara baada ya juhudi zake za kuwashawishi mabosi katika ngazi za juu ili aendelee kubaki kwenye kituo chake cha zamani cha kazi kugonga mwamba.

“Alipokuwa kule makao makuu alikutana na viongozi wakubwa lakini walimweleza kwamba ama aende kwenye kituo chake cha kazi Kahama au akubali kuachia ngazi”kilisema chanzo cha habari

Meneja wa TRA wilayani Kahama,Warioba Kanire alipoulizwa taarifa za kuripoti kwa mtumishi wake hakuweza kukiri wala kukataa juu ya taarifa hizo huku akisisitiza kwamba waulizwe viongozi waliopo makao makuu ya TRA jijini Dar es salaam.

“Sasa mimi hayo siyawezi naomba uongee na makao makuu”alisema Kanire

Alipotafutwa Irene kwa njia ya simu ili kuthibitisha tarifa hizo alisema kwamba kazi anayoifanya ni kwa mujibu wa utaratibu na suala la uhamisho hilo halimhusu mwandishi kwa kuwa yeye sio afisa rasilimali watu kutoka taasisi ya TRA.

Kuripoti kazini kwa Irene kunahitimisha mjadala mpana ambao ulidumu kwa takribani wiki mbili katika mitandao ya kijamii mbalimbali ambapo baadhi ya watu wamesisitiza kwamba ni muda sasa umefika kwa watumishi wa serikali kuzingatia taratibu za kiutumishi ikiwa ni pamoja na kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwa mujibu wa sheria pindi serikali inapotangaza mabadiliko .

View attachment 1147384

Mwisho.
Kigogo anawanyooshaaa2014
 
Mleta uzi mtu wa majungu sana unaonekana alafu unaonekana bingwa wa kujipendekeza kwa wakubwa. Huyu dada mbona mtu poa sana why such hate aisee wabongo bwana
 
Bibi kali afu ina mpunga na position nzuri.

Wanaume bado tuna safari ndefu sana.
 
Back
Top Bottom