Hatimae: Serikali kutangaza zabuni mradi wa kufua Umeme mto Rufiji(Stiegler's Gorge) keshokutwa

Huu ndo mchakato ambao sera ya manunuzi ya serikali inataka ufuatwe hivi. Siyo yale ya kukurupuka fro nowhere unatangaza "baada ya wiki iwepo kampuni ya ujenzi hapa na vifaa vikiwa tayari"
 
Hapa kazi tu

Magufuli oyeeee
Kwa hiyo ndio kusema gesi ya ntwara kumbe ni mradi hewa na hauwezi kuzalisha kiasi hicho cha megawati zitakazozalishwa hapo rufiji???

Hii nchi hii kwa kweli inaudhi sana
Link Gesi asilia inavyofungua njia kwa Watanzania kuagana na umaskini

Akielezea mikakati ya upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imeandaa mpango wa matumizi ya vyanzo vya nishati ya umeme ambapo gesi ni asilimia 40, maji asilimia 25, makaa ya mawe asilimia 30 na nishati mbadala asilimia 5.

Link Nishati ya uhakika kutokomeza umasikini–Prof. Muhongo — Ministry of Energy and Minerals

Link Pinda: Bomba la gesi kukamilika mwaka huu
 
Bwana yule kanunua mwenyewe tenda kabeba mwenyewe. Ndiyo sababu ni lazima CAG akague kila kitu kuhusiana na ununuzi wa ndege na kiasi kilichochotwa hazina bila idhini ya Bunge. Ni lazima tu atagundua uozo chungu nzima.

Mbona zabuni za ununuzi wa Bombadia hawakutangaza kwa umma?
 
Haya mambo ndo yanayotakiwa, Magufuli always walks the talk.

Ni kweli, kama alivyofanya kwenye 50m@kijiji. Ile ahadi mpaka kwenye bajeti yake ya kwanza ilikuwepo na haikutoka hata sent. Sasa leo ahadi nyingine mnashangilia kama mazwazwa.
 
Alafu wale Nyumbu utasikia hakuna kinachofanyika, utasikia kila siku anateua na kutengua

Unatukana kama hicho kilichotangazwa kimeshafanyika!! Kutangazwa kwa tenda ni jambo moja na utekekezaji ni jambo jingine boss. Unakumbuka 50m@kijiji? Leo hii unaweza kuja kutukana hapa kwa hilo?
 
shukuru Mungu hata kwa hicho kidogo kilichopatikana, mengine waachie wanasiasa.

Nishukuru kwa lipi ilhali nchi inaliwa kipuuzi puuzi na wahusika wanaangaliwa tu,kazi ni kuwabana wapinzani tu,wezi wanaoiingiza nchi kwenye matatizo kama haya wanaangaliwa tu,huu ni uzwazwa wa hali ya juu sana,sikutegemea mradi wa gesi uliopigiwa chepuo la nguvu na wanasiasa ungeangukia pua kiasi cha kushindwa kuzalisha hizo megawati,napata hisia hata huu wa rufiji utakuwa ndio kama ule wa mtwara tu
 
Link Gesi asilia inavyofungua njia kwa Watanzania kuagana na umaskini

Akielezea mikakati ya upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imeandaa mpango wa matumizi ya vyanzo vya nishati ya umeme ambapo gesi ni asilimia 40, maji asilimia 25, makaa ya mawe asilimia 30 na nishati mbadala asilimia 5.

Link Nishati ya uhakika kutokomeza umasikini–Prof. Muhongo — Ministry of Energy and Minerals

Link Pinda: Bomba la gesi kukamilika mwaka huu

Hizo link hazina lolote kwa hili linalilotokea sasa nchini kwetu,ni dhahiri shairi kwa sasa gesi iliyopigiwa chepuo na wanasiasa kuwa itakuwa ndio mkombozi na tatizo la umeme litakuwa historia nchini kwetu imefeli,kuna watu wanatakiwa wanyongwe kabisa kulipia hasara waliyoingiza katika suala hili,hawastahili kuendelea kutumalizia hewa yetu wakati washatutia hasara kubwa sana inayoitafuna nchi miaka mingi sana
 
Kwa hiyo ndio kusema gesi ya ntwara kumbe ni mradi hewa na hauwezi kuzalisha kiasi hicho cha megawati zitakazozalishwa hapo rufiji???

Hii nchi hii kwa kweli inaudhi sana
Umeme haubanani ndugu, gas ya mtwara imejengewa na inaendelea kujengewa mitambo ya kufua umeme pale kinyerezi. Vivyo hivyo na huu mradi pia tunauhitaji tena sana tu. Hata tukizalisha 10,000mw itakuwa ni vyema tu.
 
Link Gesi asilia inavyofungua njia kwa Watanzania kuagana na umaskini

Akielezea mikakati ya upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imeandaa mpango wa matumizi ya vyanzo vya nishati ya umeme ambapo gesi ni asilimia 40, maji asilimia 25, makaa ya mawe asilimia 30 na nishati mbadala asilimia 5.

Link Nishati ya uhakika kutokomeza umasikini–Prof. Muhongo — Ministry of Energy and Minerals

Link Pinda: Bomba la gesi kukamilika mwaka huu
Hongera na ubarikiwe ndugu kwa kuwaelewesha hawa watu
 
Hizo link hazina lolote kwa hili linalilotokea sasa nchini kwetu,ni dhahiri shairi kwa sasa gesi iliyopigiwa chepuo na wanasiasa kuwa itakuwa ndio mkombozi na tatizo la umeme litakuwa historia nchini kwetu imefeli,kuna watu wanatakiwa wanyongwe kabisa kulipia hasara waliyoingiza katika suala hili,hawastahili kuendelea kutumalizia hewa yetu wakati washatutia hasara kubwa sana inayoitafuna nchi miaka mingi sana
Achana na exaggeration za wanasiasa ndugu. Chamuhimu ni kuwa miradi hio ipo na inaendelea kutekelezwa.
 
..semeni mnajitangazia sabuni...maana tayari MNA watu wenu mtawapa tender hii...,huku kutangaza ni magumashi tu..tena mwisho wa siku mtapokea hata 10% kwa mtakayempa...au tayari mmeshapokea...hatudanganyikiiiii.....serikali ya ccm tunaijua....
 
Achana na exaggeration za wanasiasa ndugu. Chamuhimu ni kuwa miradi hio ipo na inaendelea kutekelezwa.

Mkuu,kuchukulia mambo yenye maslahi mapana kwa Taifa kiuwepesi wepesi ndipo kulipolifikisha Taifa letu hapa lilipo,lazima tuhoji kwa sauti ili yaliyopita yasije kujirudia tena ilhali fedha za umma ndio zishapotea
 
Mambo ndio haya sasa
FB_IMG_1504118852304.jpg
FB_IMG_1504119206881.jpg
FB_IMG_1504119216580.jpg
FB_IMG_1504119231388.jpg
FB_IMG_1504119241647.jpg
FB_IMG_1504119256667.jpg
 
Back
Top Bottom