Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Ujue tatizo la hoja ni kwamba haifi hadi amma ijibiwe, au ikubalike na kufanyiwa kazi. Huo ndio uzuri au ubaya wa hoja.Hoja haifi kwa kumpiga ngumi mtoa hoja.
Nyuma hapo, kuna kipindi ambapo yalikuwa yanajitokeza mambo ambayo kwa mtu mwenye busara na akili ya wastani tu, kusimama hadharani kuyatetea ueleweke unaongea nini ilikuwa ni ngumu sana.
Sasa hatimae katika awamu hii ya sita, mtu unaweza kusimama with ‘High confidence’ na ukajibu hoja yoyote ile ya wapinzani (logically) ikiwemo hoja ya katiba mpya na asitokee mtu mwenye hoja mbadala yenye nguvu.
Hii imewezekana kwa sababu awamu hii inafanya siasa za kisayansi. Inafanyia kazi hoja za msingi bila kujali nani katoa na inatanguliza dhamira njema kwa watu wote na kwa taifa kupitia (4Rs) na mabadiliko yanaonekana kwa uwazi sana.
Hoja pekee waliyobaki nayo upinzani ni ‘katiba mpya’ hata hivyo, nayo pia iko kwenye 'pipeline' kwa maana kwamba inatengenezewa utaratibu mzuri ambao utatusaidia kupata katiba bora na kwa right timing. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema inafanyiwa kazi kisayansi na sio kwa mihemko. Hivyo, hadi sasa hakuna tena hoja hapo.
Hii ndio siasa ya kisasa ambayo tumekuwa tunaipigania siku nyingi, yaani hoja inajibiwa kwa hoja, hoja nzuri zinapokelewa na kufanyiwa kazi, tunasonga mbele kama taifa bila kuumizana.
Tuendelee kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa kila mtu kutekeleza wajibu wake kulingana na mazingira na uwezo wake ili kufanikisha reforms zinazoendelea na ili tuweze kuifikia Tanzania tuitakayo mapema zaidi.