Hatimae muuaji manyumba akamatwa,ajipigilia msumali utosini .jijini mwanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimae muuaji manyumba akamatwa,ajipigilia msumali utosini .jijini mwanza.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by commonmwananchi, Jan 9, 2012.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  kijana mmoja anayejulikana kwa jina la warioba masaho a.k.a Manyumba.mkazi wa buzuruga/nyakato jijini mwanza,ambaye alikuwa akitafutwa baada ya kufanya mauaji katika kitongoji cha ustawi/buzuruga/jijini mwanza,ametiwa nguvuni na jeshi la polisi.
  Alifanya mauaji hayo mnamo tarehe 6/01/2012 kwa kuwashambulia kwa kuwachoma visu katika maeneo kadhaa mwilini, watu wawili katika eneo la ustawi/buzuruga jijini mwanza.
  Tukio ambalo lilipelekea mmoja wa majeruhi hao ajulikanae kwa jina la Ilida(msichana) kufariki dunia katika hospitali ya sekou toure jijini mza.
  Naye bwana manyumba baada ya kufanya tukio hilo alitoweka kusikojulikana na hatimae kutiwa nguvuni jana jioni baada ya jitihada za kumsaka kwa siku kadhaa bila mafanikio.
  Chanzo cha ugomvi huo ni mgogoro uliotokana na mahusiano ya kimapenzi na wote wakiwa wanafunzi katika shule tofauti za sekondari jijini mza.na walikuwa ni wakazi majirani katika eneo la makambini ustawi jijini mza.
  AJIDUNGA MSUMARI WA UTOSINI.
  Katika muendelezo wa matukio bwana manyumba akiwa na nia ya kujiua alijidunga msumari wa utosini kabla hajatiwa nguvuni na jeshi la polisi na hivi sasa anashikiliwa na jeshi la polisi huku akipatiwa matibabu katika hospitali ya bugando jijini mza.
  Habari hii ni kwa mujibu wa mashuhuda rasmi wa tukio .
  .
   
 2. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  duh msumari wa utosini,kha kama umeamua kujiua kwa nini utafute painful way hivyo,si angetumia hicho kisu alichotumia kuwaua wenzake? au aliogopa ?lol
   
Loading...