Hatimae Bodyguard Wa Milton Obote Arejea Uganda Kwa Familia Yake, Baada Ya Kujificha Tanzania Kwa Miaka 51

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
vicent-pic-data.jpg


Habari Wana Kijiji,

Siku ya tarehe 10, mwezi May mwaka 2021, majira ya mchana hisia zilikua juu katika kijiji cha "AGORA" nchini Uganda mara baada ya aliekua mlinzi (Bodyguard) wa aliekua Rais Dikteta Milton Obote, bwana "VINCENT OBODO" kurejea kwenye familia yake na kukutana na wake zake wawili (Waliojua mume wao alishafariki miaka mingi iliopita). Hii ni baada ya kujificha nchini Tanzania kwa miaka 51.

Kwa ufupi,

Mama Ariamo, ambae ni mke mkubwa, alisema walijua mume wao alishakufa kuanzia mwaka 1971 mara baada ya kutoweka kusikojulikana na kutokufanya mawasiliano ya aina yoyote na familia sambamba na marafiki zake.

Mzee Vincent Obodo, mlinzi binafsi wa aliekua Rais Dikteta wa Uganda, alikimbia mnamo January 1971, mara baada ya Rais Iddi Amin kufanya mapinduzi ya kiutawala wakati wakiwa nchini Singapore.

Hapo ndio ulikua mwisho wa wake zake bwana Vincent, Bi Ariamo (Umri 71) na Bi Anna Loyce Ideta (Umri 71) walipomuona mume wao kwa mara ya mwisho.

Wiwili hao, pamoja na watoto, ndugu, jamaa na marafiki waliangua vilio na kelele mara baada ya gari la UNHCR lilipofika kijijini kumrudisha mpendwa wao aliekua mafichoni nchini Tanzania.

Bi Ariamo, anasema "Mara baada ya Bwana Vincent kupotea, tulijaribu kila jitihada kutafuta taarifa zake kwa kuwasiliana na UPC (Udandan People Congress), ila jitihada hazikufua dafu, mpaka mwezi uliopita tulipopigiwa simu na Mbunge Jonathan Ebwalu Wa Mji Wa Soroti na kututaarifu kwamba mume wetu yupo hai na UNHCR wanafanya jitihada za kumrudisha nyumbani."

Bi Ariamo aliendelea kusema mara baada ya taarifa kutoka UNHCR, hisia zilikua juu sana kumwaza walipokumbuka enzi za ujana wake, kijana shupavu, mtegemezi wa familia, mshauri na mliwazaji wao.

Aliendelea kusema "Alitupenda kwa usawa, alikua mkarimu na mtu wa kumuongelea kwa mazuri aliekua boss wake Bwana Obote. Tunaamini ilikua ngumu kwake kufikia makubaliano na serikali iliofanya mapinduzi dhidi ya aliekua Boss wake, Bwana Obote.

Bwana Vincent, mwenye umri wa miaka 81, ndio mtu pekee aliekua mfuasi wa Rais Obote kurudi nchini Uganda akiwa bado mzima wa afya.

Bi Anna, mke wa pili, alisema kukutana na mumewe tena kumerudisha kumbukumbu nyingi sana za zamani pindi walivyokua vijana wadogo.

Alisema "Kurudi kwake tena ni vigumu kuamini, ila ndio amesharudi, tunawashukuru wale wote waliofanya jitihada hizi kumrudisha na kufanya makubaliano na utawala ulipo.

Aliongeza kusema, wao kama wake wa Bwana Vincent, walifanikiwa kupata watoto na wanaume wengine, ila hawakutoka nje ya nyumba alizowaachia mume wao.

Bwana John Ekoyu, mwenye umri wa miaka 56, mtoto wa Bwana Vincent, nae alisema alifanya mawasiliano na Tanzania alipokuwa akijua kwamba ameshafariki baba yake.

Aliendelea kusema "Taarifa zilinifikia kutokea Tanzania Mwezi Uliopita, April 2021, na haraka sana nikawafikishia taarifa hizo Mama yangu, dada zangu na kaka zangu. Hawakuniamini, na walihisi nimekumbwa na pepo la kumkumbuka mzee wetu.

Bwana John alisema, mara baada ya UNHCR kumrudisha mzee Vincent, aliweza kumtambua baba yake mzazi kwa kuangalia sura, macho, pua na rangi yake. Na alijua mtu aliempokea ni baba yake mzazi.

Aliongeza kusema, alianza kuwa kiongozi wa familia alipokua na umri wa miaka 10, jambo lililomlazimu kuwa mtafutaji wa familia na muangalizi mkuu. Anamshukuru mungu kwa kumrudisha baba yao tena katika maisha yao.

Pia anaomba serikali ya Uganda kufanya maandalizi ya kumsaidia kwa hali na mali mzee wao.

Story ya Bwana Vincent kuishia Tanzania,

Akikumbuka jinsi alivyofikia Tanzania, Bwana Vincent anasema,

"Obote hakuchukulia maanani report za kiintelijensia kwamba kuna mapinduzi yanataka kufanyika, alilazimisha kuendelea na safari ya kwenda Singapore. Siku iliofuatia, Serikali ilipinduliwa.

Ndege ilitua kwanza nchini Kenya, ambapo Julius Nyerere aliwasiliana nao waondoke haraka sana kwasababu ya usalama wa maisha ya Rais Obote.

Niliandaa kumpeleka boss wangu Tanzania kwaajili ya usalama wake, kutoka Jomo Kenyatta International Airport, na hapo ndio nikajikuta nipo nchini Tanzania.

Baada ya Obote kurudi madarakani, mimi nilibakia Tanzania kama mshauri wake wa nje mpaka alipopinduliwa tena.

Maisha ya ughaibuni ni mwiba, kwani yalinizuia kufanya mambo ambayo ningeweza kufanya nchini mwangu.


UNHCR walisema,


Bi Carol Kibuka Musoke, UNHCR Assosiate, urudisho wa Bwana Vincent umefanikiwa baada ya msaada mkubwa kutoka kwa serikali ya Tanzania na Uganda. Na maandalizi ya kuwarudisha wakimbizi zaidi kwenye mataifa yao na familia zao yanaendelea.
 
Huyu mzee lazima ana watoto wakubwa tu kwa sasa ingawa hakusema
La pili huenda na kadi anayo
Kwani hafanani na sisi?
Ila ana roho ngumu miaka yote hiyo
Mimi hata kwa kujificha ningeenda tu
Ila kama alipata toto la hapa likamchanganya sawaaa
 
Miaka 51 ni mingi sana, waeleze maisha yake ki uchumi na kijamii.
Hawa ni wale watu wanaolowea ugenini na kusahau kwao. Baada ya Iddi Amin kuondolewa alikuwa na chance ya kurudi kwao ila hakutaka. Hakutaka hata kufanya mawasiliano yoyote. Nadhani alikuwa amedhamiria ''kupotea'' kabisa na asifanye tena mawasiliano na watu wa nyumbani kwake lakini akaja kubadilisha mawazo.
 
Hawa ni wale watu wanaolowea ugenini na kusahau kwao. Baada ya Iddi Amin kuondolewa alikuwa na chance ya kurudi kwao ila hakutaka. Hakutaka hata kufanya mawasiliano yoyote. Nadhani alikuwa amedhamiria ''kupotea'' kabisa na asifanye tena mawasiliano na watu wa nyumbani kwake lakini akaja kubadilisha mawazo.
Wengine hupata mshtuko baada ya kuona watu waliokua nao kuuliwa au kufanyiwa unyama, wanaishia kuishi na makovu na uoga.

Mfano, alichofanyiwa Rais Doe, kukatwa mikono mbele ya vyombo vya habari na kisha kuuliwa. Nina amini aliokua nao kama walifanikiwa kutoroka basi hawakurudi tena nchini mwao.
 
Back
Top Bottom