Hatima ya watoto wa mitaani kwa taifa letu ni nini?

Massanda OMtima Massanda

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
1,056
561
Wangwana wa JamiiForums, mara nyingi tumekuwa tukishuhudia Asasi za Haki za Binadamu zikikosoa serikali kwa masuala yasiyokuwa na tija kwa mustakabali wetu! Kuna suala la msingi sana la watoto wa mitaani /chokoraa ambao hawana makazi, hawajui watakula nini, hawajui msamiati wa elimu una maana gani, nk. Kwa kifupi kwao leo ni afadhali ya jana na kesho itajijua yenyewe.

Je, Asasi hizi pamoja na serikali yetu wanatambua kwamba chokoraa au watoto wa mitaani hawa ni binadamu na hivyo hukua na kuwa watu wazima na hivyo kuzaliana? Je kizazi hiki kitakapotamalaki, kitakuwa ni kizazi cha aina gani katika taifa letu na kitakuwa na mchango gani kwa mustakabali wetu kama jamii ya Kitanzania?

Tushauri na kushauriana!
 
KAMA TUNGEKUWA NA UPENDO WA KWELI BASI KULIKUWA HAKUNA HAJA YA KUWA NA VITUO VYA WATOTO YATIMA.MAANA TUNGEWACHUKUA NA KUISHI NAO KATIKA NYUMBA ZETU.
 
Back
Top Bottom