Hatima ya vyama vyingi tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatima ya vyama vyingi tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by misha, Nov 26, 2010.

 1. m

  misha Member

  #1
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwinyi alianzisha sera ya RUKHUSA, sera hii ililenga kupunguza ukasi wa maisha kwa Watanzania,na pia alituonya kuwa 'ukifungua dirisha inzi pia huingia' pamoja na mabadiliko yaliyotokea katika nyanja mbalimbali vyama vyingi vya kisiasa vilianzishwa baada ya sera za rukhusa,hayati Nyerere alitamka kuwa 'vyama vyingi siyo dhambi'; kwa maoni yangu vyama vyingi siyo dhambi chini ya rukhusa nje ya hapo haiji,mfano Wasabato,Waislamu,Wayahudi kula nyama ya nguruwe ni haram; kwa maneno mengine nyama ya nguruwe siyo chakula halali kwa waumini wa dini hizi. Maisha ya muumini yanapokuwa hatarini ni rukhusa kuyanusuru na kama njia pekee ya kuyanusuru ni kwa kutumia nyama ya nguruwe-katika hali hii ya kunusuru maisha ya mtu nyama ya nguruwe siyo chakula tena- siyo dhambi.
  Misingi na nguzo za siasa Tanzania zinakinzana na siasa ya vyama vingi; sababu kuu zilizotolewa na Rais Mstaaf Mwinyi kwa Wananchi hazina nafasi tena kwani hali imebadilika namitazamo nayo imebadilika ni wakati wa kurudi kwenye misingi na ukweli wetu
   
Loading...