Hatima ya tanzania....nyerere aliwatabiria vipi 'watawala' wetu hawa?? Wao wanalijua?

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
1,304
Points
0

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
1,304 0
HATIMA YA TANZANIA....Kitabu cha Mwalimu Nyerere kilishatuambia...

"....
Plato, Myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu: kwanza, Wana uwezo wa kutawala, na pili, hawapendi kutawaIa. Kwa hiyo, Jamhuri ya Plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazozipenda.

Lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa Plato; watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kuwa watawala...."


Tumeyaona, TuNayaona na Tutaendelea kuyaona....'Watawala' ndio wanaoamu kuondoka wenyewe na sio uamuzi wa wananachi!

JE!...Watanzania tunao uwezo wa kusema HAPANA?
Nawasilisha!

View attachment UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.doc
 

Forum statistics

Threads 1,389,736
Members 528,016
Posts 34,032,946
Top