marshal
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 353
- 158
Habari za Kuaminika za kichunguzi zinaonesha kuwa kuna mtoto wa aliekuwa waziri wa maliasili na utalii kupewa nafasi kama administrator katika ofisi za bodi ya utalii Tanzania bila kufuata taratibu za ajira.Aidha nafasi hiyo ilikuwa na mtu ambae alifukuzwa kazi(terminated) bila kupewa sababu za kufukuzwa kazi kama sheria na taratibu za utumishi zinavyohitaji.Na kabla ya mtu huyo(aliefukuzwa) hajamaliza muda wake wa notisi aliyopewa tayari mwanadada(mtoto wa waziri) alikuwa kisha take over.Maisha ya watanzania yako rehani kwa vigigo wachache wenye uchu wa kuifanya nchi hii kuwa ya kwao. I was sympathetic kwa huyu dada aliefukuzwa kazi maana ni yatima na analea wadogo zake kwa kazi hiyo aliyokuwa akifanya!Sasa watoto wa vigogo wanchukua nafasi za yatima na kuyafanya maisha yao yawe ya dhiki ya kutupwa! kwenu wana JF,leo wamechukua ajira ya yatima huyu kesho ni yangu na keshokutwa ni wewe!!