Hatima ya jimbo la Sumbawanga mjini mashakani

Ptz

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
541
500
Wakuu shalom! Jana tar 30 Novemba 2012 katika mahakama kuu kanda ya Sumbawanga, ilitolewa ruling kuhusu hoja ya bw Aeshi aliyevuliwa ubunge kwa kukutwa na kasoro katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu mwaka 2010 uliompatia ubunge, kasoro hizo ilikuwa ni kwa bw Aeshi kujihusisha na rushwa na uchochezi wa uvunjifu wa amani katika mikutano kadhaa ya mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema mzee Yamsebo.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 mgombea wa Chadema mzee Yamsebo alifungua kesi kulalamikia uvunjifu wa sheria ya uchaguzi uliofanywa wakati wa uchaguzi mkuu uliomuweka bw Aeshi kuwa mbunge, hukumu ya kesi hiyo ilitolewa Mwezi April mwaka huu kwa kutengua ubunge wa bw Aeshi, kilichofuata ni kwa bw Aeshi kukata rufaa mahakama kuu, walipangiwa majaji watatu ruling iliyotolewa ni kuwa rufaa ilikuwa batili na hivyo kutupwa chini kwa kukosa sifa za kusikilizwa. Lakini baadaye Bw Aeshi alitoa kitu inatwa Certificate of Agency kwa uelewa wangu baada kufuatilia kwa ukaribu nikaambiwa kinachokusudiwa ni kuwa hoja hiyo inataka kesi ianze upya kwa kutupiliwa mbali hukumu ya kuvuliwa ubunge.

Sasa jana 30/11/2012 ruling ilitolewa na kuwa bw Aeshi kapewa siku 14 kukabidhi vielelezo vyake ilikusudi hoja yake ianze kufanyiwa kazi na mahakama. Na zaidi nachojua ni kuwa huyu bw Aeshi ni corrupted sana ni moja kati ya mafisadi wenye pesa chafu, huwa yuko radhi hata kuua ili anachotaka kitimie.

Naomba sasa kuuliza ni nini hatima ya jimbo la Sumbawanga mjini, je, hii hoja kisheria inamaanisha nini, ni mahakama ipi itasikiliza hoja hii, je, mahakama kuu au ya rufaa? kwa mwenye kuelwa please.
 

Kimweli

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
899
250
Ningekuwa mimi ningekubali tu uchaguzi urudiwe. Jamaa hawa ni hatari sana wanapenda madaraka sana. Ni kweli atahonga sana mpaka malori na sheri atahonga. Ila haki huwa haidhurumiwi akae akijua kama wanasumbawanga wanampenda watampa, ila inavyoonekana hapendwi that why he is doing this
 

Kasent

Member
Sep 27, 2011
57
0
Ptz Naona mtoa mada amejaa chuki na ndg Aeshi.hapo nijuwavyo mimi mahakama imempa haki kama wapeavyo wengine. Pili akishinda mtu wa chadema hapo haki ipo.akishinda wa ccm hapo rushwa sasa sijuwi haki ipo kwa chadema tu? Hebu kuweni wastarabu msiwe kama malimbukeni.
 
Last edited by a moderator:

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
0
I didnt understand what is that?

Inawezekanaje kesi ifike mpaka mahakama ya Rufaa na kutolewa hukumu halafu inarudi chini tena anaanza upya? Hii ni mpya sana kwangu.

Any way mimi sio mtaalam wa sheria, wajuvi ngoja watuelimishe haya mambo.

What is certificate of Agency?
What is the importance of it?
 

Mkuu rombo

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
1,556
1,225
aiseeeeeee babaangu ngoja niwaachie nafasi wakongwe wa jf waje wateme data
 

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,047
2,000
Kesi yake itasikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani. Kesi yake itasikilizwa tu endapo vielelezo vyake vitakuwa na sifa.
 

ojoromong'o

Member
Nov 6, 2012
91
125
Naona mtoa mada amejaa chuki na ndg Aeshi.hapo nijuwavyo mimi mahakama imempa haki kama wapeavyo wengine. Pili akishinda mtu wa chadema hapo haki ipo.akishinda wa ccm hapo rushwa sasa sijuwi haki ipo kwa chadema tu? Hebu kuweni wastarabu msiwe kama malimbukeni.

...haya basi wewe ambaye si limbukeni tufafanulie certificate of Agency nini?...
 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,365
2,000
Kisheria kesi ikitolewa maamuzi mahakama ya chini haiwezi tena kurudishwa kwenye mahakama hiyo hiyo kwa kesi ile ile na madai yale yale isipokuwa itapelewa kwenye mahakama ya rufaa ama kutengue uamuzi wa mahakama ya chini au kubariki maamuzi hayo!Jamhuri inaweza irudisha kesi iliyotolewa uamuzi kwenye mahakama hiyo hiyo lkn LZM WABADILISHE AINA YA MASHTAKA!

"Certificate of Agency"ktk kesi ya Aeshi vs Yamsebo ni kujaribu kuharakisha tu kurudiwa upya kunyambuliwa kwa vielelezo vyake vilivyokataliwa na Mahakama ya rufaa kama havina sifa vya kufanya kesi hiyo isikilizwe na mahakama hiyo!

Sio kila kesi iliyokatiwa rufaa basi mahakama ya rufaa inaichukua!Lzm uwa-convince kisheria kuwa mahakama ya chini ilikosea.
 
  • Thanks
Reactions: Ptz

Ptz

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
541
500
Ptz Naona mtoa mada amejaa chuki na ndg Aeshi.hapo nijuwavyo mimi mahakama imempa haki kama wapeavyo wengine. Pili akishinda mtu wa chadema hapo haki ipo.akishinda wa ccm hapo rushwa sasa sijuwi haki ipo kwa chadema tu? Hebu kuweni wastarabu msiwe kama malimbukeni.

Sikosa lako umetumwa! labda nikueleze kuwa kumtetea Aeshi kwa hili inahitaji uwe na akili mfu. Unaifahamu kweli haki au unaropoka tu. Nakuomba utoe hoja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom