Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,754
Heshima mbele wakuu..Kufuatia Askari watatu waliokuwa miongoni mwa watuhumiwa katika kesi inayomhusu ACP Abdallah Zombe na wenzake kuachiwa huru na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Salum Masati(baada ya kutokutwa na hatia)...Kinachonitatiza mimi ni je,ni nini hasa hatma ya Askari hawa CPL.Nyngerela Morris,PC.Noel Leonard na PC.Felix Sandeys???,wanaweza kurudishwa kazini???(sheria inasemaje kuhusu hili,mimi sijui hapa jamani),vipi kuhusu mafao yao na mishahara yao kwa kipindi chote walichokuwa mahabusu????...Na mwisho je,wanaweza kufungua kesi ya madai kutaka walipwe fidia kwa kipindi chote walichokaa mahabusu wakituhumiwa kwa makosa ambayo Mahakama Kuu imethibitsha kwamba hawakuyafanya????...Naomba msaada katika haya wakuu....Be blessed